SERIKALI KUPELEKA MAJI SAFI NA SALAMA VIJIJI VILIVYOPO KARIBU NA VYANZO VYA MAJI

SERIKALI KUPELEKA MAJI SAFI NA SALAMA VIJIJI VILIVYOPO KARIBU NA VYANZO VYA MAJI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SERIKALI KUPELEKA MAJI SAFI NA SALAMA VIJIJI VILIVYOPO KARIBU NA VYANZO VYA MAJI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SERIKALI KUPELEKA MAJI SAFI NA SALAMA VIJIJI VILIVYOPO KARIBU NA VYANZO VYA MAJI
kiungo : SERIKALI KUPELEKA MAJI SAFI NA SALAMA VIJIJI VILIVYOPO KARIBU NA VYANZO VYA MAJI

soma pia


SERIKALI KUPELEKA MAJI SAFI NA SALAMA VIJIJI VILIVYOPO KARIBU NA VYANZO VYA MAJI

WAZIRI wa Maji Proffesa Makame Mbarawa akizungumza mara baada ya kutembelea chanzo cha Maji cha Amani wilayani Muheza wakati wa ziara yake mkoani Tanga
 WAZIRI wa Maji Proffesa Makame Mbarawa kushoto akimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu
MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza wakati wa ziara hiyo


 WAZIRI wa Maji Proffesa Makame Mbarawa akishuka kwenye tanki kubwa la kuhifadhia maji eneo la Kilapula Jijini Tanga ambayo yatatoka eneo la Pongwe kuelekea wilayani Muheza kupunguza changamoto ya uhaba wa maji kwenye wilaya hiyo
 Mabomba yakiwa yameweka eneo hilo mradi huo mkubwa ukiendelea kutekelezwa
 Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly kushoto akiwa na katibu wa Mbunge wa Jimbo la Muheza kulia kushoto ni PRO wa Mamlaka hiyo Dorrah Killoh
 WAZIRI wa Maji Proffesa Makame Mbarawa kulia akionyeshwa kitu kwenye ramani na Mhifadhi wa Misitu ya Amani wilayani Muheza Mwanaidi Kijazi katika wakati alipotembelea chanzo kikubwa cha Maji wilayani Muheza cha Amani kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo  kulia ni Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly
WAZIRI wa Maji Proffesa Makame Mbarawa katikati akisisitiza jambo kwa viongozi wa wilaya ya Muheza mara baada ya kutembelea chanzo hicho

WAZIRI wa Maji Proffesa Makame Mbarawa amesema serikali kupitia mamlaka za maji watahakikisha wanapeleka huduma ya maji safi na salama kwenye vijiji vilivyopo karibu na vyanzo vya maji ili waendelee kuvitunza viweze kusaidia vizazi vya sasa na vijavyo.

Mbarawa aliyasema hayo wakati alipotembelea chanzo cha Maji cha Amani wilayani Muheza mkoani Tanga ikiwa ni ziara yake ya siku ya pili mkoani hapa ambapo aliwataka wananchi kulinda vyanzo

Alisema haitakuwa na maana iwapo wananchi hao wanaendelea kuvitunza vyanzo vya maji lakini hawana maji safi na salama hivyo watahakikisha nao wanapata huduma hiyo muhimu kwa ustawi wa maisha yao na jamii zao.

Alieleza kwa sababu mwaka 1962 maji yaliyo yakipatikana kwa mtu mmoja yalikuwa mita za ujazo 7862 hivi sasa mtu mmoja kwa mwaka anaweza kutumia maji yaliyopo mita za ujazo 1800 lakini siku hizo kulikuwa na watu milioni 10.6 lakini leo hii watu zaidi ya milioni 50 na watu wanazidi kuongezeka.

