Geita wapongeza huduma za NHIF

Geita wapongeza huduma za NHIF - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Geita wapongeza huduma za NHIF, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Geita wapongeza huduma za NHIF
kiungo : Geita wapongeza huduma za NHIF

soma pia


Geita wapongeza huduma za NHIF

Hospitali Teule ya Mkoa wa Geita ambapo mpango unaoendeshwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya za huduma za Madaktari Bingwa. 

Na Grace Michael, Geita

Mamia ya wananchi mkoani Geita wamejitokeza kupata huduma za madaktari bingwa , mpango unaotekelezwa kwa ushiriiano wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Mpango huo ulianza kutekelezwa siku ya Jumatatu wiki hii, katika mikoa ya Geita na Kigoma na unalenga kuwahudumia wagonjwa ambao wanahitaji huduma za kibingwa ambazo hazipo katika Hospitali hizo.

Madaktari bingwa wanaoshiriki katika mpango huo ni wa magonjwa ya watoto, mfumo wa mkojo, magonjwa ya ndani na moyo, magonjwa ya pua, masikio na koo pamoja na huduma za dawa za usingizi na huduma za wagonjwa mahututi.

Wakizungumza katika uzinduzi wa mpango huo uliofanyika katika viwanja vya hospitali ya mkoa wa Geita, wananchi waliojitokeza kupata huduma hizo wamesema ujio wa wataalamu hao umekuwa msaada mkubwa na umewaondolea usumbufu na gharama kubwa ambazo wangelazimika kuzitumia kufuata huduma hizo nje ya mkoa wao.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Matibabu na Ushauri wa Kitaalam Dk. Aifena Mramba ambaye alimwakilisha Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Benrard Konga , akitoa maelezo ya awali kwenye uzinduzi wa huduma hizo. 

“ … Mfuko umetenda jambo jema sana na unapaswa kupongezwa hasa kwa kuona umuhimu wa kusogeza huduma hizi karibu na wananchi wengi wenye mahitaji kwa mfano mimi ni mjane hapa nilipo lakini mpango huu umeniwezesha kuwaona hawa wataalam ambao kwa hali ya kawaida nisingewaona hivyo napongeza Mfuko wa Serikali yetu inayoongozwa na Dk. Pombe John Magufuli,..” Alisema Bi. Leah Ezekiel.

Akitoa maelezo ya awali Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya , Dk. Aifena Mramba alisema kuwa kwa muda wa siku mbili za zoezi hilo katika mikioa ya Kigoma na Geita, jumla ya wagonjwa 1,204, wameonwa na kuhudumiwa na madaktari bingwa.

Alisema kuwa idadi hiyo imetoa taswira ya mahitaji ya wananchi katika huduma za kibingwa jambo linalotoa hamasa kwa Mfuko kuangalia namna ya kuendesha program hizo katika maeneo mengi zaidi.
Dk. Mramba akikabidhi Mashuka na Vifaa tiba kwa uongozi wa Mkoa wa Geita kwa ajili ya matumizi ya zoezi la Madaktari Bingwa.

“…Kwa madaktari tuliowaleta, wametuhakikishia kuwa wako tayari kufanya kazi kwa muda wowote ili wagonjwa wote waliofika kwa ajili ya mpango huo wahudumiwe na mfano mzuri jana kuna madaktari waliofanya kazi hadi saa sita usiku…” alisema Dk. Mramba.



Hivyo makala Geita wapongeza huduma za NHIF

yaani makala yote Geita wapongeza huduma za NHIF Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Geita wapongeza huduma za NHIF mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/05/geita-wapongeza-huduma-za-nhif.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Geita wapongeza huduma za NHIF"

Post a Comment