title : JAFO APONGEZA USHIRIKIANO ULIOPO KISARAWE KATIKA UJENZI WA ZAHANATI
kiungo : JAFO APONGEZA USHIRIKIANO ULIOPO KISARAWE KATIKA UJENZI WA ZAHANATI
JAFO APONGEZA USHIRIKIANO ULIOPO KISARAWE KATIKA UJENZI WA ZAHANATI
Naibu Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo amewapongeza viongozi wote pamoja na wananchi wa wilaya ya kisarawe katika ujenzi wa zahanati Mpya 11 pamoja na wodi 2 za wazazi.
Jafo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kisarawe alitoa pongezi hizo alipokuwa akifanya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni Kisarawe.
Ujenzi huo unafanyika kupitia fedha za mfuko wa jimbo ambazo zimetumika kununua saruji na mabati na pia fedha kutoka Halmashauri ya wilaya ya kisarawe na michango ya wananchi.
Akiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa zahanati ya visiga, Jafo alipongeza wananchi wa visiga kwa kuunga mkono juhudi ya serikali ya awamu ya tano katika kujileta maendeleo.Aliwaomba viongozi wote waendelee na moyo huo huo wa mshikamano ili kufanikisha utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2015.
Katika hatua nyingine, Wananchi wa Tarafa ya Chole wilayani Kisarawe wameishukuru serikali ya awamu ya tano baada ya Mbunge wa jimbo la Kisarawe na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi kukabidhi gari la wagonjwa aina ya Toyota Landcruiser kwa Kituo cha Afya chole.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na wananchi wa Tarafa ya Chole katika kituo cha Afya Chole.
Gari la wagonjwa lilokabidhiwa katika Kituo cha Afya cha Chole
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na wataalam wa Kituo cha Afya Chole pamoja na viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe mara baada ya Kukabidhi gari la wagonjwa.
Jengo la Zahanati ya Visiga.
Hivyo makala JAFO APONGEZA USHIRIKIANO ULIOPO KISARAWE KATIKA UJENZI WA ZAHANATI
yaani makala yote JAFO APONGEZA USHIRIKIANO ULIOPO KISARAWE KATIKA UJENZI WA ZAHANATI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala JAFO APONGEZA USHIRIKIANO ULIOPO KISARAWE KATIKA UJENZI WA ZAHANATI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/05/jafo-apongeza-ushirikiano-uliopo.html
0 Response to "JAFO APONGEZA USHIRIKIANO ULIOPO KISARAWE KATIKA UJENZI WA ZAHANATI"
Post a Comment