“Ndugu zangu Serikali kupitia mamlaka za Maji tutahakikisha wananchi wanaoishi karibu na vyanzo vya maji wanapata huduma ya maji safi kwa maana haitakuwa na maana kama wataendelea kuvitunza vyanzo hivyo wakati wao hawapati maji safi na salama “

“Lakini pia nisisitize kwamba tuhakikishe vyanzo vya maji vilivyopo tunavilinda kwa nguvu zote kwani vinazidi kupungua kutokana na uharibifu wa mazingira pia wananchi wakielimishwa wanaweza kuvitunza, “Alisema.

Aidha aliwataka wananchi hao kuhakikisha wanaendelea kuvitunza vyanzo vya maji ili viweze kusaidia vizazi vya sasa na baadae kwani bila kufanya hivyo chanzo hicho kinaweza kukauka.

“Lakini kitakapokauka watu watafikiria kwenda mto Pangani na huko kunaweza pia kukauka hivyo kuna umuhimu wa kuhakikisha vyanzo hivyo vinatunzwa kwa lengo la kuendelea kuwepo “Alisema.

Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo katika taarifa yake alimueleza Waziri Mbarawa kwamba hali ya upatikani maji wilayani humo eneo la mjini ni asilimia 35 kwa mjini na kipindi cha kiangazi asilimia 18.

Alisema kwa upande wa vijiji upatikanaji wa maji ni asilimia 65 inakuwa ni nafuu kwa sababu baadhi ya maeneo kuna maji yanatiririka sehemu ambazo kumejengwa vyanzo vya maji na hivyo kuyapata kirahisi.

“Mradi wa maji eneo la Muheza mjini ulijengwa mwaka 1977 ukitumia chanzo cha Mkurumuzi kilichopo Magoroto huku kililenga kuwapata huduma hiyo wakazi 8000 lakini kwa sasa sasa wapo wakazi 32000.

Mkuu huyo wa wilaya alimueleza waziri huyo kwamba mpango wao kwa sasa ni kuhakikisha wanapata chanzo cha uhakika ili kupata maji ili kuondosha changamoto kubwa ya wilaya hiyo.

“Kwani mh Waziri wakati wa kiangazi wananchi wananua ndoo moja ya maji kwa sh.1000 jambo ambalo ni changamoto kubwa na hilo linaweza kupatiwa ufumbuzi kwa miradi mikubwa “Alisema

Naye kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu alisema eneo hilo la chanzo lilikuwa kwenye hali mbaya baada ya kuvamiwa na watu waliokuwa wakitafuta madini kabla ya kushirikiana na watu wa maliasili na serikali ya wilaya kwa ajili ya kuimarisha ulinzi na kulirudisha kwenye hadhi yake.

Alisema pia waliwapeleka wataalamu ili kuangalia kama kweli kuna mamdini kwenye eno hilo ili kama wanaweza kuruhusu uchumbaji wa madini ufanyike bila kuathiri chanzo cha maji hivho hivyo taarifa yao bado tunaisubiri.

“Lakini pia niwashukuru Tanga Uwasa wameanza mikakati ya kuwapa maji vijiji vyote vinavyozunguka chanzo hicho kuhakikisha nao wananufaika na hduuma hiyo muhimu badala ya kutumia maji yanayo tiririka “Alisema.





Hivyo makala SERIKALI KUPELEKA MAJI SAFI NA SALAMA VIJIJI VILIVYOPO KARIBU NA VYANZO VYA MAJI

yaani makala yote SERIKALI KUPELEKA MAJI SAFI NA SALAMA VIJIJI VILIVYOPO KARIBU NA VYANZO VYA MAJI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI KUPELEKA MAJI SAFI NA SALAMA VIJIJI VILIVYOPO KARIBU NA VYANZO VYA MAJI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/serikali-kupeleka-maji-safi-na-salama.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "SERIKALI KUPELEKA MAJI SAFI NA SALAMA VIJIJI VILIVYOPO KARIBU NA VYANZO VYA MAJI"

Post a Comment