title : Mbolea tani laki 4 kuagizwa nje ya nchi kuongeza uzalishaji wa mazao
kiungo : Mbolea tani laki 4 kuagizwa nje ya nchi kuongeza uzalishaji wa mazao
Mbolea tani laki 4 kuagizwa nje ya nchi kuongeza uzalishaji wa mazao
Ikiwa muundo wa kisheria wa kusimamia ununuzi wa mbolea unatarajiwa kuanza kutumika katika msimu wa kilimo wa 2017/18. Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea nchini (TFRA) imebainisha kuwa mfumo huo ukianza kutumika, takribani mbolea tani laki 4 zitaagizwa kutoka nje ya nchi ili kuongeza uzalishaji wa mazao kwa tija.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu TFRA, Lazaro Kitandu amesema kiwango hicho kitahitajika kuagizwa nje ya nchi ili kukidhi mahitaji ya mbolea nchini, ambayo kwa sasa ni tani laki 4.5 kwa mwaka, wakati inayozalishwa nchini ni tani 50,000 pekee kwa mwaka.
“Mbolea ni moja ya kichocheo muhimu katika kuongeza uzalishaji wa mazao yenye tija hata hivyo matumizi ya mbolea hapa nchini bado ni kidogo kutokana na bei ya mbolea kuwa juu. Hali hii imekuwepo kwa muda mrefu huku serikali ikiendelea kuchukua hatua mbalimbali kukabiliana na hali hii ikiwemo kwa kutoa ruzuku kwa wakulima,” amesema na kuongeza.
“Asilimia 75 ya watanzania ni wakulima wenye kipato kidogo, kutokana na hilo serikali iliuunda mfumo wa manunuzi ya mbolea unaopendekezwa ili kuimarisha utaratibu wa usambazaji ambapo wadau wote watapata uhakika wa upatikanaji mbolea kwa bei ya ushindani. Pia utasaidia wafanyabiashara wadogo kukua na kushiriki katika biashara ya mbolea.”
Amesema mbolea zitakazoagizwa nje ya nchi ni pamoja na ya kukuzia (UREA) na kupandia (DAP). Ambapo ameeleza kuwa mfumo huo utasaidia kudhibiti bei ya mbolea kwa mkulima kitendo kitakachowasaidia kupata mbolea ya uhakika kwa bei ya ushindani.
Hivyo makala Mbolea tani laki 4 kuagizwa nje ya nchi kuongeza uzalishaji wa mazao
yaani makala yote Mbolea tani laki 4 kuagizwa nje ya nchi kuongeza uzalishaji wa mazao Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Mbolea tani laki 4 kuagizwa nje ya nchi kuongeza uzalishaji wa mazao mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/05/mbolea-tani-laki-4-kuagizwa-nje-ya-nchi.html
0 Response to "Mbolea tani laki 4 kuagizwa nje ya nchi kuongeza uzalishaji wa mazao"
Post a Comment