title : MAONESHO YA TISA YA KIPEKEE YA HARUSI TRADE FAIR KUFANYIKA MEI 12 HADI13.
kiungo : MAONESHO YA TISA YA KIPEKEE YA HARUSI TRADE FAIR KUFANYIKA MEI 12 HADI13.
MAONESHO YA TISA YA KIPEKEE YA HARUSI TRADE FAIR KUFANYIKA MEI 12 HADI13.
Mwambawahabari
Na Maria Kaira
Maonesho ya tisa ya Harusi Trade Fair yanatarajiwa kufanyika Mei 12 hadi 13 mwaka huu kwenye hoteli ya Golden Tulip Oyststerbay Jiji Dar es salaam ili kuwapatia maharusi uwanja wa kuchagua mahitaji yao yote kwa ukamilifu siku ya harusi yao.
Akizungumza na waandishi wa habari Meneja Biashara Hamis Omary amesema maonesho hayo ni ya kipekee kwa Afrika mashariki na pwani na hufanyika mara moja kwa kila mwaka .
" Tunawatangazia jamii kwa ujumla watarajie maonesho yakuvutia kuburudisha pamoja na nyakati rahisi kwa bw. harusi na bi. harusi kuandaa vitu vyao vya harusi, vilevile kutakuwa na mitindo mipya Mingi kutoka kwa wauzaji bora katika sekta ya harusi kila maonesho yanavyoendelea kukua kutoka hatua moja na kwenda hatua nyingine ndivyo ubora unavyoendelea kuongezeka" amesema
Omary amesema maonesho hayo yatakuwa ya kipekee na ya kwanza hapa nchini ambayo yameweza kuwavutia washiriki wengi tangu yalipoanza mwaka 2009, pia amesema maonesho hayo yanaudhuriwa na mtu yoyote bila malipo.
Aidha Mratibu wa maonesho hayo Naomi Godwin amesema harusi ni umoja wa familia na jamii na ni jambo la mara moja maishani, ambapo amewataka maharusi kuchagua vitu vilivyo bora .Pia amesema mipango yao ni kuwapatia maharusi uwanja wa kuchagua mahitaji yao kwa Kuchagua kitu kilicho bora .
"Harusi Trade Fair inawaleta pamoja wauza bidhaa na watoa huduma tofauti katika sekta ya harusi na ni sehemu ya mtandao kwa wafanyabiashara bora wa kitanzania waliopo katika sekta hiyo ambapo zaidi ya wafanyabiashara 30 watashiriki kutoa huduma na kuuza bidhaa kwa maharusi watarajiwa pamoja na familia zao"
"Msimu wa harusi kwa watanzania unaanza tunaomba familia marafiki na wanakamati wa maandalizi ya harusi kuudhuria ili waweze kuangalia ubunifu na vipaji vya watanzania waliopo kwenye sekta ya harusi na kuzifanya harusi zao kuwa na ukumbusho wa kipekee"amesema
Naomi aliongeza kuwa kutakuwa na wapiga picha, huduma za vyakula,wapambaji wa ukumbi, huduma za nywele, wapamba USO, wamiliki wa ukumbi za sherehe, wabunifu wa nguo,waandaaji harusi na washeheresha harusi.
Hivyo makala MAONESHO YA TISA YA KIPEKEE YA HARUSI TRADE FAIR KUFANYIKA MEI 12 HADI13.
yaani makala yote MAONESHO YA TISA YA KIPEKEE YA HARUSI TRADE FAIR KUFANYIKA MEI 12 HADI13. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAONESHO YA TISA YA KIPEKEE YA HARUSI TRADE FAIR KUFANYIKA MEI 12 HADI13. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/04/maonesho-ya-tisa-ya-kipekee-ya-harusi.html
0 Response to "MAONESHO YA TISA YA KIPEKEE YA HARUSI TRADE FAIR KUFANYIKA MEI 12 HADI13."
Post a Comment