title : RC MAKONDA ATOA MAAGIZO MAZITO KWA DC ILALA NA KINONDONI
kiungo : RC MAKONDA ATOA MAAGIZO MAZITO KWA DC ILALA NA KINONDONI
RC MAKONDA ATOA MAAGIZO MAZITO KWA DC ILALA NA KINONDONI
Kufuatia kusuasua kuanza kwa miradi ya kimkakati, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amewaagiza Wakuu wa Wilaya za Ilala na Kinondoni, Wakurugenzi wa manispaa na wakuu wa idara kuhakikisha hadi kufikia Jumanne ya March 26 miradi yote iwe imeanza utekelezaji ikimaanisha kuwa mikataba imesainiwa na mkandarasi yupo kazini.
RC Makonda amefikia hatua hiyo baada ya kuchukizwa kuona miradi haijaanza kutekelezwa hadi sasa licha ya Rais Dkt. John Magufuli kutoa fedha zote za miradi lakini baadhi ya watendaji wamekuwa wakichelewesha kuanza kwa miradi.
Aidha RC Makonda amempa Siku tatu Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bi. Sophia Mjema na Mkurugenzi wa manispaa hiyo kuhakikisha mkataba wa ujenzi wa machinjio ya kisasa Vingunguti unasainiwa mara moja na mkandarasi anaanza kazi.
Hivyohivyo RC Makonda amempa siku tano Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni na Mkurugenzi wake kuhakikisha ujenzi na Maboresho ya ufukwe wa kisasa wa Coco unaanza mara moja.
Mhe. Makonda amesema endapo wahusika watashindwa kutekeleza agizo hilo watatafsiriwa kuwa wameshindwa kusimamia fedha na miradi ya serikali.
Itakumbukwa mwaka jana Rais Dkt.John Magufuli alitoa fedha za kutosha kwaajili ya miradi ya kimkakati ya kuwakwamua wananchi ikiwemo ujenzi wa barabara, hospital, zahanati,vituo vya daladala,maji,umeme,elimu na machinjio ili kupunguza kero za wananchi.

Hivyo makala RC MAKONDA ATOA MAAGIZO MAZITO KWA DC ILALA NA KINONDONI
yaani makala yote RC MAKONDA ATOA MAAGIZO MAZITO KWA DC ILALA NA KINONDONI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RC MAKONDA ATOA MAAGIZO MAZITO KWA DC ILALA NA KINONDONI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/03/rc-makonda-atoa-maagizo-mazito-kwa-dc.html
0 Response to "RC MAKONDA ATOA MAAGIZO MAZITO KWA DC ILALA NA KINONDONI"
Post a Comment