title : VIJANA WAASWA KUPIMA AFYA ZAO MARA KWA MARA
kiungo : VIJANA WAASWA KUPIMA AFYA ZAO MARA KWA MARA
VIJANA WAASWA KUPIMA AFYA ZAO MARA KWA MARA
Na Vero Ignatus, Arusha
Wataalam wa afya kwa kushirikiana na shirika la Tupange pamoja wamekutana na vijana mbali mbali mkoani Arusha katika kuhamasisha upimaji wa afya pamoja na kutoa elimu ya uzazi kwa vijana
Wataalamu hao wamekuta na vijana katika eneo la makumbusho ya Azimio la Arusha lengo la kukutana na vijana hao ikiwa ni kuwapa elimu ya uzazi pamoja na kuchangia damu sambamba na kupima afya zao
Akizungumza na Michuzi Blog Mratibu wa afya ya uzazi na mtoto wilaya Arusha Bi Laura chua amesema wameemua kuwa kutanisha ilikuwapa elimu ya uzazi kwani wengi wao hawana elimu ya uzazi hali inayopelekea vijana (kike) nchini kupata mimba zisizo tarajiwa.
“Siku ya leo tumekutana na vijana mbali mbali na vijana waishio hapa mkoani arusha katika kuwapa elimu na kuwa hamasisha katika uchangiaji damu pamoja na upimaji virusi vya ukimwi kwa hiyari pia tuna mikakati mingi kwa mwaka huu katika kuwafikia vijana hawa tumepanga kuweka matamsha mengi ya uhamasishaji na wiki ijayo tumepanga tumeandaa tamasha ambalo litafanyika katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid ili tuwahamasishe vijana.Alisema
Mbali na matamasha ambayo wataandaa wamesema watatumia waandishi habari,pamoja na wasanii katika kuhamasisha vijana kwani vijana wengi wamejawa na imani potofu za kutoamini maswala ya afya hivyo kupelekea vijana wa kike na wakiume kupoteza ndoto zao.
Aidha mratibu wa Mradi wa tupange pamoja amesema vijana wengi hawapati fursa ya kutaka kujifunza hivyo kwa kushirikiana na wataalamu wa afya wamepanga mikakati ya kuwafuata vijana na kuwahamasisha ili watambue maswala ya husuyo afya ya uzazi kwa kuandaa matamasha na kuwatumia waandishi habari katika kuaanda vipindi mbali mbali za uhamasishaji.
Alisisitiza vijana wajitokeze katika fursa hizo ambazo zinatokea katika mkoa wa Arusha kwani wakiwekeza zaidi katika kujifunza na kushiriki katika upimaji wa afya zao watakuwa wanajiwekea usalama katika maisha ya ujana.
Pichani ni baadhi ya vijana waliojitokeza kupata Elimu ya Afya ya Uzazi katika viwanja vya Makumbusho ya Azimio la Jijini Arusha
Mmoja wa waandishi habari Bw onesmo loy akiteta nawili matatu na vijana waliojitokeza maeneo hayo
Baadhi ya watalam wa afya kutoka katika zahanati ya levolosi iliopo arusha(watatu waliosimama) wakiwa tayari kwa ajili yakutoa elimu kwa vijana.
Hivyo makala VIJANA WAASWA KUPIMA AFYA ZAO MARA KWA MARA
yaani makala yote VIJANA WAASWA KUPIMA AFYA ZAO MARA KWA MARA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala VIJANA WAASWA KUPIMA AFYA ZAO MARA KWA MARA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/vijana-waaswa-kupima-afya-zao-mara-kwa.html
0 Response to "VIJANA WAASWA KUPIMA AFYA ZAO MARA KWA MARA"
Post a Comment