title : Total Tanzania Kuzindua Kiwanda chake cha Vilainishi (Lubricants) jijini Dar es Salaam kesho Februari 8, 2019-
kiungo : Total Tanzania Kuzindua Kiwanda chake cha Vilainishi (Lubricants) jijini Dar es Salaam kesho Februari 8, 2019-
Total Tanzania Kuzindua Kiwanda chake cha Vilainishi (Lubricants) jijini Dar es Salaam kesho Februari 8, 2019-
Kampuni ya Mafuta ya Total Tanzania Limited itazindua kiwanda chake cha Vilainishi (Lubricants) kilichoko katika eneo la viwanda la Chang'ombe- Temeke, Dar es Salaam.
Uzinduzi wa kiwanda hiki, kutaifanya kampuni ya mafuta ya Total Tanzania kuwa ndio kampuni pekee ya kimataifa nchini Tanzania yenye kutengeneza vilainishi vyake yenyewe ambapo inatarajiwa itazalisha zaidi ya tani 15,000 za vilainishi kwa ajili ya soko la ndani ya nchi na ziada itauzwa nje nchi.
Kwa zaidi ya miaka 50 ya uwepo wake nchini Tanzania, Kampuni ya mafuta ya Total Tanzania ilikuwa ikiagiza vilainishi vyake kutoka nje ya nchi lakini kuanzia sasa, vilainishi hivyo vinatengenezwa humu humu nchini.
Uzinduzi wa kiwanda hiki, kutaifanya kampuni ya mafuta ya Total Tanzania Limited kuunga mkono kwa vitendo, mkakati wa rais Magufuli na serikali yake ya Awamu ya Tano katika ujenzi wa Tanzania ya Viwanda. Kiwanda hiki licha ya kuchangia katika maendeleo ya taifa kiuchumi na kitekinolojia, pia kitatoa nafasi za ajira kwa Watanzania.
Kwa upande wao, wamiliki wa moja ya vituo vya mafuta vya Total, Total Tageta, Vincent Lymo na mkewe Mary Vincent Lymo, waliishukuru kampuni ya Total kwa kuwaonyesha fursa kutoka kuutumia uwanja huo kwa kufyatulia motafali, hadi kuwa kituo cha kwanza cha mafuta chenye hadhi ya kimataifa, ambacho sasa kitauza vilainishi vya Total
Total Tanzania ni kampuni ya Mafuta ya petroli iliingia nchini Tanzania tangu mwaka1969. Biashara ya Total Tanzania inalenga katika kutoa huduma za usambazaji na uuzaji wa mafuta ya petroli, dizeli vilainishi na bidhaa za mafuta, ambayo ni kuuzwa katika vituo mbalimbali vya mafuta
Total ipo katika nchi zaidi ya 130, na inafanya kila linalowezekana kuboresha maisha watu wa nchi hizo kiuchumi na kijamii kwa kuzingatia uhifadhi wa mazingira husika. End
Kuhusu Kampuni ya Total
Total ni kampuni ya kimataifa ya nishati ya mafuta na gesi ni ni moja ya makapini ya kwanza kabisa ya kimataifa kujihusisha katika nishati ya jua duniani kote. Ina wafanyakazi 100 000 wenye kuchangia dhima ya kampuni : kuzalisha nishati bora na safi na salama, na kuizalisha kwa ufanisi zaidi, nguvu zaidi na ubunifu wa hali ya juu, huku ikiwa ni nishati ya gharama nafuu ili watu wengi waweze kuimudu.
Total ipo katika nchi zaidi ya 130, na inafanya kila linalowezekana kuboresha maisha watu wa nchi hizo kiuchumi na kijamii kwa kuzingatia uhifadhi wa mazingira husika.
Total imeanzisha kampeni kabambe utafutaji na uzalishaji wa mafuta kwa kuongeza idadi ya visima vya mafuta huku ikijitahidi kupata nishati endelevu kwa ajili ya Bara la Afrika kwa sasa na baadae. Total imejikita katika uhamasishaji wa utafutaji vya vyanzo vipya vya nishati kutoa kipaumbele cha elimu ya nishati kwa vijana ili kuendeleza uwezo wa kipekee wa bara hili la Afika kujiletea maendeleo. Mbali na hilo,Kampuni ya Total ndio sambazaji wa kwanza wa bidhaa za mafuta (mafuta ya petroli, dizeli, mafuta ya taa , lami, na GPL, nk) katika bara la Afrika. Shukrani kwa mizizi yake ya kihistoria, ubora wa bidhaa na huduma zake, kutoka jumla ya vituo 4200 vya mafuta katika nchi arobaini barani Afrika. Vituo vya mafuta vya Total ni vituo tegemeo kwa wafanya biashara binafsi na wateja wake. Lengo letu ni kuwezesha upatikanaji mkubwa zaidi wa nishati, ambayo pia inahusisha kuendeleza upatikana wa vyanzo vingi na mbadala vya nishati na kwa gharama nafuu - kama vile nishati ya jua, kwa kuuza vifaa vya nishati ya jua
Total tunasikiliza mahitaji ya wadau wetu, na sisi kwenda nao pamoja nao katika kuendeleza maendeleo ya kiuchumi, ajira, elimu na afya. www.total.com
Kuhusu Total Tanzania
Total Tanzania ni kampuni ya Mafuta ya petroli iliingia nchini Tanzania tangu mwaka1969. Biashara ya Total Tanzania inalenga katika kutoa huduma za usambazaji na uuzaji wa mafuta ya petroli, dizeli vilainishi na bidhaa za mafuta, ambayo ni kuuzwa katika vituo mbalimbali vya mafuta na pia katika idara maalum ndani ya wake shirika hilo. Total Tanzania Limited inatumia utaalamu wake katika kutoa huduma za kuaminika kwa wateja wake kwa mfumo wa kadi maalum “ Kadi ya Total” kwa ajili ya ununuzi wa mafuta na huduma mbalimbali magari katika vituo vya mafuta vya Total Katika kujitanua kibiashara kuelekea kwenye matumizi ya nishati mbadala, kampuni ya Total Tanzania Limited kupitia mradi wake wa Total Access to Solar (TATS) project, inasambaza taa za nishati jua zinazoitwa AWANGO kwa jamii ya Watanzania.
Vincent Lyimo na mkewe Mary Lyimo, wamiliki wa Kituo cha Total Tegeta cha jijini Dar es salaam wakizungumza siku ya uzinduzi wa kituo chao hivi karibuni.
Hivyo makala Total Tanzania Kuzindua Kiwanda chake cha Vilainishi (Lubricants) jijini Dar es Salaam kesho Februari 8, 2019-
yaani makala yote Total Tanzania Kuzindua Kiwanda chake cha Vilainishi (Lubricants) jijini Dar es Salaam kesho Februari 8, 2019- Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Total Tanzania Kuzindua Kiwanda chake cha Vilainishi (Lubricants) jijini Dar es Salaam kesho Februari 8, 2019- mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/total-tanzania-kuzindua-kiwanda-chake.html
0 Response to "Total Tanzania Kuzindua Kiwanda chake cha Vilainishi (Lubricants) jijini Dar es Salaam kesho Februari 8, 2019-"
Post a Comment