title : TAARIFA RASMI KUHUSU MAADHIMISHO YA SIKU YA KUMBUKUMBU YA KARUME (KARUME DAY), 2019 ILIYOSOMWA NA KAIMU WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS, MHE. DKT SIRA UBWA MAMBOYA
kiungo : TAARIFA RASMI KUHUSU MAADHIMISHO YA SIKU YA KUMBUKUMBU YA KARUME (KARUME DAY), 2019 ILIYOSOMWA NA KAIMU WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS, MHE. DKT SIRA UBWA MAMBOYA
TAARIFA RASMI KUHUSU MAADHIMISHO YA SIKU YA KUMBUKUMBU YA KARUME (KARUME DAY), 2019 ILIYOSOMWA NA KAIMU WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS, MHE. DKT SIRA UBWA MAMBOYA
Ndugu wananchi,
Kwanza kabisa nachukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema na Mwenye Kurehemu kwa kuendelea kuijaalia nchi yetu kuwa katika hali ya amani na utulivu mkubwa.
Ndugu Wananchi,
Kama tunavyoelewa kwamba kila inapofika tarehe 7 Aprili ya kila mwaka nchi yetu huadhimisha kumbukumbu ya kifo cha Sheikh Abeid Amani Karume, Jemedari Mkuu wa Mapinduzi yetu Matukufu ya tarehe 12 Januari, 1964 ambayo yaliung’oa utawala wa kisultani hapa Zanzibar. Sheikh Karume aliuwawa kwa kupigwa risasi na wapinga mapinduzi katika eneo la ukumbi wa iliyokuwa Afisi Kuu ya Chama cha Afro-Shirazi hapo Kisiwandui tarehe 7 Aprili mwaka 1972. Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume yana lengo la kumkumbuka kiongozi wetu huyu pamoja na viongozi wetu wengine wote waasisi wa Taifa letu waliotangulia mbele ya haki.
Ndugu Wananchi,
Kutokana na azma hiyo, Serikali imeamua kuanzia mwaka huu wa 2019, maadhimisho haya yatafanywa kwa wiki moja kuanzia tarehe 2 Aprili na kufikia kilele chake tarehe 7 Aprili. Maadhimisho haya yatahusisha shughuli mbalimbali ikiwemo kufanya ziara na kusomwa dua katika makaburi ya viongozi wakuu wa kitaifa waliokwishafariki dunia pamoja na kufanya makongamano yenye mnasaba na historia na mchango wa Mzee Karume katika maendeleo ya Zanzibar. Shughuli hizi zitafanyika Unguja na Pemba.
Ndugu wananchi,
Kufuatia utaratibu huu mpya wa Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Siku ya Karume, kwa mwaka huu wa 2019 ratiba ya maadhimisho hayo itakuwa kama ifuatavyo:-
Siku /Muda
|
Tukio
|
Sehemu
|
J’nne, 2 April 2019
Saa 3.00 Asubuhi
|
Kufanya Ziara na kusoma dua kwenye kaburi la Marehemu Sheikh Aboud Jumbe Mwinyi
|
Migombani, Wilaya ya Mjini
|
|
Wawi, Wilaya ya Chakechake
|
|
Kufanya ziara na kusoma dua katika Kaburi la Marehemu Sheikh Thabit Kombo
|
Chukwani Wilaya ya Magharibi B
|
|
J’tano, 3 April 2019; Saa 3.00 Asubuhi
|
Kufanya ziara na kusoma dua katika Kaburi la Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi wa Awamu ya Nne Marehemu Sheikh Idris Abdul Wakil
|
Makunduchi, Wilaya ya Kusini
|
Ijumaa 5 April 2019 Saa 3.00 Asubuhi
|
Kongamano la Kumuenzi Sheikh Abeid Amani Karume – Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi wa Awamu ya Kwanza
|
Ukumbi wa Makonyo, a Chake chake Pemba
|
J’mosi 6 April 2019 Saa 3.00 Asubuhi
|
Kongamano la Kumuenzi Sheikh Abeid Amani Karume – Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi wa Awamu ya Kwanza
|
Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul Wakil, Kikwajuni, Unguja
|
Mapokezi ya Maandamano ya Vijana ya Siku ya Karume
|
Kisiwandui, Wilaya ya Mjini Unguja
|
|
J’pili 7 Aprili 2019 Saa 1.00 Asubuhi
|
Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Karume
|
Kisiwandui , Wilaya ya Mjini Unguja
|
Ndugu wananchi,
Kwa mnasaba huo, Napenda kuchukua fursa hii kuwaalika rasmi ku
hudhuria katika matukio hayo kwa siku, muda na sehemu zilizoainishwa. Ili kuhakikisha shughuli hii inafanyika kwa amani na utulivu mkubwa, siku ya Jumapili ya tarehe 7 Aprili, 2019 kuanzia saa 12:00 Asubuhi mpaka saa 7:00 Mchana, barabara ya Michenzani ‘round about’ hadi Mkunazini itafungwa kwa vyombo vyote vya usafiri.
Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Zanzibar
AHSANTENI KWA KUNISIKILIZA
Hivyo makala TAARIFA RASMI KUHUSU MAADHIMISHO YA SIKU YA KUMBUKUMBU YA KARUME (KARUME DAY), 2019 ILIYOSOMWA NA KAIMU WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS, MHE. DKT SIRA UBWA MAMBOYA
yaani makala yote TAARIFA RASMI KUHUSU MAADHIMISHO YA SIKU YA KUMBUKUMBU YA KARUME (KARUME DAY), 2019 ILIYOSOMWA NA KAIMU WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS, MHE. DKT SIRA UBWA MAMBOYA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TAARIFA RASMI KUHUSU MAADHIMISHO YA SIKU YA KUMBUKUMBU YA KARUME (KARUME DAY), 2019 ILIYOSOMWA NA KAIMU WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS, MHE. DKT SIRA UBWA MAMBOYA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/04/taarifa-rasmi-kuhusu-maadhimisho-ya.html
0 Response to "TAARIFA RASMI KUHUSU MAADHIMISHO YA SIKU YA KUMBUKUMBU YA KARUME (KARUME DAY), 2019 ILIYOSOMWA NA KAIMU WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS, MHE. DKT SIRA UBWA MAMBOYA"
Post a Comment