title : MATUKIO MBALIMBALI YA BUNGENI LEO JIJINI DODOMA
kiungo : MATUKIO MBALIMBALI YA BUNGENI LEO JIJINI DODOMA
MATUKIO MBALIMBALI YA BUNGENI LEO JIJINI DODOMA
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akizungumza na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Kazi, Vijana na Ajira), Anthony Mavunde, bungeni jijini Dodoma, Februari 7, 2019.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akizunguma na Naibu Waziri wa Kilimo, Innocent Bashungwa, Bungeni jijini Dodoma, Februari 7, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango, bungeni jijini Dodoma, Februari 7, 2019.
Mbunge wa zamani, Semindu Pawa akitambulishwa bungeni jijini Dodoma, Februari 7, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na walimu na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Ufundi ya Kilosa mkoani Morogoro kwenye viwanja vya bunge jijini Dodoma, Februari 7, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na walimu na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya St. Monica ya Arusha kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Februari 7, 2019. Kushoto kwake ni Mbunge wa Viti Maalum, Cecilia Pareso na kulia kwa Waziri Mkuu ni Mwalimu Mkuu wa shule Msaidizi, Sista Colletah.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na mwanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya Msingi ya Assumption ya Arusha, Ritta Deo Moshi kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Februari 7, 2019. Mtoto huyo na wenzake walikwenda bungeni kujifunza shughuli mbalimbali za Bunge. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Hivyo makala MATUKIO MBALIMBALI YA BUNGENI LEO JIJINI DODOMA
yaani makala yote MATUKIO MBALIMBALI YA BUNGENI LEO JIJINI DODOMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MATUKIO MBALIMBALI YA BUNGENI LEO JIJINI DODOMA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/matukio-mbalimbali-ya-bungeni-leo.html
0 Response to "MATUKIO MBALIMBALI YA BUNGENI LEO JIJINI DODOMA"
Post a Comment