title : MANISPAA YA ILALA JIJINI DAR ES SALAAM YAOMBWA KULINUSURU DARAJA ZISISOMBWE NA MAFURIKO
kiungo : MANISPAA YA ILALA JIJINI DAR ES SALAAM YAOMBWA KULINUSURU DARAJA ZISISOMBWE NA MAFURIKO
MANISPAA YA ILALA JIJINI DAR ES SALAAM YAOMBWA KULINUSURU DARAJA ZISISOMBWE NA MAFURIKO
MwambawahabariWakazi wa Gongolamboto wakipita katika daraja ambalo kingo zake zimesombwa na mafuriko barabara ya kuelekea Machinjio ya Pugu Kajiungeni Dar es Salaam leo.Jitihada za makusudi zisipochukuliwa daraja hilo litasombwa na maji.

Mwonekano wa eneo hilo baada ya kusombwa na mafuriko.
Na Dotto Mwaibale
MANISPAA ya Ilala imeombwa kufanya jitihada za makusudi kuinusuru daraja linaloungani eneo la Gongola mboto na Machinjio ya Pugu ambalo lipokatika hatari ya kusombwa na maji.
Mwito huo umetolewa Dar es Salaam leo na wakazi wa Pugu Machinjioni ambao wamesema iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa mawasiliano kati ya wananchi wa eneo
hilo na Gongolamboto yatatoweka hivyo kuwa adha kwao kwa kufika makwao kwa kupitia Pugu Kajiungeni badala ya barabara ya Gongo lamboto Pugu Machinjioni kupitia kiwanda cha kutengeneza nguo cha Namera.
“Tunaomba manispaa yetu ilifanyie ukarabati daraja hili ambapo kwa sehemu kubwa kingo zake zimesombwa na maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha ” alisema Omari Mshamu mkazi wa eneo hilo.
Mkazi mwingine wa eneo hilo Marietha Stanslaus alisema iwapo daraja hilo linasombwa na maji watakaopata shida zaidi ni wanafunzi kwani watalazimika kutumia njia ndefu kufika mashuleni kwao kutokana kuwa wengi wao wanasoma shule za Gongolamboto.
Hivyo makala MANISPAA YA ILALA JIJINI DAR ES SALAAM YAOMBWA KULINUSURU DARAJA ZISISOMBWE NA MAFURIKO
yaani makala yote MANISPAA YA ILALA JIJINI DAR ES SALAAM YAOMBWA KULINUSURU DARAJA ZISISOMBWE NA MAFURIKO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MANISPAA YA ILALA JIJINI DAR ES SALAAM YAOMBWA KULINUSURU DARAJA ZISISOMBWE NA MAFURIKO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/04/manispaa-ya-ilala-jijini-dar-es-salaam.html
0 Response to "MANISPAA YA ILALA JIJINI DAR ES SALAAM YAOMBWA KULINUSURU DARAJA ZISISOMBWE NA MAFURIKO"
Post a Comment