title : TPDC yazidi kujikita kileleni michuano ya Mei mosi
kiungo : TPDC yazidi kujikita kileleni michuano ya Mei mosi
TPDC yazidi kujikita kileleni michuano ya Mei mosi
Timu ya Mpira wa Miguu ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania yazidi kujikita kileleni kwenye mashindano ya Mei Mosi yanayofanyika Mkoani Kilimanjaro baada ya kuizamisha timu ya mpira wa miguu ya uchukuzi kwa jumla ya mabao 2-0.
TPDC imefanikiwa kupata ushindi huo kupitia wachezaji wake mahiri Phinias Ademba ambaye aliipatia timu yake gori la kwa kwanza mnamo dakika ya 26 ya kipindi cha kwanza ambapo gori hilo lilidumu hadi kipindi cha pili dakika ya 58 pale mchezaji Walter Mwanga alipoipatia timu ya TPDC gori la pili lililodumu hadi mwisho wa mchezo.
Ushindi huu umeifanya TPDC kuongoza katika kundi kundi B ikiwa na jumla ya point sita na magori matatu ikifuatiwa na Hai DC ikiwa na pointi tatu. Katika mechi awali TPDC ilijipatia pointi tatu baada ya kuifunga timu ya Hai DC gori moja kwa sifuri. TPDC inatarajia kushuka dimbani tena tarehe 26 kuchuana na timu ya Mpira wa Miguu ya Moshi DC.
Wachezaji wa TPDC wakitoka uwanjani kwa mbwembwe wakisindikizwa na wafanyakazi wenzao waliokuwa wakishuhudia timu yao ikitoa kipigo kikali dhidi ya Uchukuzi.
Baadhi ya watumishi wa TPDC wakishangilia na kuipongeza timu yao mara baada ya mechi dhidi ya TPDC na Uchukuzi kukamilika huku TPDC ikiibuka na ushindi wa magori 2-0.
Hivyo makala TPDC yazidi kujikita kileleni michuano ya Mei mosi
yaani makala yote TPDC yazidi kujikita kileleni michuano ya Mei mosi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TPDC yazidi kujikita kileleni michuano ya Mei mosi mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/04/tpdc-yazidi-kujikita-kileleni-michuano.html
0 Response to "TPDC yazidi kujikita kileleni michuano ya Mei mosi"
Post a Comment