title : KAMATI YA BUNGE YA ARDHI. MALIASILI NA UTALII YAPANIA KURUDISHA HADHI YA CHUO CHA MWEKA
kiungo : KAMATI YA BUNGE YA ARDHI. MALIASILI NA UTALII YAPANIA KURUDISHA HADHI YA CHUO CHA MWEKA
KAMATI YA BUNGE YA ARDHI. MALIASILI NA UTALII YAPANIA KURUDISHA HADHI YA CHUO CHA MWEKA
Wizara ya Maliasili na Utalii imesema imeanza kuzifanyia kazi baadhi ya changamoto zinazokikabili Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori, Mweka ili kiendeleze hadhi yake ya kuwa Chuo cha Kimataifa.
Hatua hiyo inakuja kufuatia kupungua kwa idadi ya wanafunzi wa kigeni wanaojiunga na Chuo hicho kila mwaka.
Akizungumza mbele ya Wajumbe wa Kamati Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii iliyotembelea Chuo hicho mkoani Kilimanjaro, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amesema shabaha ya Wizara ni kukiona chuo hicho kikiendelea kuwa na hadhi ya Kimataifa.
Amewaeleza Wajumbe hao kuwa hatua zilizochukuliwa ni pamoja na Wizara kuendelea kufanya mazungumzo na vyombo vya udhibiti na Usimamizi wa Elimu hapa nchini ( TCU na NACTE) ili viangalie namna ya kuondoa masharti magumu yanayosababisha baadhi ya masomo yanayotolewa na nchi nyingine yasitambuliwe chuoni hapo.
Mhe.Kanyasu ameiambia kamati hiyo kuwa sababu nyingine ya idadi ya Wanafunzi wa kigeni kupungua ni baadhi nchi kama Malawi na Kenya kuanzisha vyuo vyao tofauti na ilivyokuwa mwanzo.
Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Shabani Shekilindi amesema Chuo hicho kinakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo za uhaba wa wahadhiri pamoja na uchakavu wa miundombinu.
Amesema kupitia Kamati anayoiongoza atahakikisha kuwa changamoto zote zinapatiwa majibu ili chuo hicho kiendelee kutoa huduma bora.
Amekishauri chuo hicho kiendelee kuzitangaza kozi zake ndani na nje ya nchi.
Naye Mjumbe wa Kamati hiyo Mhe. Boniphace Getere amekishauri chuo hicho kiingie mkataba na watu binafsi kwa ajili kujenga mabweni yatayokayosaidia kutatua changamoto ya wanafunzi 228 kati ya 600 wanaolazimika kupanga nyumba nje ya Chuo hicho.
Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori , Mweka kilianzishwa mwaka 1963 kikiwa na wanafunzi 25 kutoka Kenya, Uganda Malawi , Cameroun na Tanzania.
Hivyo makala KAMATI YA BUNGE YA ARDHI. MALIASILI NA UTALII YAPANIA KURUDISHA HADHI YA CHUO CHA MWEKA
yaani makala yote KAMATI YA BUNGE YA ARDHI. MALIASILI NA UTALII YAPANIA KURUDISHA HADHI YA CHUO CHA MWEKA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KAMATI YA BUNGE YA ARDHI. MALIASILI NA UTALII YAPANIA KURUDISHA HADHI YA CHUO CHA MWEKA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/03/kamati-ya-bunge-ya-ardhi-maliasili-na.html
0 Response to "KAMATI YA BUNGE YA ARDHI. MALIASILI NA UTALII YAPANIA KURUDISHA HADHI YA CHUO CHA MWEKA"
Post a Comment