RAIS DK. SHEIN AWATAKA WAZAZI, WALEZI KUWEKA MAZINGIRA BORA KWA WATOTO KUPATA ELIMU

RAIS DK. SHEIN AWATAKA WAZAZI, WALEZI KUWEKA MAZINGIRA BORA KWA WATOTO KUPATA ELIMU - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa RAIS DK. SHEIN AWATAKA WAZAZI, WALEZI KUWEKA MAZINGIRA BORA KWA WATOTO KUPATA ELIMU, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : RAIS DK. SHEIN AWATAKA WAZAZI, WALEZI KUWEKA MAZINGIRA BORA KWA WATOTO KUPATA ELIMU
kiungo : RAIS DK. SHEIN AWATAKA WAZAZI, WALEZI KUWEKA MAZINGIRA BORA KWA WATOTO KUPATA ELIMU

soma pia


RAIS DK. SHEIN AWATAKA WAZAZI, WALEZI KUWEKA MAZINGIRA BORA KWA WATOTO KUPATA ELIMU


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiangalia moja ya meza mpya zilizoagiziwa kwa ajili ya matumizi ya Skuli za Sekondari na Msingi Zanzibar, baada ya kufungua madarasa manne ya Skuli ya Sekondari ya Mchanga Mdogo Wilaya ya Wete Pemba akiwa katika ziara yake kutembelea Miradi ya Maendeleo.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiangalia moja ya meza mpya zilizoagiziwa kwa ajili ya matumizi ya Skuli za Sekondari na Msingi Zanzibar, baada ya kufungua madarasa manne ya Skuli ya Sekondari ya Mchanga Mdogo Wilaya ya Wete Pemba akiwa katika ziara yake kutembelea Miradi ya Maendeleo.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akikata utepe kuashiria kufungua jengo jipya la Skuli ya Sekondari ya Mchanga Mdogo Wilaya ya Wete Pemba leo.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akiwasili katika viwanja vya Skuli ya Mchanga Mdogo akiwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Riziki Pembe Juma kushoto, wakielekea katika jengo ljipya la Madarasa ya Skuli ya Sekondari ya Mchanga Mdogo kwa ajili ya uwekaji jiwe la msingi, akiwa katika ziara yake Kisiwani Pemba.(Picha na Ikulu)
WANAFUNZI wa Skuli ya Sekondari na Msingi ya Mchanga Mdogo Wilaya ya Wete Pemba, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwahutubia wakati wa hafla ya ufunguzi wa Madarasa ya Skuli ya Sekondari Mchanga Mdogo Pemba.
WANANCHI wa Kijiji cha Mchanga Mdogo Wilaya ya Wete Pemba wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia baada ya hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi Skuli ya Sekondari ya Mchanga Mdogo Pemba.

WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Riziki Pembe Juma akihutubia kabla ya kumkaribisha mgeni rasmin kuwahutubia Wananchi wa Kijiji cha Mchanga Mdogo Wilaya ya Wete Pemba, wakati wa hafla ya ufunguzi wa Jengo la Skuli ya Sekondari Mchanga Mdogo
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Madarasa Mapya ya Skuli ya Sekondari Mchanga Mdogo Wilaya ya Wete Pemba, akiwa katika ziara yake kutembelea Miradi ya Maendeleo Kisiwani Pemba.
WANAFUNZI wa Skuli ya Msingi Mchanga Mdogo Wilaya ya Wete Pemba wakiimba Wimbo wa Sisi Sote Tumengomboka wakati wa hafla ya ufunguzi wa majengo ya Skuli ya Sekondari Mchanga Mdogo Kisiwani Pemba leo.
 

……………………………………………………………………………………..
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amewataka wazazi na walezi kote nchini kuwasaidia na kuwatengenezea mazingira bora watoto wao ili waweze kusoma bila taabu.

Kwa nyakati tofauti, Dk. Shein amesema hayo leo wakati alipofungua jengo la madarasa manne katika skuli ya sekondari Mchangamdogo pamoja na kuweka jiwe la msingi la jengo la madarasa manne katika skuli ya msingi Bopwe, Wilaya ya Wete Pemba.

