title : Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Safarini Nchini Jordan Kwa Ziara ya Kiserikali.
kiungo : Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Safarini Nchini Jordan Kwa Ziara ya Kiserikali.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Safarini Nchini Jordan Kwa Ziara ya Kiserikali.
Na.Othman Khamos OMPR.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameondoka Zanzibar kupitia Mjini Dar es salaamu kuelekea Amman Nchini Jordan kuhudhuria Jukwaa la Uchumi la Dunia { World Economy Forum - WCF} la Siku Tatu litakalohudhuriwa na zaidi ya Wajumbe 2,000 kutoka Nchi 58 Duniani.
Balozi Seif anamuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli kwenye Jukwaa hilo la Kanda ya Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika litakaloshirikisha Vingozi Wakuu wa Nchi, Wafanyabiashara,wamiliki wa Makampunni ya Kimataifa, Wawakilishi wa Taasisi za Kiraia, Mashirikia ya Kimataifa, Wana Habari pamoja na Vijana.
Kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyefuatana na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi ameagwa na Mwaziri, baadhi ya Watendaji Wakuu wa Serikali pamoja na Viongozi wa Kisiasa.
Katika Mkutano huo wa Jukwaa la Dunia la Uchumi Balozi Seif ameongozana na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar Balozi Amina Salum Ali, pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed.
Mjini Amman Jordan.
Baadae Waziri wake anayehusika na Mipango na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa pia Mwenyekiti wa Mfuko wa Maendeleo wa Mfalme Abdullah Bwana Imad Fakhoury atapata wasaa wa kuwasilisha mpango wa maendeleo wa Taifa hilo.
Mpango huo umekuja kufuatia mabadiliko makubwa ya uchumi yaliyofanywa na Nchi hiyo ndani ya kipindi cha miaka kumi iliyopita pamoja na kutafuta mbinu ya kupata utulivu na Amani wa Mashariki ya Kati na Kanda ya Afrika kutokana na wimbi kubwa la wakimbizi lililosababishwa na vita kwenye maeneo hayo.
Jordan imekuwa muandaaji maarufu wa Jukwaa la Dunia la Uchumi { World Economy Forum }kwa takriban mara Tisa sasa na 16 kwa Kanda na Mashariki ya Kati ya Kaskazini mwa Afrika ambapo Viongozi wa Mataifa ya palestina, Misri, Kosovo, Iraq, Tanzania na Morocco wanatazamiwa kushiriki Jukwaa hilo.
Jukwaa la Uchumi la Dunia { World Economy Fforum - WCF} limeasisiwa Mwaka 1971 chini ya Muanzilishi na Mwenyekiti wake Profesa Klaus Schwab huko Davos, Switzerland.
Hivyo makala Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Safarini Nchini Jordan Kwa Ziara ya Kiserikali.
yaani makala yote Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Safarini Nchini Jordan Kwa Ziara ya Kiserikali. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Safarini Nchini Jordan Kwa Ziara ya Kiserikali. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/05/makamu-wa-pili-wa-rais-wa-zanzibar_17.html
0 Response to "Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Safarini Nchini Jordan Kwa Ziara ya Kiserikali."
Post a Comment