MAKAMPUNI YA MADINI YACHANGIA AJIRA NA KUINUA UCHUMI NCHINI.

MAKAMPUNI YA MADINI YACHANGIA AJIRA NA KUINUA UCHUMI NCHINI. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAKAMPUNI YA MADINI YACHANGIA AJIRA NA KUINUA UCHUMI NCHINI., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAKAMPUNI YA MADINI YACHANGIA AJIRA NA KUINUA UCHUMI NCHINI.
kiungo : MAKAMPUNI YA MADINI YACHANGIA AJIRA NA KUINUA UCHUMI NCHINI.

soma pia


MAKAMPUNI YA MADINI YACHANGIA AJIRA NA KUINUA UCHUMI NCHINI.

  Image result for picha za migodi

Jovina Bujulu 
mwambawahabari

Ukuaji wa uchumi katika nchi nyoyote duniani hujengwa na sekta mbalimbali ikiwemo madini, utalii, misitu na makusanyo ili kuwahudumia wananchi katika mahitaji yao ya kila siku.

Miongoni mwa huduma ambazo hutolewa baada ya makusanyo ya mapato yatokanayo na sekta hizi yanasaidia kuboresha utoaji wa elimu, afya, maji na nishati kwa manufaa ya wananchi.

Sekta ya madini nchini imekuwa na mchango mkubwa katika kukuza uchumi na shughuli mbalimbali za maendeleo kupitia uwekezaji, ikiwemo ujenzi wa miundombinu muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu, hivyo kuwa na mchango chanya katika kuinua kipato cha nchi na wananchi  kwa ujumla.

Ili sekta madini iwe na tija kwa nchi na wananchi wake, Serikali imeweka mamlaka ya kuratibu ili kuhakikisha kuwa makampuni ya uchimbaji madini yanafanya shughuli zake kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za nchi.

Mchango wa makampuni haya umekuwa na tija kwa taifa kwa kutengeneza ajira pamoja na kulipa kodi zinazostahili kulipwa, kuchangia soko la fedha za kigeni, manunuzi ya huduma pamoja na michango ya hiyari kwa shughuli mbalimbali za maendeleo kwa jamii zinazozunguka makampuni hayo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania ya mwaka 2015, inaonyesha kuwa sekta rasmi ya uchimbaji madini ilitoa ajira 7,355 ambazo ni za moja kwa moja  na zaidi ya ajira 3,000 kupitia makampuni ya wakandarasi.
Upatikanaji wa ajira hizo unaonesha kuwa mtu mmoja aliyepata ajira anahudumia watu 11 wasio na kazi  na hivyo kuwezesha wastani wa watu 114,000 kuendelea kuishi na kupata huduma za msingi.
Kwa upande wa kulipa kodi, taarifa hiyo inaonyesha kuwa kati ya mwaka 2009 na 2015 makampuni makubwa yamelipa kodi Serikalini zaidi ya shilingi billioni 870 ikiwa ni mrahaba  na zaidi ya shilingi billioni 680 zililipwa kama kodi ya mapato na kodi nyinginezo ambazo sio za moja kwa moja.
Aidha, katika kipindi cha mwaka 2015 pekee, shilingi billioni 146 zililipwa na migodi mikubwa mitano ya dhahabu pamoja na mgodi mmoja wa almasi kama mrabaha na kodi ya mapato.
Uendeshaji wa sekta ya madini nchini upo chini ya Serikali na taasisi zake ambazo ni Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) na Shirika la Uchimbaji wa Madini la Taifa (STAMICO), ambapo sera zilizowekwa mwishoni mwa miaka ya 1990 ziliwavutia wawekezaji wageni ambao walianzisha migodi mikubwa ya uchimbaji wa dhahabu.


Hivyo makala MAKAMPUNI YA MADINI YACHANGIA AJIRA NA KUINUA UCHUMI NCHINI.

yaani makala yote MAKAMPUNI YA MADINI YACHANGIA AJIRA NA KUINUA UCHUMI NCHINI. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAKAMPUNI YA MADINI YACHANGIA AJIRA NA KUINUA UCHUMI NCHINI. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/04/makampuni-ya-madini-yachangia-ajira-na_25.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MAKAMPUNI YA MADINI YACHANGIA AJIRA NA KUINUA UCHUMI NCHINI."

Post a Comment