title : JKCI yaendelea kufanya matibabu maalum ya moyo kwa watoto
kiungo : JKCI yaendelea kufanya matibabu maalum ya moyo kwa watoto
JKCI yaendelea kufanya matibabu maalum ya moyo kwa watoto
Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Godwin Sharau kwa kushirikiana na madaktari kutoka Shirika la Open Heart International (OHI) la nchini Australia wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa kuziba tundu kwenye moyo wakati wa kambi maalum ya matibabu ya moyo ya siku saba inayoendelea katika taasisi hiyo. Jumla ya watoto tisa wamefinyiwa upasuaji wa kuziba matundu na hali zoa zinaendelea vizuri
Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Evarist Nyawawa kwa kushirikiana na madaktari wa Shirika la Open Heart International (0HI) la nchini Australia wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa kubadilisha valvu wakati wa kambi maalum ya matibabu inayoendelea katika taasisi hiyo. Jumla ya watu wazima watano wenye matatizo ya moyo wamefanyiwa upasuaji katika kambi hiyo ya siku saba na hali zao zinaendelea vizuri.
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Lilian Peter kwa kushirikina na wenzake wa Shirika la Open Heart International (OHI) la nchini Australia wakimuhudumia mtoto aliyelazwa katika chumba cha wagonjwa waliopo katika uangalizi maalum (ICU) wakati wa kambi maalum ya matibabu ya moyo ya siku saba inayofanywa katika taasisi hiyo. Jumla ya watoto tisa wamefanyiwa upasuaji na hali zao zinaendelea vizuri. Picha na Genofeva Matemu - JKCI
Hivyo makala JKCI yaendelea kufanya matibabu maalum ya moyo kwa watoto
yaani makala yote JKCI yaendelea kufanya matibabu maalum ya moyo kwa watoto Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala JKCI yaendelea kufanya matibabu maalum ya moyo kwa watoto mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/03/jkci-yaendelea-kufanya-matibabu-maalum.html
0 Response to "JKCI yaendelea kufanya matibabu maalum ya moyo kwa watoto"
Post a Comment