title : WATANZANIA WAASWA KUWA WAZALENDO NA KULINDA AMANI ILIYOPO
kiungo : WATANZANIA WAASWA KUWA WAZALENDO NA KULINDA AMANI ILIYOPO
WATANZANIA WAASWA KUWA WAZALENDO NA KULINDA AMANI ILIYOPO
Na. Immaculate Makilika- MAELEZO - DODOMA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu, Ajira na Wenye ulemavu, Jenista Mhagama amewaasa Watanzania kuwa wazalendo pamoja na kudumisha amani na utulivu uliopo nchini.
Akizungumza, leo mjini Dodoma wakati akifuatatilia maandalizi ya Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano yatakayofanyika Aprili 26 mwaka huu katika Uwanja wa Jamhuri uliopo mjini Dodoma.
“Tunapoadhimisha miaka 53 ya Muungano ninawaomba watanzania kuwa wazalendo pamoja na kulinda amani ya nchi” alisema Waziri Mhagama
Pia, Waziri Mhagama aliwaomba watanzania hasa wakazi wa Dodoma kuhudhuria kwa wingi katika Maadhimisho hayo yatakayofanyika jumatano wiki hii.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana alisema kuwa mkoa wake umejipanga vizuri katika kufanikisha maadhimisho hayo, ambapo pia alivishukuru vyombo vya habari kwa kuhamasisha wananchi juu ya maadhimisho hayo.
“Wananchi wamehamasika kushiriki katika maadhimisho haya ya miaka 53 ya Muungano, ninawashukuru kwa kazi kubwa mliyoifanya na tunaamini mtaendelea kuhamasisha wananchi kushiriki katika maadhimisho hayo” alisema Rugimbana
Maandalizi ya Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano yamehudhuriwa pia na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini Christina Mndeme, pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali.
Aidha, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, ambapo pia yatahudhuriwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohammed Shein na viongozi mbalimbali wa dini na Serikali.
Maadhimisho hayo ya miaka 53 ya Muungano yanatarajiwa kupambwa namaonesho kutoka kutoka vikosi mbalimbali vya ulinzi na usalama, burudani za vikundi vya ngoma pamoja na maonesho ya halaiki.
Waziri Mhagama akikagua maandalizi ya kuadhimisha Sherehe za Miaka 53 ya Muungano katika viwanja vya Jamhuri leo Mjini Dodoma.
Baadhi ya wananchi wakifuatilia maonesho ya maandalizi ya Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika terehe 26 Aprili Mjini Dodoma kwa mara ya kwanza tangu Serikali ilipohamia Dodoma.
Vikosi vya Ulinzi na Usalama vikiwa kwenye gwaride la maandalizi ya maadhimisho ya Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika terehe 26 Aprili Mjini Dodoma.
Vikosi vya Ulinzi na Usalama vikiwa kwenye gwaride la maandalizi ya maadhimisho ya Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika terehe 26 Aprili Mjini Dodoma.
Vikosi vya Ulinzi na Usalama vikiwa kwenye gwaride la maandalizi ya maadhimisho ya Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika terehe 26 Aprili Mjini Dodoma.
Hivyo makala WATANZANIA WAASWA KUWA WAZALENDO NA KULINDA AMANI ILIYOPO
yaani makala yote WATANZANIA WAASWA KUWA WAZALENDO NA KULINDA AMANI ILIYOPO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WATANZANIA WAASWA KUWA WAZALENDO NA KULINDA AMANI ILIYOPO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/04/watanzania-waaswa-kuwa-wazalendo-na.html
0 Response to "WATANZANIA WAASWA KUWA WAZALENDO NA KULINDA AMANI ILIYOPO"
Post a Comment