title : DKT. MWAKYEMBE AIAGIZA BASATA KUSIMAMIA MISS TANZANIA
kiungo : DKT. MWAKYEMBE AIAGIZA BASATA KUSIMAMIA MISS TANZANIA
DKT. MWAKYEMBE AIAGIZA BASATA KUSIMAMIA MISS TANZANIA
Na Shamimu Nyaki-WHUSM.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe ameliagiza Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kusimamia mashindano ya Miss Tanzania kwa ufanisi na kuhakikisha yanazingatia kanuni za uandaaji wa mashindano ya urembo.
Mhe. Mwakyembe ameyasema hayo jana Mjini Dododma wakati alipokutana na Kamati ya Miss Tanzania iliyoongozwa na mwenyekiti Bw Hashim Lundenga na kuwataka kusimamia vyema shindano hilo ili kupata washindi wenye viwango vinavyotakiwa Kimataifa.
“Nawaagiza BASATA simamieni shindano hili ili tupate washindi wenye viwango watakaosaidia Tanzania kujitangaza Kimataifa katika urembo”, Alisema Mhe. Mwakyembe.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Braza la Sana la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Muingereza amemuahidi Mhe Waziri Mwakyembe kuwa atasisamia kwa karibu na kwa ufanisi mashindano ya Miss Tanzania ili yawe na ubora zaidi utakaowezesha nchi kufanya vizuri kwenye mashindano ya Dunia.
Naye Mweyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania Bw. Hashim Lundenga ameahidi kushirikiana na Wizara pamoja na BASATA katika kuandaa na kuboresha shindano la Miss Tanzania ili kuwa na nguvu ya pamoja katika kupata ushindi utakaoletea Taifa heshima.
Mashindano ya Miss Tanzania yanayotarajiwa kufanyika baadae mwaka huu yanaandaliwa na kusimamiwa na Kamati inayoongozwa na Mwenyekiti Bw. Hashim Lundenga, Katibu Wake Bw.Bosco Majaliwa na Mjumbe Bw. Deo Kapten.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Miss Tanzania mara baada ya kufanya mazungumzo ofisini kwake Mjini Dododma jana.Wa kwanza kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa Bw.Godfrey Muingereza.
Hivyo makala DKT. MWAKYEMBE AIAGIZA BASATA KUSIMAMIA MISS TANZANIA
yaani makala yote DKT. MWAKYEMBE AIAGIZA BASATA KUSIMAMIA MISS TANZANIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DKT. MWAKYEMBE AIAGIZA BASATA KUSIMAMIA MISS TANZANIA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/04/dkt-mwakyembe-aiagiza-basata-kusimamia.html
0 Response to "DKT. MWAKYEMBE AIAGIZA BASATA KUSIMAMIA MISS TANZANIA"
Post a Comment