title : FILAMU ZA KITANZANIA KUTEKA MAONYESHO TAMASHA LA ZIFF
kiungo : FILAMU ZA KITANZANIA KUTEKA MAONYESHO TAMASHA LA ZIFF
FILAMU ZA KITANZANIA KUTEKA MAONYESHO TAMASHA LA ZIFF
mwambawahabari blog
Zanzibariinatarajiwa kuwa mwenyeji wa mashindano ya Filamu 23 za Kitanzania zilizo fanikiwa kushinda kinyang’anyiro cha filamu bora 132 zitakazoonyeshwa katika tamasha la Nchi za Jahazi linalotarajia kufanyika Zanzibar kuanzia tarehe 8-16 Julai Zanzibar.
Fabrizio Combolo ni mkurugenziwa wa mshindano hayo , wakati wakizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam amesema tamasha hilo ambalo linatarajia kushirika mataifa 70 kutoka sehemu mbalimbali duniani.
Combolo alisema filamu zinazotarajiwa kuonyeshwa katika tamasha hilo ni filamu ndefu, filamu makala, filamu katuni na kwa mara ya kwanza Nchi ya Namibia imeweza kutayarisha filamu pamoja na filamu ya Winnie iliyotayarishwa kutoka Afrika Kusini.
“Kutakuwa na makala kutoka Afrika ya Kusuni yenye jina la Winnie ambayo itazungumzia maisha ya Winnie Mandera na kwa Tanzania kutakuwa na filamu yenye jina la Kiumeni ambayo imeshaanza kuonekana katika majumba ya sinema hapa nchini.
Kutokana na kukua kwa soko la filamu nchini, tamasha hilo kwa mara ya kwanza litaziduliwa na filamu ya Kitanzania ya T-Junction, iliyotayarishwa na Amil Shivji, jambo ambalo ni tofauti na huko nyuma ambapo walikuwa wanazindua na filamu kutoka nje ya nchi.
Amesema tamasha hilo pia litakuwa na filamu ya makala maalum ya maisha ya Mwanamuziki wa Marekani, marehemu Winnie Hauston filamu iliyoandaliwa na Mtunzi Nick Bloomfield.
Tamasha hilo pia litaweza kuonyesha filamu ya makala maalum ya Ujangili iliyorekodiwa hapa nchini ikiwa na lengo la kuhamasisha jamii kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya wanyamapori.
Hata hivyo Afisa Habari na Masoko wa tamasha hilo Lara Preston alisema kuwa kwa mara ya kwanza wameamua kuwa na soko filamu litakalofanyika ndani ya ukumbi huo ili kutoa hamasa ya kukuza tasnia ya filamu katika Afrika Mashariki.
Naye Mwenyekiti wa Mfuko wa Emerson, Said Elg alisema kuwa wapo tayari kushirikiana na ZIFF katika kunyanyua soko la filamu hivyo katika tamasha hilo watatoa tuzo kwa washindi na kwa wanafunzi 15 kutoka vyuo vya filamu watakaofanya vizuri.
Tamasha litajumuisha tuzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na :-Tuzo za nchi za Jahazi, Tuzo za Sembene Ousmane, Tuzo za filamu bora ya Afrika, Tuzo za Adiaha, Tuzo za filamu bora kwa wanawake, Tuzo za filamu bora ya Kimataifa, Tuzo za Zanzibar Emerson na Tuzo ya video ya mwanamuziki bora wa Afrika Mashariki.
Hivyo makala FILAMU ZA KITANZANIA KUTEKA MAONYESHO TAMASHA LA ZIFF
yaani makala yote FILAMU ZA KITANZANIA KUTEKA MAONYESHO TAMASHA LA ZIFF Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala FILAMU ZA KITANZANIA KUTEKA MAONYESHO TAMASHA LA ZIFF mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/05/filamu-za-kitanzania-kuteka-maonyesho.html
0 Response to "FILAMU ZA KITANZANIA KUTEKA MAONYESHO TAMASHA LA ZIFF"
Post a Comment