title : Waogeleaji 29 kuiwakilisha Bluefins mashindano ya Isamilo
kiungo : Waogeleaji 29 kuiwakilisha Bluefins mashindano ya Isamilo
Waogeleaji 29 kuiwakilisha Bluefins mashindano ya Isamilo
Muogeleaji wa klabu ya Bluefins Husain Hassanali akichapa maji katika mashindano ya Taliss-IST. Husain ni miongoni mwa waogeleaji watakao shindana katika mashindano ya Isamilo.
Na Mwandishi wetu
Dar es Salaam. Klabu inayokuja juu kwa kasi katika mchezo wa kuogelea nchini, Bluefins imetangaza kikosi cha waogeleaji 29 kwa ajili ya kushindana katika mashindano ya Isamilo yaliyopangwa kuanza ijuu mkoani Mwanza.
Muasisi na Kocha Mkuu wa timu hiyo, Rahim Alidina aliwataja waogeleaji wa kile kuwa ni Alexis Misabo, Filbertha Demello, Maryam Ipilinga, Viva Pujari, Sarah Shariff, Aminaz Kachra, Fatema Manji, Muskan Gaikwad, Aliyana Kachra, Zainab Moosajee na Lina Goyayi.
Waogeleaji wa kiume ni Moiz Kaderbhai, Idris Zavery, Sahal Harunani, Isaac Mukani, Enrico Barretto, Zac Okumu, Hassan Harunani, Mohamedhussein Imran, Husain Hassanali, Burhanuddin Mustansir na Ayaan Shariff.
Wengine ni Kaysan Kachra, Parth Motichand, Shuneal Bharwani, Sahil Chudasama, Salman Yasser, Christian Fernandes na Revocatus Josephat.
Alidina alisema kuwa wamewajumuisha waogeleaji wenye umri wa miaka saba (7) kwa lengo la kuwapa uzoefu wa mashindano kabla ya kushindana katika mashindano ya Taifa yaliyopangwa kufanyika mwezi Aprili.
Alisema kuwa waogeleaji hao wapo katika maandalizi ya mwisho na wanatarajia kuondoka jijini kabla ya Ijumaa ya wiki hii kwenda kuonyesha uwezo wao.
“Haya ni mashindano ya tatu kwa mwaka huu, tulianza na Morogoro na baadaye Taliss-IST. Yote hayo tumefanya vizuri,” alisema.
Alisema kuwa wanatarajia kufanya vyema katika mashindano hayo pamoja na waogeleaji wao kuweka muda mpya wa kuogelea (PBS).
"Timu yetu imekuwa ikifanya vizuri katika mashindano hayo ambayo yanaandaliwa na klabu ya kuogelea ya Mwanza (MSC). Tulishinda mwaka 2016 na mwaka 2017 na 2018 tulimaliza katika nafasi ya pili. Mikakati yetu ni kuweka historia mwaka huu,” alisema.
Hivyo makala Waogeleaji 29 kuiwakilisha Bluefins mashindano ya Isamilo
yaani makala yote Waogeleaji 29 kuiwakilisha Bluefins mashindano ya Isamilo Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Waogeleaji 29 kuiwakilisha Bluefins mashindano ya Isamilo mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/waogeleaji-29-kuiwakilisha-bluefins.html
0 Response to "Waogeleaji 29 kuiwakilisha Bluefins mashindano ya Isamilo"
Post a Comment