MASHAHIDI KESI YA GUGAI WAENDELEA KUSUBIRI KIBALI

MASHAHIDI KESI YA GUGAI WAENDELEA KUSUBIRI KIBALI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MASHAHIDI KESI YA GUGAI WAENDELEA KUSUBIRI KIBALI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MASHAHIDI KESI YA GUGAI WAENDELEA KUSUBIRI KIBALI
kiungo : MASHAHIDI KESI YA GUGAI WAENDELEA KUSUBIRI KIBALI

soma pia


MASHAHIDI KESI YA GUGAI WAENDELEA KUSUBIRI KIBALI

Na Karama Kenyunko Globu ya Jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imekwama kuendelea na usikilizwaji wa kesi ya utakatishaji fedha na kumiliki mali zisizolingana na kipato chake, inayomkabili aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Rushwa (Takukuru),Godfrey Gugai kutokana na kuchelewa kupatikana kwa kibali cha kuwaita mashahidi kutoka mikoani.

Wakili wa serikali kutoka Takukuru Vitilis Peter ameeleza hayo leo Februari 20.2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba, pindi kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kusikilizwa.

Amedai,  waliomba kibali cha kuwaita mashahidi kutoka mikoani lakini wamepata taarifa kuwa kibali hicho kimepatikana leo na kusababisha wao kushindwa kuandaa mashahidi.

Amedai,  ili shahidi aweze kutoa kuleta kutoa ushahidi akiwa anatokea mkoani ni lazima kipatikane kibali kwa sababu atatakiwa kulipwa.

Haya hivyo,  wakili wa utetezi, Alex Mgongolwa ameuomba upande wa mashitaka kuwataja mashahidi watakaowaleta ili kuweka kumbukumbu ili asipokuja mmoja aletwe shahidi mwengine.

Akijibu hoja hiyo, Wakili Peter amedai hawawezi kutaja majina ya mashahidi hao ila mahakama itambue kuwa mashahidi wawili wanatokea Mwanza na watatu wanatokea Musoma. 

Kufuatia hayo,  Hakimu Simba amewataka upande wa mshitaka kuhakikisha wanaleta mashahidi ili kesi hiyo iweze kuendelea.

Kesi hiyo, imeahirishwa hadi Hakimu hadi Machi 4 na 6, mwaka huu kwaajili ya kuendelea na ushahidi kwa upande wa mashitaka.

Mbali na Gugai, washitakiwa wengine katika kesi hiyo, ni George Makaranga, Leonard Aloys na Yasin Katera.

Gugai na wenzake wanakabiliwa na makosa 43, kati ya hayo, makosa 19 ni ya kughushi, 23 ni utakatishaji fedha na moja ni kumiliki mali zilizozidi kipato halali, ambalo linamkabili Gugai.

Katika kesi ya msingi, Gugai na mwenzake, wanakabiliwa na makosa 43, kati ya hayo 19 ni ya kughushi, 23 ni utakatishaji fedha na moja ni kumiliki mali zilizozidi kipato halali, ambalo linamkabili Gugai.

Gugai anakabiliwa na kosa la kumiliki mali kinyume na kipato chake, ambapo alitenda kosa hilo kati ya January 2005 na Decembea 2015.

Inadaiwa kuwa akiwa Takukuru Dar es Salaam, Gugai alikuwa akimiliki mali za zaidi ya Sh bilioni 3.6 ambazo hazilingani na kipato chake huku akishindwa kuzitolea maelezo.


Hivyo makala MASHAHIDI KESI YA GUGAI WAENDELEA KUSUBIRI KIBALI

yaani makala yote MASHAHIDI KESI YA GUGAI WAENDELEA KUSUBIRI KIBALI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MASHAHIDI KESI YA GUGAI WAENDELEA KUSUBIRI KIBALI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/mashahidi-kesi-ya-gugai-waendelea.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MASHAHIDI KESI YA GUGAI WAENDELEA KUSUBIRI KIBALI"

Post a Comment