WATANZANIA WAHIMIZWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA TAMASHA LA JAMAFEST LITAKALOFANYIKA NCHINI UGANDA MWAKA HUU

WATANZANIA WAHIMIZWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA TAMASHA LA JAMAFEST LITAKALOFANYIKA NCHINI UGANDA MWAKA HUU - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WATANZANIA WAHIMIZWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA TAMASHA LA JAMAFEST LITAKALOFANYIKA NCHINI UGANDA MWAKA HUU, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WATANZANIA WAHIMIZWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA TAMASHA LA JAMAFEST LITAKALOFANYIKA NCHINI UGANDA MWAKA HUU
kiungo : WATANZANIA WAHIMIZWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA TAMASHA LA JAMAFEST LITAKALOFANYIKA NCHINI UGANDA MWAKA HUU

soma pia


WATANZANIA WAHIMIZWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA TAMASHA LA JAMAFEST LITAKALOFANYIKA NCHINI UGANDA MWAKA HUU

mwambawahabari
jamafest1

Na. Abuu Kimario
Bodi ya Filamu Tanzania

Watanzania wanaojihusisha na shughuli mbalimbali za ubunifu wamehimizwa kutumia fursa zinazopatikana kwenye tamasha la kazi za utamaduni na sanaa kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki JAMAFEST. Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa wajasiriamali wilaya ya Kinondoni Mwanne Yusuf Msekalile almaarufu Mwanamakuka kwenye kikao cha maandalizi ya awali ya ushiriki wa Tanzania katika tamasha hilo litakalofanyika nchini Uganda baadae mwaka huu.
Bi Mwanne mbali ya kuwa kiongozi wa wajasiriamali wilaya ya Kinondoni, pia ni mjasiriamali wa siku nyingi ambaye ameshawahi kushiriki tamasha hilo mara kadhaa. Bi Mwanne ameeleza tamasha la JAMAFEST ni fursa adhimu ambayo wajasiriamali wa Tanzania wanatakiwa kuichangamkia bila ya kukosa kwa sababu kupitia tamasha hilo wajasiriamali kutoka Tanzania wanaweza kuuza bidhaa zao, kupanua masoko na kujenga ushirikiano wa kibishara na wajasirimali kutoka nchi wanachama.
Mbali ya kutoa fursa ya kuongeza soko tamasha hilo pia ni jukwaa la wajasiriamali wa Tanzania kujifunza mbinu mbalimbali za kibiashara na kujitangaza aliongeza bi Mwanne.
Bi Mwanne aliendelea kueleza kuwa bidhaa za Tanzania kama michoro ya hina, vyakula hasa vitafunwa, manukato na sabuni zisizowekwa kemikali, filamu, picha za kuchora na nguo za batiki zimekuwa ni kivutio kikubwa tangu tamasha hilo lilipofanyika kwa mara ya kwanza nchini Rwanda.
Kwa mujibu wa maelezo ya Afisa Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanna na Michezo Joyce Hagu tamasha la JAMAFEST mwaka huu linatarajiwa kufanyika nchini Uganda ambapo maeneo tisa yatashirikishwa.
Maeneo hayo tisa ni pamoja na maonesho ya kazi za ubunifu, warsha, mikutano na midahalo, maonesho ya jukwaani kwa fani mbalimbali za utamaduni na Sanaa, maonesho ya Sanaa za ufundi, ususi na uchoraji.
Shughuli zingine ni michezo na maonesho ya watoto, michezo ya jadi, maonesho ya filamu, maonesho ya mavazi na urembo na mwisho ni vyakula vya asili.
Wakati huohuo Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Joyce Fisso ambaye alikuwa mwenyekiti wa kikao hicho amewaasa wadau wa sekta ya filamu nchini kushiriki kikamilifu kwa kupeleka kazi zao.

Tamasha la JAMAFEST ni matokeo ya juhudi za nchi zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki kutekeleza ibara ya 119 ya Mkataba wa uanzishwaji wa Jumuiya Afrika Mashariki ambao unazitaka nchi wanachama kuhimiza na kukuza ushirikiano kwenye nyanja za utamaduni na michezo. Tamasha la mwaka huu litakuwa la tatu kufanyika, mwenyeji wa kwanza tamasha hilo ilikuwa nchini Rwanda mwaka 2013 na nchi ya Kenya ilipata nafasi ya kuwa mwenyeji mwaka 2015.



Hivyo makala WATANZANIA WAHIMIZWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA TAMASHA LA JAMAFEST LITAKALOFANYIKA NCHINI UGANDA MWAKA HUU

yaani makala yote WATANZANIA WAHIMIZWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA TAMASHA LA JAMAFEST LITAKALOFANYIKA NCHINI UGANDA MWAKA HUU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WATANZANIA WAHIMIZWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA TAMASHA LA JAMAFEST LITAKALOFANYIKA NCHINI UGANDA MWAKA HUU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/04/watanzania-wahimizwa-kuchangamkia-fursa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WATANZANIA WAHIMIZWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA TAMASHA LA JAMAFEST LITAKALOFANYIKA NCHINI UGANDA MWAKA HUU"

Post a Comment