Huo ni muendelezo wa ziara zake za kukaguwa miradi mbali mbali ya maendeleo pamoja na utekelezaji wa Ilani ya CCM. Dk. Shein aliwataka wazazi an walezi kuepuka kuwatuma watoto kupita kiasi katika masuala yasio na mnasaba wa elimu, kwa msingi kuwa hayaendani na umri walionao, hususan katika suala zima la kujiendeleza kitaaluma.

Alisema wapo baadhi ya wazazi na walezi wanaowatumikisha vibaya watoto wao katika kazi za kujikimu kimaisha ikiwemo biashara, hivyo kuwatwisha mzigo usioendana na wakati wao. Aidha, aliwataka walimu kufanikisha dhana ya ulezi wa wanafunzi kwa kuwabidisha kitaaluma, sambamba na kuwataka kuondokana na vitendo vyote vya uharibifu dhidi ya wanafunzi, ikiwemo udhalilishaji wa kijinsia.

“Mwalimu na mwanafunzi ni mtu na mzee wake mnapaswa kujenga urafiki na sio uadui’, alisema. Vile vile Dk. Shein aliwataka walimu kufanyakazi zao kwa misingi ya taaluma ya ualimu pamoja na kuzingatia maadili ya kazi hiyo, akiweka wazi azma ya Serikali ya kuwachukulia hatua walimu wote watakaobainika kukiuka miongozo na sheria za kazi.

Katika hatua nyengine, Dk. Shein aliwataka wanafunzi kusoma kwa bidii na jitihada zote, akibainisha kutokuwepo kwa sababu zozote zile zitakazomfanya mwanafunzi kushindwa kusoma vizuri kutokana na mazingira bora yaliowekwa na Serikali.

Alisema Serikali itaendelea kuimarisha sekta ya elimu, kwa kukamilisha madarasa saba yanayohitajika katika skuli ya Sekondari Mchangamdogo ili kukidhia mahitaji ya wnaafunzi, sambamba na mahitaji ya skuli zote nchini, kw akuyapatia vifaa vya kufundishia pamoja na samani.

Dk. Shein alirudia kauli yake kwa kusema lengo la Serikali ni kuwajengea mazingira bora wanafunzi ili kuhakikisha inapata wataalamu katika fani zote, akibainisha kuwa wataalamu ndio chachu ya maendeleo ya taifa lolote Duniani.

Alisema Serikali ya awamu ya saba itaendelea kusimamia upatikanaji bora wa elimu bila malipo katika skuli za maandalizi, msingi na sekondari na kubainisha jukumu la Serikali la kuwaondolea dhima wazazi katika uchangiaji wa vifaa.

Dk. Shein aliwahakikishia wazazi na wanafunzi kuwa serikali itaendelea kutekeleza ahadi ya upatikanaji wa elimu na taaluma yenyewe kwa kuimarisha miundombinu na upatikanaji wa samani zote ili kuwawekea mazingira bora ya kielimu wanafunzi. Aidha, alisema pamoja na serikali kukosa uwezo wa kutosha wa kutoa elimu bure katika masomo ya Vyuo Vikuu, itaendleea kutoa mikopo kwa wanafunzi wote wa elimu ya juu.

Nae, Waziri wa Nchi, (OR), Serikali za Mitaa, Tawala za Mikoa na Idara maalum za SMZ, Haji Omar Kheir, alisema Wizara yake itatimiza jukumu la kusimamia sekta ya elimu katika ngazi ya maandalizi na msingi, akibainisha madarasa manne ya Skuli ya msingi Bopwe (yaliowekewa jiwe la msingi) kuwa ni miongoni mwa madarasa 60 yalioendelezwa na Wizara hiyo kupitia mfumo wa Ugatuzi.

Aidha, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Riziki Pembe Juma aliipongeza Serikali katika kusimamia vyema sekta ya elimu pamoja na kuwajengea mazingira mazuri wanafunzi ya kupata elimu.

Mapema, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Madina Majaka , alisema ujenzi wa jengo la madarasa manne katika skuli ya Sekondari Mchangamdogo umegharimu zaidi ya shilingi Milioni 34.4, ambapo utapunguza mlundikano wa wanafunzi madarasani, akibainisha haja ya kupatikana madarasa mengine saba ili kuondokana kabisa na kadhia hiyo.

