WAKAZI MTAA WA JUHUDI MAENEO YA MBAGALA KIZUIANI WAIOMBA HALMASHAURI TEMEKE KUWAJENGEA MITARO KUNUSURU MAKAZI YAO ,

WAKAZI MTAA WA JUHUDI MAENEO YA MBAGALA KIZUIANI WAIOMBA HALMASHAURI TEMEKE KUWAJENGEA MITARO KUNUSURU MAKAZI YAO , - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAKAZI MTAA WA JUHUDI MAENEO YA MBAGALA KIZUIANI WAIOMBA HALMASHAURI TEMEKE KUWAJENGEA MITARO KUNUSURU MAKAZI YAO ,, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAKAZI MTAA WA JUHUDI MAENEO YA MBAGALA KIZUIANI WAIOMBA HALMASHAURI TEMEKE KUWAJENGEA MITARO KUNUSURU MAKAZI YAO ,
kiungo : WAKAZI MTAA WA JUHUDI MAENEO YA MBAGALA KIZUIANI WAIOMBA HALMASHAURI TEMEKE KUWAJENGEA MITARO KUNUSURU MAKAZI YAO ,

soma pia


WAKAZI MTAA WA JUHUDI MAENEO YA MBAGALA KIZUIANI WAIOMBA HALMASHAURI TEMEKE KUWAJENGEA MITARO KUNUSURU MAKAZI YAO ,

WAKATI Mamlaka ya Hali ya Hewa(TMA)ikitangaza uwepo wa mvua nchini,wakazi wa Mbagala Kiuzuiani Mtaa wa Juhudi wameiomba Halmashauri ya Temeke na Mkoa wa Dar es Salaam kuwawekea mifereji au mitaro ya kupitisha maji ili kunusuru makazi yao na watu wa maeneo hayo.

Wamesema katika eneo la Juhudi changamoto kubwa ni maji kujaa katika makazi ya watu ambayo msingi wake mkubwa ni kukosekana kwa mifereji ya kupitisha maji ya mvua,hivyo yanalazimika kupata katika barabara  na matokeo yake yanakwenda kutuama katika makazi ya watu.

Wakizungumza leo wakazi wa mtaa huo wakiongozwa na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Juhudi Athuman Namna, wamesema ombi lao kubwa ni eneo hilo kuwekwa mifereji kwani wanaamini ndio ufumbuzi wa kero ya maji kutuama ambayo ni ya muda mrefu huku wakieleza matumaini yao kwa Serikali ya Awamu ya Tano ambayo imejikita kuwasiliza wanyonge na kutatua kero zao.

Wakati mvua za masika zikianza kushika kasi katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo  mkoa wa Dar es Salaam wakazi wa mtaa wa Juhudi kata ya Kiburugwa wameeleza hofu yao kufuatia mvua hizo.

Wamesema kukosekana kwa mitaro ya kupitisha maji makazi yao  yamekuwa njia ya maji taka na inapofika msimu wa mvua maisha yao wanakuwa hatarini pamoja na uwepo wa magonjwa ya mlipuko yakiwamo ya kipindupindu.

Mkazi wa eneo hilo Hawa Kombo amesema mvua zinaponyesha wakazi wa mtaa huo wanakuwa hatarini kutokana na maji mengi kuelekezwa kwenye nyumba zao.

Amesisitiza wapo roho juu, kwani wakiona dalili ya mvua au manyunyu  wanakosa raha huku akifafanua mvua ikinyesha maji yote ya juu yanakuja kwenye nyumba zao na barabarani nako maji yanajaa na kusababisha njia kutopitika kabisa

“Sasa wapo ambao wanatumia mwanya huo kufungulia vyoo vyao basi hapo ndio hatari inapozidi kuwa kubwa magonjwa kama kipindupindu yanakuwa sehemu ya maisha yetu mvua zikianza,”

Wakati huo huo mkazi mwingine wa eneo hilo Rashid Mgaza amesema kuwa hali ya kufurika maji wakati mwingine inasababisha watoto kushindwa kwenda shuleni kwani kuna wakati maji yanakuwa mengi kiasi cha kufika usawa wa madirisha ya nyumba.

