MRADI WA BOMBA LA KUSAFIRISHIA MAFUTA GHAFI (EACOP) KUTOA AJIRA KWA WAKAZI WA WILAYA YA MBOGWE.

MRADI WA BOMBA LA KUSAFIRISHIA MAFUTA GHAFI (EACOP) KUTOA AJIRA KWA WAKAZI WA WILAYA YA MBOGWE. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MRADI WA BOMBA LA KUSAFIRISHIA MAFUTA GHAFI (EACOP) KUTOA AJIRA KWA WAKAZI WA WILAYA YA MBOGWE., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MRADI WA BOMBA LA KUSAFIRISHIA MAFUTA GHAFI (EACOP) KUTOA AJIRA KWA WAKAZI WA WILAYA YA MBOGWE.
kiungo : MRADI WA BOMBA LA KUSAFIRISHIA MAFUTA GHAFI (EACOP) KUTOA AJIRA KWA WAKAZI WA WILAYA YA MBOGWE.

soma pia


MRADI WA BOMBA LA KUSAFIRISHIA MAFUTA GHAFI (EACOP) KUTOA AJIRA KWA WAKAZI WA WILAYA YA MBOGWE.

Mwambawahabari
unnamed
Mkuu wa wilaya ya Mbogwe bi Martha Mkupasi amewataka wananchi wa Mbogwe watoe ushirikiano wa kutosha kwa Mradi Pendekezwa  wa ujenzi wa Bomba la Kusafirishia  Mafuta Ghafi (EACOP) linalotarajiwa kujengwa kutoka Ziwa Albert  kupitia  Kabaale (Uganda) hadi  Rasi ya Chongoleani iliyo karibu na Bandari ya Tanga nchini Tanzania.

Mkuu wa wilaya ameyasema hayo alipofungua kikao cha  maoni ya wadau (scoping) kwa Wakuu wa Idara na watendaji  wa kata wa Halmashauri ya wilaya ya Mbogwe kuhusu Tathmini ya Athari kwa  Mazingira na Jamii (TAM)  ya mradi wa EACOP. 

 Akiongea wakati wa ufunguzi bi Martha amesema mradi huo utaleta maendeleo kwa wanambogwe  wote hivyo ni jukumu lao kuulinda .

Mradi wa Ujenzi wa Bomba la Kusafirishia  Mafuta Ghafi kutoka Uganda (Ziwa Albert) hadi Tanzania (Tanga) lenye urefu wa kilometa 1445 linatarajiwa kupita katika wilaya ya Mbogwe.  Akiongea wakati wa kikao hicho ,mwezeshaji kutoka kampuni ya JSB Envi-Dev  Ltd   Dr. Godfrey Kamukara ameelezea faida zitakazopatikana kutokana na mradi huo zikiwemo upatikanaji wa ajira kwa wakazi wa Mbogwe .  

Hata hivyo alitahadharisha kuwa mradi huo unatarajiwa kusababisha  mwingiliano wa makabila mbali mbali hivyo kuwataka watendaji hao wawaelimishe wananchi kujikinga na maradhi ikiwemo ugonjwa wa ukimwi.

Dr.Kamukara amewataka watendaji kuwaelimisha wananchi kuhusu mafuta ghafi ili wananchi wasitoboe bomba wakidhani ni mafuta yanayofaa kwa matumizi . Alieleza kuwa mafuta ghafi ni mafuta ambayo bado hayajasafishwa kwa matumizi ya kawaida.

Kampuni ya RSK ya Uingereza  na washirika wake kutoka Uganda ( ECO partners ) na Tanzania ( JSB Envi-Dev Ltd)  wameanza kazi ya  Tathimini ya Athari kwa Mazingira na Jamii  kwa kushirikisha jamii yote inayopitiwa na mradi  kwa kutoa maoni ya mambo  muhimu ya kuzingatiwa wakati wa utekelezaji wa mradi huo.


Hivyo makala MRADI WA BOMBA LA KUSAFIRISHIA MAFUTA GHAFI (EACOP) KUTOA AJIRA KWA WAKAZI WA WILAYA YA MBOGWE.

yaani makala yote MRADI WA BOMBA LA KUSAFIRISHIA MAFUTA GHAFI (EACOP) KUTOA AJIRA KWA WAKAZI WA WILAYA YA MBOGWE. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MRADI WA BOMBA LA KUSAFIRISHIA MAFUTA GHAFI (EACOP) KUTOA AJIRA KWA WAKAZI WA WILAYA YA MBOGWE. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/05/mradi-wa-bomba-la-kusafirishia-mafuta_25.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MRADI WA BOMBA LA KUSAFIRISHIA MAFUTA GHAFI (EACOP) KUTOA AJIRA KWA WAKAZI WA WILAYA YA MBOGWE."

Post a Comment