RAY na Mama Kanumba Kimenuka....

RAY na Mama Kanumba Kimenuka.... - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa RAY na Mama Kanumba Kimenuka...., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : RAY na Mama Kanumba Kimenuka....
kiungo : RAY na Mama Kanumba Kimenuka....

soma pia


RAY na Mama Kanumba Kimenuka....

Mama mzazi wa aliyekuwa nyota wa filamu bongo, marehemu  Steven Kanumba, Flora Mtegoa siku ya kumbukumbu ya mwanaye makaburini Kinondoni, alimfyatukia msanii wa filamu nchini,  Vincent Kigosi ‘ray’ aliyekuwa swahiba wa mwanaye kuwa, hajawahi kumuona hata siku moja makaburini hapo kuomboleza kifo cha mwanaye miaka yote ambayo hufanya kumbukumbu hiyo.


Akizungumza na Amani makaburini hapo, Aprili 7, mwaka huu,  mama Kanumba alisema kuwa, tangu aanze kuazimisha kumbukumbu za mwanaye hajawahi kumuona  Ray akiomboleza wala hata kuungana naye makaburini kama mastaa wengine wanavyofanya. “Yaani sijawahi kumuona huyo Ray akijumuika na sisi makaburini, utadhani yeye ataishi milele duniani.


Kumbuka somo la leo kutoka kwenye Biblia linatufundisha kuwa, kila binadamu atakufa,” alisema mama Kanumba. Aidha, mama huyo alisema kuwa kama Ray na mwanaye waliwahi kuwa na ugomvi basi amsamehe kwani binadamu tumefunzwa kusamehe na sasa hayupo tena duniani.

“Unajua huenda walikoseana marehemu akiwa hai lakini mpaka leo naona kama ana kinyongo, asamehe tu. Naongea hayo kwa sababu sijawahi kuona akimuenzi hata kwa kufika makaburini kuungana na sisi, utadhani hakuwahi kuwa na uhusiano naye.

Nawashukuru sana wasanii wa kike wao ndiyo huungana na mimi katika maombolezo ingawa kwa mwaka huu hawakujitokeza lakini siwezi kuwasema vibaya kiukweli,” alisema mama huyo.

Baada ya habari hizi kutoka kwa mama Kanumba, Amani juzi lilizungumza na Ray aliyeamua kufunguka kuwa, yeye humuenzi Kanumba kwa njia nyingi tu si lazima kujionesha makaburini na si  lazima kuutangazia umma.

“Mimi najua marehemu alikuwa rafiki yangu na nimekuwa nikimkumbuka na kumuenzi kwa mambo mengi tu si lazima kuungana na mama Kanumba makaburini ndiyo nionekane,” alisema Ray kwa sauti yenye kumshangaa mama Kanumba kwa madai yake hayo.


Hivyo makala RAY na Mama Kanumba Kimenuka....

yaani makala yote RAY na Mama Kanumba Kimenuka.... Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala RAY na Mama Kanumba Kimenuka.... mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/04/ray-na-mama-kanumba-kimenuka.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "RAY na Mama Kanumba Kimenuka...."

Post a Comment