MGOGORO WA WAKULIMA NA WAFUGAJI KWALA WAPATIWA UFUMBUZI-DR RUHETA

MGOGORO WA WAKULIMA NA WAFUGAJI KWALA WAPATIWA UFUMBUZI-DR RUHETA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MGOGORO WA WAKULIMA NA WAFUGAJI KWALA WAPATIWA UFUMBUZI-DR RUHETA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MGOGORO WA WAKULIMA NA WAFUGAJI KWALA WAPATIWA UFUMBUZI-DR RUHETA
kiungo : MGOGORO WA WAKULIMA NA WAFUGAJI KWALA WAPATIWA UFUMBUZI-DR RUHETA

soma pia


MGOGORO WA WAKULIMA NA WAFUGAJI KWALA WAPATIWA UFUMBUZI-DR RUHETA

 NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA 
TIMU ya kitaifa ya kufuatilia na kutatua migogoro ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi wakiwemo wakulima, imeingilia kati mgogoro uliodumu kwa miaka saba baina ya wakulima na wafugaji wa Kwala,wilayani Kibaha Mkoani Pwani na kufanikiwa kuumaliza .

Mgogoro huo unabaki historia baada ya wafugaji wa bonde la mto Ruvu  ,Mwembe Ngozi kupewa agizo la kuondoka na kuhamia eneo la Waya,  ranchi ya Taifa NARCO iliyopo Ruvu ili kuwaacha huru wakulima ambao walikuwa wakipata hasara kutokana na mazao yao kulishiwa mifugo.  

Mkurugenzi msaidizi wizara ya mifugo na uvuvi, ambae pia ni mwenyekiti wa timu hiyo, Dr. Martin Ruheta, aliwataka wafugaji hao akiwemo Sauti Mbili na Masanja Kidirgo ambao wana ng'ombe zaidi ya 500 waondoke kuanzia march 18 mwaka huu. 
Aliwaomba, wafugaji hao na wengine waondoke huku serikali ikiendelea kutafuta maeneo ya kudumu, kwa wale ambao mifugo haitoenea kwenye ranchi hiyo. 

"Timu hii ilianza kazi mwezi octoba mwaka jana, mkoa wa Kigoma, Katavi, Rukwa, Mbeya ambapo kwa mkoa wa Pwani walianzia Mkuranga, Rufiji, Kisarawe na Leo tunamaliza mgogoro huu hapa Kwala "alifafanua Ruheta. 

Nae mkuu wa wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama alibainisha ,kwasasa hawaombi tena, bali kuanzia jumatatu ijayo waondoke na atakaekaidi akikutwa ng'ombe wake atakuwa halali kwake .

Assumpter aliyaasa, makundi hayo yaheshimiane ili kuondoa migogoro isiyo ya lazima. 

Makamu mwenyekiti wa Chama Cha Wafugaji (CCWT) Esta Moreto alisema ameridhishwa na maagizo hayo ila anaomba wafugaji waondoe mifugo na sio makazi yao kwakuwa wengine wana wanawake wajawazito na watoto. 


Hivyo makala MGOGORO WA WAKULIMA NA WAFUGAJI KWALA WAPATIWA UFUMBUZI-DR RUHETA

yaani makala yote MGOGORO WA WAKULIMA NA WAFUGAJI KWALA WAPATIWA UFUMBUZI-DR RUHETA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MGOGORO WA WAKULIMA NA WAFUGAJI KWALA WAPATIWA UFUMBUZI-DR RUHETA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/03/mgogoro-wa-wakulima-na-wafugaji-kwala.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MGOGORO WA WAKULIMA NA WAFUGAJI KWALA WAPATIWA UFUMBUZI-DR RUHETA"

Post a Comment