‘MABODI’ NI MAARUFUKU KUCHAGUA VIONGOZI WASALITI NDANI YA CCM

‘MABODI’ NI MAARUFUKU KUCHAGUA VIONGOZI WASALITI NDANI YA CCM - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa ‘MABODI’ NI MAARUFUKU KUCHAGUA VIONGOZI WASALITI NDANI YA CCM, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : ‘MABODI’ NI MAARUFUKU KUCHAGUA VIONGOZI WASALITI NDANI YA CCM
kiungo : ‘MABODI’ NI MAARUFUKU KUCHAGUA VIONGOZI WASALITI NDANI YA CCM

soma pia


‘MABODI’ NI MAARUFUKU KUCHAGUA VIONGOZI WASALITI NDANI YA CCM



NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR. 

WAFUASI wa CCM wameshauriwa kutowachagua baadhi ya wanachama wenye kashfa na tabia za usaliti kuwa viongozi wa ngazi mbali mbali zinazowaniwa ndani ya chama na jumuiya zake hicho kupitia uchaguzi unaoendelea hivi sasa. 

Ushauri huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Zanzibar, Dkt. Abdalla Juma Saadala “ Mabodi” katika mwendelezo wa mafunzo elekezi ya kuwajengea uwezo watendaji na viongozi wa majimbo ya Mkoa wa Magharibi Unguja, ili waelewe kwa kina Mabadiliko ya Katiba ya CCM na kanuni mbali mbali yaliyofanyika hivi karibuni mjini Dodoma. 

Dkt. Mabodi alisema chama hicho ili kiendelee kuimarika ni lazima wanachama wake ambao ni waaminifu wafanye maamuzi magumu ya kuwaweka kando kwa njia ya Kidemokrasia baadhi ya wanachama wenye dalili na sifa za usaliti sambamba na kamati za maadili kuanzia ngazi za chini kuwafanyia vikao vya kikanuni kuwajadili na kuwapatia fursa za kujitetea endapo watakutwa na makosa wachukuliwe hatua kwa mujibu wa maelekezo ya Katiba na kanuzi za maadili. 

Pia Dkt. Mabodi alieleza kwamba lengo la kuchukua maamuzi hayo sio kuwaonea watu hao bali ni kukisafisha chama ili kibaki na wanachama waadilifu watakaokilinda na kukipigania katika mazingira yoyote hasa wakati wa chaguzi za chama na dola pamoja na vipindi mbali mbali vya misukosuko ya kisiasa nchini. 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt. Abdalla Juma Saadala” Mabodi” akitoa ufafanuzi wa mabadiliko ya Katiba ya CCM yaliyofanyika mwaka 2017, kwa washiriki wa mafunzo elekezi ya kuwajengea uwezo ili waweze kuzikabili changamoto za uchaguzi wa chama na jumuiya zake. 
Mwasilishaji ambaye pia ni Afisa kutoka Makao Makuu ya CCM Dodoma, Nd.Alhaji Rajab Kundya akiwasilisha mada za Mabadiliko ya katiba ya CCM ya mwaka 2017, pamoja na maboresho ya kanuzi ya uchaguzi ya chama hicho. 
Ni baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia kwa makini mada zinazowasilishwa wakiwemo makatibu, wenyeviti , wajumbe wa kamati za siasa za ngazi za matawi hadi majimbo kwa chama na jumuiya zake, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mkoa wa Mjini Amani Unguja.(PICHA NA AFISI KUU CCM ZANZIBAR). 



Hivyo makala ‘MABODI’ NI MAARUFUKU KUCHAGUA VIONGOZI WASALITI NDANI YA CCM

yaani makala yote ‘MABODI’ NI MAARUFUKU KUCHAGUA VIONGOZI WASALITI NDANI YA CCM Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala ‘MABODI’ NI MAARUFUKU KUCHAGUA VIONGOZI WASALITI NDANI YA CCM mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/05/mabodi-ni-maarufuku-kuchagua-viongozi.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "‘MABODI’ NI MAARUFUKU KUCHAGUA VIONGOZI WASALITI NDANI YA CCM"

Post a Comment