title : SHIRIKA LA ANGA LA ETIHAD LAMTEUA ROBIN KAMARK KUWA OFISA MTENDAJI MKUU WA IDARA YAKE TANZU YA AIRLINE EQUITY PARTNERS
kiungo : SHIRIKA LA ANGA LA ETIHAD LAMTEUA ROBIN KAMARK KUWA OFISA MTENDAJI MKUU WA IDARA YAKE TANZU YA AIRLINE EQUITY PARTNERS
SHIRIKA LA ANGA LA ETIHAD LAMTEUA ROBIN KAMARK KUWA OFISA MTENDAJI MKUU WA IDARA YAKE TANZU YA AIRLINE EQUITY PARTNERS
Shirika la Anga la Etihad limetangaza uteuzi wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Idara yake tanzu ya Airline Equity partners, Bwana Robin Kamark ambaye atashughulikia kuongoza na kuendeleza mikakati ya uwekezaji inayojumuisha wabia wa Shirika hilo kama vile; Airberlin, Alitalia, Jet Airways, Air Serbia, Air Seychelles, Etihad Regional na Virgin Australia.
Mtendaji huyo mkuu atakuwa chini ya Rais wa Shirika hilo na Mkurugenzi Mkuu. Kamark anachukua nafasi ya Bruno Matheu ambaye alishika wadhifa huo tangu Mei 2016 ambaye imeelezwa kwamba anaachia ngazi kutokana na sababu zake binafsi.
Kamark amefanya kazi katika sekta ya anga kwa takriban miaka 17, huku akifanikiwa kufikia malengo ya mikakati yake ya kibiashara na masuala ya utawala katika Shirika la SAS ambako pia alikuwa akitekeleza majukumu yake kama Ofisa Mkuu wa Biashara.
Kwa miaka mitano yake ya mwishoni amefanya kazi kama Makamu wa Rais na Ofisa Mkuu wa Biashara katika kitengo cha bidhaa za ASA zinazoongoza kwa huduma za kifedha na biashara.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Anga la Etihad, Mhe. Mohamed Mubarak Fadhel Al Mazrouei amesema kwamba “Shirika hili linaendelea kuwekeza duniani katika kiwango chenye ubora wa juu, ikiwamo kujenga timu nzuri itakayoongoza biashara na kuipelekea katika hatua kubwa zaidi za maendeleo.”
Alisema, “Robin ni kiongozi anayeheshimika katika sekta ya anga duniani pia ana uzoefu mkubwa kutoka Shirika la SAS. Amefanya kazi kubwa ya kuboresha shirika hilo la ndege. Hivi karibuni amepanua wigo wa taaluma yake katika masuala ya huduma za kifedha.”
Aliongeza kuwa, “Ushirikiano na kampuni yetu utaendelea kuwa alama muhimu katika biashara na Robin ataongoza mipango hiyo kwa kuweka mikakati na kuendeleza dhamira yetu.”
“Tunapenda kumshukuru Bruno kwa juhudi zake kubwa alizoonyesha kwa kipindi cha miaka miwili na nusu kutokana na kufanikiwa kujenga na kuhimarisha ushirikiano wetu katika kitengo cha Airline Equity partners,” alisema kiongozi huyo.
Hivyo makala SHIRIKA LA ANGA LA ETIHAD LAMTEUA ROBIN KAMARK KUWA OFISA MTENDAJI MKUU WA IDARA YAKE TANZU YA AIRLINE EQUITY PARTNERS
yaani makala yote SHIRIKA LA ANGA LA ETIHAD LAMTEUA ROBIN KAMARK KUWA OFISA MTENDAJI MKUU WA IDARA YAKE TANZU YA AIRLINE EQUITY PARTNERS Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SHIRIKA LA ANGA LA ETIHAD LAMTEUA ROBIN KAMARK KUWA OFISA MTENDAJI MKUU WA IDARA YAKE TANZU YA AIRLINE EQUITY PARTNERS mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/04/shirika-la-anga-la-etihad-lamteua-robin.html
0 Response to "SHIRIKA LA ANGA LA ETIHAD LAMTEUA ROBIN KAMARK KUWA OFISA MTENDAJI MKUU WA IDARA YAKE TANZU YA AIRLINE EQUITY PARTNERS"
Post a Comment