MV. NYERERE KUFUNGWA INJINI MPYA

MV. NYERERE KUFUNGWA INJINI MPYA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MV. NYERERE KUFUNGWA INJINI MPYA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MV. NYERERE KUFUNGWA INJINI MPYA
kiungo : MV. NYERERE KUFUNGWA INJINI MPYA

soma pia


MV. NYERERE KUFUNGWA INJINI MPYA

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Iddi Mgwatu, ametembelea na kukagua kivuko cha MV. Nyerere kinachotoa huduma kati ya Bugorola na Ukara katika kisiwa cha Ukerewe mkoa wa Mwanza na kujionea utendaji kazi wa kivuko hicho pamoja na changamoto zake.

Akiongea na watumishi wa kivuko hicho baada ya kujionea changamoto ya uendeshaji wa kivuko hicho, Dkt. Mgwatu alisema “tutanunua injini mbili mpya na kukifanyia matengezo ya kinga kivuko hiki ili kuongeza zaidi ufanisi wake na hatimae kiweze kusafirisha abiria na mali zao kwa haraka zaidi na katika hali ya usalama mkubwa kwani injini zilizoko sasa zimechoka hivyo kushindwa kuendesha kivuko ipasavyo.”

Aidha Dkt. Mgwatu aliwataka watumishi wa kivuko cha MV. Nyerere kufanya kazi kwa bidii sambamba na kuziba mianya ya uvujaji wa mapato ya serikali, pamoja na kuzingatia weledi na uadilifu katika utendaji wa kazi.

Katika hatua nyingine, Dkt. Mgwatu alitembelea kivuko cha MV. Mara katika Mkoa wa Mara pamoja na kivuko cha MV. Ruvuvu katika mkoa wa Kagera na kujionea utendaji kazi wa vivuko hivyo pamoja na changamoto zake.
Kivuko cha MV. Nyerere kinachotoa huduma kati ya Bugorola na Ukara katika kisiwa cha Ukerewe mkoani Mwanza.
Fundi wa kivuko cha MV. Nyerere akionyesha utendaji wa injini mojawapo ya kivuko cha MV. Nyerere kinachotoa huduma kati ya Bugorola na Ukara katika kisiwa cha Ukerewe mkoani Mwanza. Nyuma yake ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Iddi Mgwatu.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Iddi Mgwatu (wa pili kushoto) akiangalia utendaji kazi wa moja ya injini ya kivuko cha MV. Nyerere katika chumba cha mifumo ya kuendeshea kivuko hicho. Kivuko cha MV. Nyerere kinatoa huduma kati ya Bugorola na Ukara katika kisiwa cha Ukerewe mkoani Mwanza.
Kivuko cha MV. Mara kinachotoa huduma kati ya Iramba na Majita mkoani Mara.
Kivuko cha MV. Ruvuvu kinachotoa huduma katika eneo la Rusumo Mkoani Kagera. Picha na Theresia Mwami.


Hivyo makala MV. NYERERE KUFUNGWA INJINI MPYA

yaani makala yote MV. NYERERE KUFUNGWA INJINI MPYA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MV. NYERERE KUFUNGWA INJINI MPYA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/05/mv-nyerere-kufungwa-injini-mpya_14.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MV. NYERERE KUFUNGWA INJINI MPYA"

Post a Comment