title : SERIKALI YAELEKEZA KUSIMAMISHWA KAZI MKUU IDARA YA UTAWALA NA UTUMISHI MANISPAA YA ILALA NA KUWACHUKULIA HATUA ZA KINIDHAMU WATUMISHI WENGINE
kiungo : SERIKALI YAELEKEZA KUSIMAMISHWA KAZI MKUU IDARA YA UTAWALA NA UTUMISHI MANISPAA YA ILALA NA KUWACHUKULIA HATUA ZA KINIDHAMU WATUMISHI WENGINE
SERIKALI YAELEKEZA KUSIMAMISHWA KAZI MKUU IDARA YA UTAWALA NA UTUMISHI MANISPAA YA ILALA NA KUWACHUKULIA HATUA ZA KINIDHAMU WATUMISHI WENGINE

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ofisini kwake jijini Dodoma leo kuhusu kusimamishwa kazi kwa Mkuu wa Idara ya Utawala na Utumishi wa Manispaa ya Ilala Bi. Benadeta Mwaikambo na kuwachukulia hatua za kinidhamu maofisa wanaohusika na Mfumo Shirikishi wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (HCMIS) kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao kikamilifu.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (kushoto) akifafanua kuhusu kusimamishwa kazi kwa Mkuu wa Idara ya Utawala na Utumishi wa Manispaa ya Ilala Bi. Benadeta Mwaikambo wakati akizungumza na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ofisini kwake jijini Dodoma leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, ACP Ibrahim Mahumi na Mwandishi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bi. Aneth Andrew.
………………………….
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro ametoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kumsimamisha kazi Mkuu wa Idara ya Utawala na Utumishi wa Manispaa hiyo, Bi. Benadeta Mwaikambo na kuwachukulia hatua za kinidhamu maofisa wanaohusika na Mfumo Shirikishi wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (HCMIS) kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao kikamilifu.
Dkt. Ndumbaro ametoa maelekezo hayo leo wakati akizungumza na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ofisini kwake jijini Dodoma, kufuatia utafiti uliofanywa kuhusu malalamiko ya watumishi ambao ulibaini Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kuongoza kwa kuwa na malalamiko mengi ya watumishi ikifuatiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.
Dkt. Ndumbaro amefafanua baadhi ya malalamiko hayo kuwa, ni pamoja na kutopandishwa vyeo kwa watumishi kutokana na kutokuwa na taarifa sahihi za watumishi, uhakiki wa vyeti, kuwepo kwa upendeleo katika masuala ya kiutumishi, ushughulikiaji usioridhisha wa masuala ya kiutumishi, uwasilishaji wa madai ya malimbikizo ya mishahara Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora yakiwa hayana usahihi na yenye mapungufu kutokana na uzembe.
Dkt. Ndumbaro ametoa mfano wa madai ya malimbikizo ya mishahara yaliyowasilishwa Ofisi ya Rais-Utumishi ya walimu wastaafu 40 ambapo kati ya hayo, madai 24 yalikuwa sahihi na 16 yalikuwa hayana taarifa sahihi ikiwemo kutogongwa mhuri wa mwajiri kuthibitisha madai hayo na kuongeza kuwa licha ya Manispaa ya Ilala kurejeshewa madai hayo kwa ajili ya marekebisho takribani miezi saba iliyopita lakini hadi sasa ni madai ya wastaafu wawili tu yaliyowasilishwa.
Sanjari na hilo, Dkt. Ndumbaro ameelekeza kuhamishwa kwa Maofisa Utumishi walio chini ya Idara ya Utawala na Utumishi ya Manispaa hiyo kwenda katika halmashauri ambazo hazihudumii watumishi wengi ili waweze kumudu majukumu yao kikamilifu.
Dkt. Ndumbaro ametoa wito kwa watumishi wa umma nchini hususan maofisa wanaoshughulikia masuala mbalimbali ya kiutumishi kufanya kazi kwa weledi, uadilifu na kutatua changamoto za watumishi kwa wakati na kuongeza kuwa ofisi yake itaendelea kufanya ufuatiliaji kwa taasisi zote zinazolalamikiwa.
Hivyo makala SERIKALI YAELEKEZA KUSIMAMISHWA KAZI MKUU IDARA YA UTAWALA NA UTUMISHI MANISPAA YA ILALA NA KUWACHUKULIA HATUA ZA KINIDHAMU WATUMISHI WENGINE
yaani makala yote SERIKALI YAELEKEZA KUSIMAMISHWA KAZI MKUU IDARA YA UTAWALA NA UTUMISHI MANISPAA YA ILALA NA KUWACHUKULIA HATUA ZA KINIDHAMU WATUMISHI WENGINE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YAELEKEZA KUSIMAMISHWA KAZI MKUU IDARA YA UTAWALA NA UTUMISHI MANISPAA YA ILALA NA KUWACHUKULIA HATUA ZA KINIDHAMU WATUMISHI WENGINE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/serikali-yaelekeza-kusimamishwa-kazi.html
0 Response to "SERIKALI YAELEKEZA KUSIMAMISHWA KAZI MKUU IDARA YA UTAWALA NA UTUMISHI MANISPAA YA ILALA NA KUWACHUKULIA HATUA ZA KINIDHAMU WATUMISHI WENGINE"
Post a Comment