title : MEYA MANISPAA YA TEMEKE ABDALLAH CHAUREMBO ATOA OMBI KWA BENKI YA DUNIA
kiungo : MEYA MANISPAA YA TEMEKE ABDALLAH CHAUREMBO ATOA OMBI KWA BENKI YA DUNIA
MEYA MANISPAA YA TEMEKE ABDALLAH CHAUREMBO ATOA OMBI KWA BENKI YA DUNIA
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
MEYA wa Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam Abdallah Chaurembo ametoa ombi kwa Benki ya Dunia kuendelea kuisaidia fedha Serikali ya Tanzania na hasa ndani ya manispaa hiyo ili kuendelea kutekeleza miradi ya maendeleo ya wananchi.
Chaurembo ametoa ombi hilo wakati maofisa wa Benki ya Dunia walipofanya ziara ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo kupitia Mradi wa Utekelezaji wa Jijii la Dar es Salaam (DMDP).
Maofisa hao wa benki ya dunia wametembelea miradi hiyo wakiongozwa na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Sulemani Jafo.
Akifafanua zaidi kuhusu utekelezaji wa miradi ya DMDP ,Chaurembo amesema katika kufanikisha miradi hiyo wao Temeke waliamua kukopa fedha Benki ya CRDB Sh.Bilioni 20 ambazo zilitumika kulipa fidia wananchi katika baadhi ya maeneo ili kupisha mradi huo.
Ameongeza kwa kumwambia Waziri Jafo kuwa pamoja na kukopa fedha hizo wameendelea kulipa deni bila tatizo na manispaa ya Temeke iko salama kwani utekelezaji wa miradi ya maendeleo unakwenda vizuri.
" Pamoja na kukopa fedha Sh Bilioni 20 kutoka Benki ya CRDB ,tunalipa deni bila tatizo.Pia tunaendelea na kutekeleza miradi mbalimbali ndani ya manispaa yetu.Hivyo Temeke tuko salama sana,"amesema Chaurembo.
Pia amesema wanatoa ombi kwa Serikali ili kupata fedha hizo za fidia kama ambavyo imefanyika kwa manispaa ya Kinondoni na Ilala,hivyo ni vema Serikali Kuu ikawapa fedha hizo.
Wakati huo huo ametumia fursa hiyo kutoa ombi kwa Benki ya Dunia iwapo bajeti yao itaruhusu waendelee kuisaidia fedha Manispaa ya Temeke na kufafanua kuwa mrado wa DMDP unatekelezwa katika kata 12 na hivyo bado kuna kata nyingine ambazo nazo zinahitaji kuendelezwa.
"Tunashukuru Serikali yetu ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dk.John Magufuli ambaye amedhamiria kuboresha maisha ya wananchi kupitia miradi ya maendeleo.
"Kwetu Temeke pamoja na kutambua juhudi hizo tunaomba ombi kwa Benki ya Dunia kuendelea kutusaidia fedha kwa kushirikiana na Serikali yetu ili tuendelee kuboresha maeneo yetu," amefafanua Chaurembo.
Kuhusu namna ambavyo miradi inavyotekelezwa,Chaurembo amesema viongozi wa Manispaa ya Temeke wakiwamo madiwani wamekuwa makini kuhakikisha thamani ya fedha inayotolewa kwa ajili ya miradi hiyo inakwenda sambamba na ubora wa mradi.
"Tumekuwa makini kufuatilia miradi hii ili iandane na fedha inayotolewa.Ndio maana miradi hii kwa Temeke inavutia sana na inatekelezwa kwa kiwango cha hali ya juu," amesema Chaurembo huku akisisitiza kwa usimamizi mzuri wa miradi hiyo ndio maana wanapata ujasiri wa kuomba fedha kwa ajili ya kuendelea kuboresha miundombinu.
Hivyo makala MEYA MANISPAA YA TEMEKE ABDALLAH CHAUREMBO ATOA OMBI KWA BENKI YA DUNIA
yaani makala yote MEYA MANISPAA YA TEMEKE ABDALLAH CHAUREMBO ATOA OMBI KWA BENKI YA DUNIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MEYA MANISPAA YA TEMEKE ABDALLAH CHAUREMBO ATOA OMBI KWA BENKI YA DUNIA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/meya-manispaa-ya-temeke-abdallah.html
0 Response to "MEYA MANISPAA YA TEMEKE ABDALLAH CHAUREMBO ATOA OMBI KWA BENKI YA DUNIA"
Post a Comment