“Mvua zikinyesha wakazi wa Juhudi hatuna amani kwanza hata mtoto akienda shule unakuwa roho juu hayo maji yanayotiririka hata mtu mzima ni hatari kupita sasa ndio apite mtoto.Ombi letu kwa Serikali itusikie huku nako tunaoishi ni watu na kwa kuwa serikali yetu ni ya wanyonge basi itusikie na kutupatia ufumbuzi wa changamoto hii,” amesema Mgaza

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Juhudi Athuman Namna amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na kueleza kuwa imesababishwa na maji yanayotoka maeneo ya juu kukosa mwelekeo na matokeo yake yanashuka chini kwenye makazi ya watu.

Ameongeza kwa nafasi yake na kwa kushirikiana na wananchi wamechukua hatua mbalimbali za kuwasilina na viongozi wa Manispaa ya Temeke lakini bado hawajapata ufumbuzi wa tatizo hilo.

“Tukisikia mvua amani inatoweka huku kwetu na kama hii iliyotangazwa watu wanalazimika kuacha nyumba zao lakini ikitengenezwa mifereji hili tatizo litakuwa historia,”

“Niwaombe viongozi wangu wasikae ofisini waje kuona hali ilivyo maana kwa kuambiwa unaweza usielewe ila ukweli ni kwamba tuna wakati mgumu sana kuelekea hiki kipindi cha mvua,”amesema Namna

Wakazi wengine wamesema hawana tatizo na Serikali kwani wanaimani na ndio maana haja ya kutoa kilio cha hasa kipindi hiki ambacho mvua hazijashika kasi kwani kuna hatari zaidi kama hakutafanyika jitihada za kuwekwa mitaro hivi sasa."

Michuzi Blog ambayo ilifika eneo hilo,imeshuhudia baadhi ya wakazi wakiwa wameacha nyumba zao na kwenda kutafuta maeneo ya kujisitiri wakiohofia mvua ambazo zimeanza kunyesha zinaweza kusababisha madhara .
 Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Juhudi uliko Mbagala Kizuiani Athuman Namna akionesha uharibifu wa makazi ya watu ambao umetokana na maji kutuama eneo hilo kutokana na kukosekana kwa mitaro ya kupitisha maji ya mvua katika mtaa huo.
 Moja ya nyumba ambayo iko hatarini kudondoka kutokana na mvua kuharibu miundombinu ya barabara ambayo inaelezwa ni kutokana na kukosekana kwa mitaro ya kupitisha maji ya mvua na hivyo kusambaa barabarani
 Watoto wakiwa katika barabara ya Mtaa wa Juhudi katika eneo la Mbagala Kizuiani jijini Dar es Salaam.Kwa mujibu wa wakazi wa eneo hilo barabara hiyo ambayo inatagemewa imeharibiwa na maji ya mvua kwani haina mitaro ya kupitisha maji
 Gari ikiwa imesimama baada ya dereva kukwama katika eneo hilo la Mtaa wa Juhudi lililopo Mbagala Kizuiani jijini Dar es Salaam.Barabara hiyo pamoja na maeneo hayo yameharibiwa na mvua na kusababisha kero kwa wananchi walio wengi


Hivyo makala WAKAZI MTAA WA JUHUDI MAENEO YA MBAGALA KIZUIANI WAIOMBA HALMASHAURI TEMEKE KUWAJENGEA MITARO KUNUSURU MAKAZI YAO ,

yaani makala yote WAKAZI MTAA WA JUHUDI MAENEO YA MBAGALA KIZUIANI WAIOMBA HALMASHAURI TEMEKE KUWAJENGEA MITARO KUNUSURU MAKAZI YAO , Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAKAZI MTAA WA JUHUDI MAENEO YA MBAGALA KIZUIANI WAIOMBA HALMASHAURI TEMEKE KUWAJENGEA MITARO KUNUSURU MAKAZI YAO , mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/03/wakazi-mtaa-wa-juhudi-maeneo-ya-mbagala.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WAKAZI MTAA WA JUHUDI MAENEO YA MBAGALA KIZUIANI WAIOMBA HALMASHAURI TEMEKE KUWAJENGEA MITARO KUNUSURU MAKAZI YAO ,"

Post a Comment