Aidha, Katibu Mkuu, Wizara nchi (OR), Serikali za mitaa, Tawala za Mikoa na Idara maalum za SMZ, Radhia Rashid alisema ujenzi wa jengo la madarasa manne katika skuli ya msingi Bopwe utagharimu shilingi Milioni 53.6 hadi utakapokamilika, fedha zinatokana na Bajeti ya serikali pamoja na michango ya wananchi.

WAKATI HUO HUO, RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein alisema Serikali imefanya kazi kubwa na ngumu katika kuliimarisha zao la karafuu na hatimae kuleta tija kwa wananchi, hususan wa kisiwa cha Pemba. Alisema bado zao hilo lina umuhimu mkubwa katika uchumi wa Zanzibar , na kusisitiza azma ya serikali katika kuliendleeza kibiashara.

Dk. Shein alisema hayo katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete, alipozungumza na Viongozi na wanachama wa CCM, pamoja na kupokea taarifa ya Utekelezaji wa kazi za Maendeleeo Wilaya Wete kwa kipindi cha Agosti 2017 hadi Disemba, 2018. Alisema amefurahishwa sana na hali ya amani na utulivu iliyopo katika Wilaya hiyo na Mkoa wa Kaskazini Pemba kwa ujumla, hatua iliyotoa fursa kwa wananchi kufanya shughuli zao za maendeleo bila vikwazo.

Aidha, alilipongeza Baraza la Mji wa Wete kwa kukusanya vyema mapato hadi kufikia asilimia 96.6 ya malengo lililopangiwa. Sambamba na hilo Dk. Shein alisema ameridhishwa na hatua za Wilaya hiyo kusajili wanafunzi katika skuli za msingi na maandalizi, kwa kigezo kuwa huo ndio msingi bora wa elimu kuelekea ngazi za elimu ya sekondari.

Alisema changamoto za maji katika maeneo ya Uvinje na Kiuyu Mjini yatapatiwa ufumbuzi, na kuonya tabia ya ubinafsi iliopo kwa baadhi ya watendaji wa Mamlaka ya Maji (ZAWA), Wilayani humo inayodhoofisha upatikanaji wa huduma hiyo. Aidha, Dk. Shein akaukumbusha uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, kukamilisha ujenzi wa Chuo cha Amali Mtamwe ambapo ujenzi wake ulianza takriban miaka minane iliyopita, ukiwa umesita.

Mapema, Waziri wa Nchi (OR), Serikali za mitaa, Tawala za Mikoa na Idara maalum za SMZ, Haji Omar Kheir aliwataka wananchi wanaojishughulisha na biashara za magendo, ikiwemo ya zao la karafuu kuacha mara moja, akibainisha kuwa Serikali itachukuwa hatua za kisheria pamoja na kutaisha mali za wahusika.

Nae, Mkuu wa Wilaya ya Wete, Abeid Juma Ali, alisema miongoni mwa changamoto zilizoikabili Wilaya hiyo atika kipindi hicho ni pamoja na upungufu wa wafanyakazi katika sekta ya Afya, upungufu wa madarasa na walimu katika skuli za msingi na sekondari.

Abdi Shamna, Ikulu Zanzibar


Hivyo makala RAIS DK. SHEIN AWATAKA WAZAZI, WALEZI KUWEKA MAZINGIRA BORA KWA WATOTO KUPATA ELIMU

yaani makala yote RAIS DK. SHEIN AWATAKA WAZAZI, WALEZI KUWEKA MAZINGIRA BORA KWA WATOTO KUPATA ELIMU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala RAIS DK. SHEIN AWATAKA WAZAZI, WALEZI KUWEKA MAZINGIRA BORA KWA WATOTO KUPATA ELIMU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/rais-dk-shein-awataka-wazazi-walezi.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "RAIS DK. SHEIN AWATAKA WAZAZI, WALEZI KUWEKA MAZINGIRA BORA KWA WATOTO KUPATA ELIMU"

Post a Comment