title : Tuboreshe Sekta ya Elimu katika soko la ajira kimataifa-Makinda
kiungo : Tuboreshe Sekta ya Elimu katika soko la ajira kimataifa-Makinda
Tuboreshe Sekta ya Elimu katika soko la ajira kimataifa-Makinda
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
SPIKA Mstaafu, Anne Makinda, ameshauri kuboresha sekta ya elimu ili kuwahakikisha vigezo vya elimu vya Tanzania vinaendana na vigezo vya kimataifa na Dunia ndiyo inataka tuende hivyo Akizungumza katika mahafali ya 14 ya Chuo Kikuu cha Aga Khan yaliyofanyika juzi jijini Dar es Salaam, Makinda amesema Tanzania haina budi kufanya hivyo kwa sababu ni sehemu ya dunia na haina soko lake yenyewe ya kuajiri hivyo wahitimu wetu wanaweza kufanya kazi Duniani kutokana na elimu waliopata.
“Kama tuko katika dunia vigezo vyetu lazima viendane na wenzetu ili tuwe na elimu itakayotuwezesha kushindana katika soko la dunia, hatuna soko la Tanzania peke yake Aga Khan wamethubu katika uwekezaji katika elimu” amesema Spika Makinda. Makinda amesema ameshangazwa na wastani wa walimu na wanafunzi chuoni hao hali inayoashiria kuwa chuo hicho kinafuata vigezo vya kimataifa katika ufundishaji kwa Mwanafunzi watatu kwa Mwalimu Mmoja.
“Ni mara yangu ya kwanza kufika katika chuo hiki, lakini nafahamu kuwa ndicho chuo cha kwanza Tanzania kutoa shahada ya uuguzi Ila nimeshangazwa na idadi ya walimu yaani walimu wako ishirini wanafunzi 59 inamaana kila mwalimu mmoja anahudumia wanafunzi watatu” alisema Makinda.
Aliwashauri wahitimu wa kada mbalimbali nchini kujitoalea kwa moyo wao wote kusaidia jamii na kutokubali kukatishwa tama na changamoto wanazokutana nazo. Makinda amesema endapo kila mhitimu mmoja wa shahada ya uuguzi na ukunga chuoni hapo atajitolea walau asilimia 35 tu ya muda wake kuwahudumia wagonjwa itawatia nguvu.
Rais wa Chuo Kikuu cha Aga Khan Firoz Rasul amesema chuo hicho kimeendelea kuhakikisha kinatoa elimu bora ambapo mwaka jana mhitimu wa chuo hicho tawi la Dar es Salaam alitajwa kama tuzo ya mwalimu bora wa mwaka nchini Kenya. "Zaidi ni kwamba kwa mara ya pili mhitimu wa Aga Khan ametajwa katika fainali ya kuwania zawadi ya dola milioni katika tuzo za kimataifa za walimu" amesema
Amesema programu mbalimbali wamefanikiwa kuwajengea uwezo na mbinu mpya za ufundishaji zaidi ya walimu 3,000 ambazo zimewanufaisha zaidi ya wanafunzi 100,000. Amesema kwa sasa wanajipanga kuanzisha stashahada ya ualimu kuunga mkono juhudi za Serikali ili kuwaongezea uwezo walimu wa shule za misingi.
Spika Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Anne Makinda akizungumza katika mahafali ya 14 ya Chuo Kikuu Aga Khan yaliyofanyika katika viwanja vya Diamond jijini Dar es Salaam.
Rais wa Chuo Kikuu Aga Khan Firoz Rasul akizungumza akitoa maelezo ya Chuo Kikuu Aga Khan katika Mahafali ya 14 yaliyofanyika katika viwanja vya Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Chuo Kikuu Aga Khan Jaji Mkuu Mstaafu Othman Chande akimtunuku shahada ya Uzamili Abdallah Hoza katika mahafali ya 14 ya Chuo Kikuu Aga Khan yaliyofanyika katika viwanja vya Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.
Wahitimu wakiingia katika mahafali ya 14 ya Chuo Kikuu Aga Khan yaliyofanyika katika viwanja vya Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wahadhiri wa Chuo Kikuu Aga Khan wakiingia Ukumbini katika mahafali ya 14 ya Chuo hicho.
Hivyo makala Tuboreshe Sekta ya Elimu katika soko la ajira kimataifa-Makinda
yaani makala yote Tuboreshe Sekta ya Elimu katika soko la ajira kimataifa-Makinda Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Tuboreshe Sekta ya Elimu katika soko la ajira kimataifa-Makinda mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/tuboreshe-sekta-ya-elimu-katika-soko-la.html
0 Response to "Tuboreshe Sekta ya Elimu katika soko la ajira kimataifa-Makinda"
Post a Comment