Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar afungua mafunzo elekezi ya kuwajengea uwezo watendaji na viongozi wa majimbo ya CCM

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar afungua mafunzo elekezi ya kuwajengea uwezo watendaji na viongozi wa majimbo ya CCM - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar afungua mafunzo elekezi ya kuwajengea uwezo watendaji na viongozi wa majimbo ya CCM, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar afungua mafunzo elekezi ya kuwajengea uwezo watendaji na viongozi wa majimbo ya CCM
kiungo : Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar afungua mafunzo elekezi ya kuwajengea uwezo watendaji na viongozi wa majimbo ya CCM

soma pia


Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar afungua mafunzo elekezi ya kuwajengea uwezo watendaji na viongozi wa majimbo ya CCM

 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar  Dkt. Abdalla Juma Saadala akizungumza wakati wa mafunzo elekezi ya kuwajengea uwezo watendaji na viongozi wa Majimbo 9 ya CCM na jumuiya zake Mkoa wa Mjini Unguja.
Washiriki wa mafunzo hayo wakisikiliza kwa makini Nasaha za Mgeni rasmi  Dkt. Abdalla Juma Saadala huko ktk ukumbi wa Mkoa huo Aman Unguja.

NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar,  Abdalla Juma Saadala "Mabodi" amezitaka jumuiya za Chama hicho kutumia vizuri fursa ya uchaguzi kuwapitisha viongozi wenye sifa na uwezo wa kukiletea ushindi chama katika Uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Kauli hiyo ameitoa wakati akifungua mafunzo elekezi ya kuwajengea uwezo viongozi wa majimbo Tisa (9) ya Chama na Jumuiya za Mkoa wa Mjini juu ya mabadiliko ya Katiba ya CCM ya 1977 yaliyofanyika hivi karibuni yaliyofanyika Katika ukumbi wa mkoa huo Aman Unguja.

Alisema uchaguzi  unaofanyika hivi sasa katika kwa ngazi mbali mbali za Chama hicho ndio uwanja wa kuandaa jeshi kamili la kisiasa lililokamilika kila idara na lenye ujuzi na mafunzo yote ya vita ya kisiasa litakaloweza kupambana kwa ujasiri na kufanikisha ushindi katika uchaguzi mbali mbali za Dola ili CCM iendelee kushinda na kutawala kupitia utaratibu wa Kidemokrasia.

Aliwasihi washiriki wa mafunzo hayo kutumia vyema mafunzo hayo ya siku moja ili waweze kuwa na uelewa mpana wa Mabadiliko kadhaa yaliyofanyika ndani ya katiba ya CCM ili watekeleze kwa ufanisi majukumu yao na kuwaelimisha wanachama wengine juu ya taaluma hiyo.

Dkt.Mabodi alieleza kwamba matarajio ya taasisi hiyo ya kisiasa ni kuona   kasi ya mabadiliko ya kiutendaji kwa haraka hasa kwa viongozi na watumishi wa Chama na jumuiya zake.

Pia aliongeza kwamba mbali na matarajio hayo mafunzo hayo yatamaliza mizozo na malalamiko yaliyokuwa yalisababisha kutokuwepo kwa ufanisi mzuri wa kiutendaji kwa baadhi ya maeneo ndani ya Mkoa huo.

Naibu Katibu Mkuu huyo alisema hatovumilia tabia za kupangwa safu za viongozi  kwani kufanya hivyo ni kukiuka Kanuni za maadili na miongozo ya uchaguzi huo.

" Tumekuwa tukisema siku zote kuwa CCM ndio mwalimu wa Demokrasia yaani hivyo vyama vya upinzani demokrasia na ustaarabu wa kisiasa tumewafunza sisi hivyo dhana hizo lazima tuzisimamie na kuzitekeleza kwa vitendo kupitia uchaguzi unaoendelea ndani ya taasisi yetu.", alisema Dkt.Mabodi na kuzitaka kamati za uchaguzi na maadili kufuatilia kwa kina mwenendo wa uchaguzi na watakapobaini kasoro watoe taarifa kwa ngazi husika ili zitafutiwe ufumbuzi wa haraka.

Alifafanua kwamba kupitia uchaguzi huo panatakiwa kupatikana viongozi na watendaji watakaoendeleza siasa za upendo, maendeleo, umoja pamoja na mshikamano unaojali misingi ya kidemokrasia ndani na nje ya taasisi hiyo.
Hata hivyo alieleza dhamira ya chama hicho kupitia mabadiliko yaliyofanyika katika Katiba ya Taasisi hiyo kuwa ni pamoja na kila mwanachama kujipanga kisaikolojia kusaidia kuimarisha uchumi wa CCM kupitia rasilimali zilizopo sambamba na kubuni miradi mingine ya kimaendeleo.

Sambamba na hayo kupitia Mafunzo hayo Dkt.Mabodi aliwakumbusha washiriki hao kwamba ili wafanikiwe katika utendaji wao ni lazima watumie vizuri rasilimali watu ya wazee wa CCM pamoja na wastaafu katika sekta za umma na binafsi kwani wana uwezo na uzoefu mkubwa  wa kushauri na kutoa maelekezo mazuri juu ya masuala mbali mbali ya kiutendaji ndani ya Chama hicho.

Mapema akizungumza katika mafunzo hayo Mwenyekiti wa Mkoa huo, Nd. Bora afya Juma Silima alisema Mkoa huo umejipanga kufanikisha kwa ufanisi uchaguzi huo ili kulinda historia ya chama hicho katika kufanikisha uchaguzi unaoheshimu misingi ya utawala bora na demokrasia kwa wananchi wote.


Hivyo makala Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar afungua mafunzo elekezi ya kuwajengea uwezo watendaji na viongozi wa majimbo ya CCM

yaani makala yote Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar afungua mafunzo elekezi ya kuwajengea uwezo watendaji na viongozi wa majimbo ya CCM Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar afungua mafunzo elekezi ya kuwajengea uwezo watendaji na viongozi wa majimbo ya CCM mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/05/naibu-katibu-mkuu-wa-ccm-zanzibar_23.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar afungua mafunzo elekezi ya kuwajengea uwezo watendaji na viongozi wa majimbo ya CCM"

Post a Comment