Wadau wakutana kujadili uwekezaji katika kilimo

Wadau wakutana kujadili uwekezaji katika kilimo - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Wadau wakutana kujadili uwekezaji katika kilimo, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Wadau wakutana kujadili uwekezaji katika kilimo
kiungo : Wadau wakutana kujadili uwekezaji katika kilimo

soma pia


Wadau wakutana kujadili uwekezaji katika kilimo

 Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kwa kushirikiana na Mfuko wa Kukuza Sekta ya Fedha (FSDT) imewakutanisha pamoja wadau kutoka sekta mbalimbali za maendeleo nchini kujadili masuala mbalimbali yatakayosaidia uwekezaji mkubwa katika sekta ya kilimo Tanzania.

Akizungumza katika kikao kazi hicho mwenyekiti wa Kikundi Kazi, aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bw. Peniel Lyimo alisema kuna haja ya  dhamira ya dhati na uwekezaji mkubwa katika sekta ya kilimo nchini ili kusaidia juhudi za Serikali za kuinua ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini.
Mwenyekiti wa Kikundi Kazi, Bw. Peniel Lyimo (Katikati) akizungumza na wajumbe wa Kikundi Kazi (Hawapo pichani) wakati wa mkutano wa wadau wa kujadili uwekezaji katika sekta ya kilimo uliofanyika katika Hoteli ya Court Yard, Dar es Salaam. Wanaomsikiliza Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga na Mkuu wa Kilimo na Fedha Vijijini wa FSDT, Bw. Mwombeki Baregu (Kulia).

Bw. Lyimo alisema kuwa ufinyu mkubwa wa upatikanaji wa fedha mikopo kwa ajili ya maendeleo ya kilimo nchini unachangiwa kwa kiasi kikubwa na mikopo mingi kutoka taasisi za fedha kuelekezwa zaidi kwenye upande wa biashara za bidhaa hali inayorudisha nyuma mapinduzi katika sekta ya kilimo nchini.

“Kuna haja ya kutafuta suluhisho la changamoto za upatikanaji wa fedha mikopo kwa ajili ya Kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini,” alisema.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga akizungumza juu ya umuhimu wa wadau katika kuchagiza uwekezaji katika sekta ya kilimo nchini.

Akizungumzia umuhimu wa kikao kazi hicho, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga alisema kikao hicho kinalenga kuwaleta wadau kutoka sekta mbalimbali ili kujadili kwa kina njia sahihi za kuchagiza uwekezaji wenye tija katika kilimo nchini.

Bw. Assenga alisema kuwa kwa kushirikiana na wadau mbali mbali wa maendeleo kutachagiza kusaidia uwekezaji mkubwa kwenye Sekta ya Kilimo, na kuleta mapinduzi ya kilimo nchini.

“Kimsingi Kikao hiki kinalenga kuanzisha mtandao mpana wa majadiliano na wadau mbalimbali, zikiwemo Wizara zinazohusika na Kilimo na Taasisi mbali mbali za Serikali na Binafsi, ili kukubaliana vipaumbele na namna ya kushirikiana katika kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya TADB katika kuleta mapinduzi ya kilimo nchini,” alisema.
Mkuu wa Kilimo na Fedha Vijijini wa FSDT, Bw. Mwombeki Baregu (Kulia) akizungumza wakati wa mkutano huo. Pichani ni Mwenyekiti wa Kikundi Kazi, Bw. Peniel Lyimo (Katikati) na Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga.



Hivyo makala Wadau wakutana kujadili uwekezaji katika kilimo

yaani makala yote Wadau wakutana kujadili uwekezaji katika kilimo Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Wadau wakutana kujadili uwekezaji katika kilimo mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/04/wadau-wakutana-kujadili-uwekezaji.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Wadau wakutana kujadili uwekezaji katika kilimo"

Post a Comment