title : UHUSIANO KATI YA TANZANIA NA FINLAND WAZIDI KUIMARIKA
kiungo : UHUSIANO KATI YA TANZANIA NA FINLAND WAZIDI KUIMARIKA
UHUSIANO KATI YA TANZANIA NA FINLAND WAZIDI KUIMARIKA
Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki yuko nchini Finland kwa ziara ya kikazi ya siku mbili tarehe 25 hadi 26 Februari. Ziara hiyo imefanyika kufuatia mwaliko kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Finland, Mhe. Timo Soini.Mheshimiwa Waziri ameanza ziara hiyo kwa kukutana na mwenyeji wake, Mheshimiwa Waziri Timo Soini. Kwenye mazungumzo yao, Mawaziri hao wamekubaliana kuboresha ushirikiano kwenye sekta biashara, uwekezaji, mafunzo ya ufundi, kuongeza ajira kupitia sekta ya misitu, kuendeleza ushirikiano katika majukwaa ya kimataifa kwa kuzingatia usawa, pamoja na kuwajengea uwezo wanawake na watoto.
Wakati wa mazungumzo, Waziri Soini wa Finland alipongeza jitihada zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kupambana na rushwa na kusimamia uwajibikaji. Pia, aliipongeza Tanzania kwa kuendelea kuhifadhi wakimbizi na mchango wake katika usuluhishi wa migogoro inayozikabili baadhi ya nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu. Mawaziri hao walikubaliana kuendelea kushirikiana katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za kiusalama ikiwa ni pamoja na biashara ya madawa ya kulevya, biashara haramu ya kusafirisha watu, na matishio ya ugaidi.
Kabla ya mazungumzo hayo, Mheshimiwa Balozi Mahiga alikutana na kufanya mazungumzo na Bw. Sampo Suihko, Mkurugenzi Mkuu wa Chuo cha OMNIA Espoo ambaye alieleza utayari wa Taasisi yake kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kubadilishana uzoefu wa kutoa mafunzo ya elimu ya ufundi yanayoendana na soko la ajira.
Pia, Mheshimiwa Mahiga alifanya mazungumzo na Mheshimiwa Matti Ahtisaari, Rais Mstaafu wa Finland na Mwanzilishi wa Taasisi ya Utatuzi wa Migogoro. Mheshimiwa Ahtisaari aliipongeza Tanzania kwa kazi nzuri inayofanya katika utatuzi wa migogoro kwenye nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu na kusihi kusihi kuendeleza jitihada hizo kwa ustawi wa Dunia nzima.
Vilevile, Balozi Mahiga alifanya mazungumzo na Bw. Jukka Kallio, Makamu wa Rais wa ya Helsinki. Katika mazungumzo hayo, uongozi wa Bandari ya Vuosaari uko tayari kushirikiana na uongozi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania katika kuboresha mifumo (Digitalization) itakayoongeza ufanisi wa Bandari ya Dar es salaam.
Kadhalika, Mheshimiwa Waziri Mahiga alifanya mazungumzo na Jumuiya ya Wafanyabiashara (Business Finland) na Makampuni makubwa ya kibiashara nchini Finland. Wafanyabiasha hao walipongeza jitihada zinazoendelea kufanyika nchini Tanzania katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji. Waliahidi kuwekeza nchini na kushawishi makampuni mbalimbali kuona umuhimu wa kuwekeza nchini Tanzania.
Leo Mheshimiwa Waziri amehitimisha ziara hiyo kwa kufanya mazungumzo na Bi. Anne-Mari Virolainen, Waziri wa Biashara na Maendeleo wa Finland; Bw. Mauri Pekkarinen, Naibu Spika wa Bunge la Finland na baadaye kuzungumza na Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge hilo; na Bw. Juhan Damski, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utabiri wa Hali ya Hewa ya nchini Finland.
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA
USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI
26 Februari 2019
Hivyo makala UHUSIANO KATI YA TANZANIA NA FINLAND WAZIDI KUIMARIKA
yaani makala yote UHUSIANO KATI YA TANZANIA NA FINLAND WAZIDI KUIMARIKA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala UHUSIANO KATI YA TANZANIA NA FINLAND WAZIDI KUIMARIKA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/uhusiano-kati-ya-tanzania-na-finland.html
0 Response to "UHUSIANO KATI YA TANZANIA NA FINLAND WAZIDI KUIMARIKA"
Post a Comment