title : Mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (Mviwata) walalamikia ushuru wa mazao
kiungo : Mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (Mviwata) walalamikia ushuru wa mazao
Mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (Mviwata) walalamikia ushuru wa mazao
Mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (Mviwata), umelalamikia tozo, ushuru wa masoko na tozo za kusafirisha kwa gunia badala ya kutozwa kwa uzito, kwani hujenga mazingira shawishi kwa wanunuzi na madalali kuzidisha uzito wa vifungashi zaidi ya kiwango stahiki.
Mratibu wa Mviwata mkoani Manyara, Martin Pius alisema hayo mjini Babati kwenye warsha ya uboreshaji matumizi ya vipimo na kuzingatia vipimo sahihi vya ujazo na matumizi ya mizani wakati wa kufanya biashara ya mazao ya kilimo.
Pius alisema lengo lao ni kutafuta hatua za pamoja kwenye kuboresha biashara ya mazao ya kilimo kwa kuzingatia vipimo sahihi vya ujazo ili kuongeza tija kwa wakulima, wanunuzi na halmashauri kwa ujumla.
Alisema inatakiwa kuandaa mpango wa pamoja unaotekelezeka kwa ajili ya kuwezesha matumizi ya vipimo katika wilaya ya Babati na kupashana habari ya maboresho katika sheria ya vipimo, kanuni zake na marekebisho yaliyofanywa.
“Matumizi sahihi ya vipimo ni muhimu sana katika kuhakikisha uwazi na uhakika wa vipimo vinavyotumika, ili wazalishaji, wanunuzi na watumiaji walindwe na serikali ikusanye mapato inayostahili na takwimu sahihi za uzalishaji na mauzo zipatikane,” alisema.
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa Manyara, Mhandisi Munis Weransari akifungua warsha ya matumizi sahihi ya vipimo kwenye mazao iliyoandaliwa na Mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (Mviwata) na kufanyika mjini Babati
Katibu Tawala Msaidizi Mkoani Manyara, (Huduma za Uchumi na Uzalishaji) Felix Mwasenga akifunga warsha ya matumizi sahihi ya vipimo kwenye mazao iliyoandaliwa na Mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (Mviwata) na kufanyika mjini Babati .
Hivyo makala Mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (Mviwata) walalamikia ushuru wa mazao
yaani makala yote Mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (Mviwata) walalamikia ushuru wa mazao Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (Mviwata) walalamikia ushuru wa mazao mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/05/mtandao-wa-vikundi-vya-wakulima.html
0 Response to "Mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (Mviwata) walalamikia ushuru wa mazao"
Post a Comment