title : NAIBU MKURUGENZI WA IMF AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI
kiungo : NAIBU MKURUGENZI WA IMF AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI
NAIBU MKURUGENZI WA IMF AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Tao Zhang amewasili nchini kwa ziara ya kikazi na kupokelewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), pamoja na Maafisa wengine waandamizi wa Serikali. katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Akiwa nchini, Tao Zhang, atafanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Ikulu Jijini Dar Es Salaam
Aidha, Zhang atawasilisha mtazamo wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF)kwa wadau hapa nchini kwa lengo la kuifanya Tanzania kuwa na maendeleo endelevu, kuimarisha uchumi mkubwa (Macroeconomy) na kuwa na uchumi shirikishi.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano Serikaini
Wizara ya Fedha na Mipango.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kulia) pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Amina Khamis Shaabani (kushoto) wakijadili jambo kabla ya kuwasili kwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Tao Zhang katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) anaeziwakilisha nchi 23 za Afrika, Bw. Maxwell Mkwezalamba (kushoto) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustino Mahiga, muda mfupi kabla ya kuwasili kwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Tao Zhang, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Katikati ni Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb).
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kushoto), akisikiliza jambo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) anaeziwakirisha nchi 23 za Afrika, Bw. Maxwell Mkwezalamba (kulia) katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere muda mfupi kabla ya kuwasili kwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Tao Zhang.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kushoto) na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Tao Zhang (kulia) wakifurahia jambo baada ya kusoma habari kuhusu ujio wa Zhang hapa nchini ambapo alikiri kutoa taarifa na kusudi la ujio wake zilizoandikwa na Gazeti la Daily News. Ni muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Tao Zhang (kulia) akiongozana na mwenyeji wake Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kushoto) baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (katikati) na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Tao Zhang (kushoto) waklipeana mkono walipofika katika moja ya Hoteli jijini Dar es salaam.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)
Hivyo makala NAIBU MKURUGENZI WA IMF AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI
yaani makala yote NAIBU MKURUGENZI WA IMF AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NAIBU MKURUGENZI WA IMF AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/05/naibu-mkurugenzi-wa-imf-awasili-nchini.html
0 Response to "NAIBU MKURUGENZI WA IMF AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI"
Post a Comment