title : KUJAZA KWA NAFASI YA MWENYEKITI WA TEITI
kiungo : KUJAZA KWA NAFASI YA MWENYEKITI WA TEITI
KUJAZA KWA NAFASI YA MWENYEKITI WA TEITI
Kifungu 7(2) cha Sheria ya Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia, Mwaka 2015
Utangulizi
Utekelezaji wa shughuli za Tanzania Extractive Industries Transparency Initiative (TEITI) zinasimamiwa na Kamati ya TEITI yenye wajumbe kumi na tano (15) kutoka makundi matatu: – Asasi za kiraia; Kampuni na Serikalini. Kila kundi linawakilishwa na wajumbe watano ambao uteuzi wao hufanywa kutoka katika makundi husika. Sheria tajwa hapo juu, imeweka utaratibu katika Kifungu cha 7 wa namna ya kumpata Mwenyekiti.
Majukumu ya Kamati ya TEITI
Majukumu ya Kamati ni kuhamasisha Serikali kuweka mifumo ya uwazi katika usimamizi wa rasilimali za madini, mafuta na gesi asilia ili kuboresha mapato na manufaa yanayotokana na shughuli za utafutaji na uchimbaji wa rasilimali hizo nchini. Mazingira ya uwazi yanayolengwa ili kuwa na manufaa ya rasilimali husika ni katika:
- Utoaji wa leseni na mikataba ya uchimbaji wa madini, mafuta na gesi asilia;
- Usimamizi katika uwekezaji na uendeshaji;
- Ukusanyaji wa mapato; na
- Mgawanyo wa mapato na matumizi.
Kufuatia kwisha kwa muda wa Mwenyekiti aliyopo sasa, Kamati ya Uteuzi (Nomination Committee) inakaribisha maombi kutoka kwa wananchi wenye sifa:-
- Awe Mtanzania aliye na rekodi ya utendaji uliotukuka;
- Awe na uelewa na ufahamu mzuri juu ya sekta za madini, gesi asilia na mafuta; na
- Awe mtu anayeweza kujenga mahusiano ya kikazi na kampuni zilizo katika sekta hii, asasi za kiraia na Serikali.
Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni Mei 17, 2017. Maombi yatumwe kwa anwani ifuatayo:
Katibu Mkuu,
Wizara ya Nishati na Madini,
Barabara ya Kikuyu,
- L. P. 422,
40474 DODOMA.
baruapepe: info@teiti.or.tz
Hivyo makala KUJAZA KWA NAFASI YA MWENYEKITI WA TEITI
yaani makala yote KUJAZA KWA NAFASI YA MWENYEKITI WA TEITI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KUJAZA KWA NAFASI YA MWENYEKITI WA TEITI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/04/kujaza-kwa-nafasi-ya-mwenyekiti-wa-teiti.html
0 Response to "KUJAZA KWA NAFASI YA MWENYEKITI WA TEITI"
Post a Comment