title : MKUU WA WILAYA ASISITIZA KUKAMILISHA MAANDALIZI YA ENEO LA WAJASIRIAMALI
kiungo : MKUU WA WILAYA ASISITIZA KUKAMILISHA MAANDALIZI YA ENEO LA WAJASIRIAMALI
MKUU WA WILAYA ASISITIZA KUKAMILISHA MAANDALIZI YA ENEO LA WAJASIRIAMALI
Mkuu wa wilaya ya Korogwe Mhe. Kissa Gwakisa ametoa agizo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha eneo lililotengwa kwa ajili ya wajasiriamali linaanza kufanyiwa maandalizi ya awali ili kuondoa changamoto ya eneo la kuzalisha kwa mjasiriamali mdogo.
Alitoa maagizo hayo wakati akifungua mafunzo ya TBS kwa wajasiriamali wadogo, yaliyofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya mji wa Korogwe, ambapo wajasiriamali 104 walihudhuria.
Mh.Gwakisa alisema eneo la uzalishaji ni kilio cha wazalishaji wadogo wengi, na hivyo hatua hiyo itawasaidia wajasiriamali hao kupata alama ya ubora kwa bidhaa wanazozalisha.
Kwa upande wake, Afisa masoko mwandamizi wa TBS, Bi. Gladness Kaseka, alitoa shukrani kwa Mkuu wa wilaya kwa kuwajali wajasiriamali hao kwani itawasaidia kupata leseni ya kutumia alama ya ubora na vilevile huduma hiyo kwa mjasiriamali mdogo ni bure.
Kaseka aliwakumbusha kuomba mafunzo maalum TBS, ambapo TBS hufanya kwa kushirikiana na SIDO na TFDA, bila gharama yoyote.
Wajasiriamali waliopata elimu hiyo, wamefurahishwa na Shirika hilo kuwafikia na kuwaongezea uelewa wa Viwango na kuwajulisha juu ya fursa ya bure kwao, kupata leseni ya TBS itawasaidia kuuza bidhaa zao popote na ushindani halali sokoni.
Sambamba na mafunzo hayo Shirika pia lilitoa elimu ya viwango kwa wananchi katika maeneo ya stendi ya zamani ya manundu, stendi mpya, soko la manundu na sabasaba, pamoja na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Nyerere yenye jumla ya wanafunzi na walimu 746.
Mkuu wa wilaya ya Korogwe, Mhe. Kissa Gwakisa, akifungua semina kwa wajasiriamali wadogo juu ya utaratibu wa kupata alama ya ubora ya TBS, katika ukumbi wa halmashauri ya mji wa Korogwe.
Wajasiriamali wakisikiliza mafunzo juu ya utaratibu wa kupata alama ya ubora ya TBS na fursa ya huduma ya bure kutoka kwa maafisa wa TBS
Wananchi wilayani Korogwe wakipata elimu ya viwango kutoka kwa Maafisa Udhibiti Ubora waTBS, Bi. Amina Yassin na Bi. Janeth Kakuru.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nyerere,wilayani Korogwe wakipata elimu kutoka kwa Afisa Masoko Mwandamizi(TBS), Bi. Gladness Kaseka
Hivyo makala MKUU WA WILAYA ASISITIZA KUKAMILISHA MAANDALIZI YA ENEO LA WAJASIRIAMALI
yaani makala yote MKUU WA WILAYA ASISITIZA KUKAMILISHA MAANDALIZI YA ENEO LA WAJASIRIAMALI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MKUU WA WILAYA ASISITIZA KUKAMILISHA MAANDALIZI YA ENEO LA WAJASIRIAMALI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/03/mkuu-wa-wilaya-asisitiza-kukamilisha.html
0 Response to "MKUU WA WILAYA ASISITIZA KUKAMILISHA MAANDALIZI YA ENEO LA WAJASIRIAMALI"
Post a Comment