title : KAMPUNI YA HALOTEL YALETA HAUWENI KWA WATEJA WAKE, WAZINDUA HUDUMA MPYA YA ROYAL BANDO, TOMATO BANDO.
kiungo : KAMPUNI YA HALOTEL YALETA HAUWENI KWA WATEJA WAKE, WAZINDUA HUDUMA MPYA YA ROYAL BANDO, TOMATO BANDO.
KAMPUNI YA HALOTEL YALETA HAUWENI KWA WATEJA WAKE, WAZINDUA HUDUMA MPYA YA ROYAL BANDO, TOMATO BANDO.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mawasiliano Halotel Bw. Nguyen Van Trung pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Mhina Semwenda kulia, wakiwa na wasanii mbalimbali ambao ni mabalozi wa kampuni hiyo wakigonganisha glasi zenye mvinyo wakati wa uzinduzi wa huduma mpya za kupiga simu Royal Bando na Tomato Bando leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mawasiliano Halotel Bw. Nguyen Van Trung akimmiminia mvinyo msanii wa kizazi kipya Mr. Blue ambaye ni balozi wa kampuni hiyo kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Mhina Semwenda pamoja na wasanii mbalimbali ambao ni mabalozi wa kampuni hiyo wakati wa uzinduzi wa huduma mpya za kupiga simu ya Royal Bando na Tomato Bando zilizozinduliwa leo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya watendaji wa Kampuni ya Mawasiliano Halotel wakiwa katika uzinduzi leo jijini Dar es Salaam.
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel Tanzania imefanikiwa kuzindua huduma mpya ya 'Royal bando' pamoja 'Tomato bando' ambayo inawawezesha wateja kupata huduma ya mawasiliano kwa gharama nafuu kwa kupiga simu ndani na nje ya nchi.
Huduma hiyo mpya kutoka haloteli inampa fursa mteja kupiga bila kikomo simu za ndani na kimataifa pamoja na kutumia intaneti bila kikomo na kuunganishwa moja kwa moja pindi kifurushi kinapokwisha.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Halotel Tanzania, Nguyen Van Trung, amesema huduma ya Royal bando inakwenda kuleta hauweni kwa wateja wote wa halotel.
Amesema kuwa halotel inaendelea kuzingatia ubora na unafuu wa huduma pamoja na kuhakikisha wanakuwa na ubunifu katika kuwafikia wateja wa makundi hapa nchini.
“Leo tunafuraha kubwa kuwatangazia ujio wa huduma mpya ya ‘Royal bundle’ kwani imekuja kukata kiu ya wateja katika maeneo tofauti" amesema Bw. Van Trung.
Amefafanua kuwa anatambua umuhimu wa sekta ya mawasiliano katika shughuli za kiuchumi, hivyo wanapenda kampuni ya halotel kuwa kikwazo katika kufanikisha mpango huo.
Ameeleza kuwa katika kufika malengo mbalimbali leo wameamua kuwatangazia watanzania wote kuwa shilingi 10,000 inaweza kupiga simu za ndani na nje ya nchi ikiwemo India, China, Canada na Marekani bila ya kikomo kwa kutumia intaneti bila ya kikomo, kutuma SMS bila ya kikomo.
Amesema kuwa kama muda wa kifurushi utakapokwisha tutakuunganisha mara kwa mara,” amesema Bw. Van Trung.
Amesema kuwa hiyo ni fursa kwa wateja ambao tayari wamekwisha sajiliwa na Halotel, wakati kwa wateja wapya wao wataungwa moja kwa moja kwa gharama niliyotajwa.
Imeelezwa kuwa faida nyengine za kujiunga na huduma hiyo ni pale shilingi hiyo10,000 kwa mwezi mteja atajipatia muda wa maongezi wa dakika 520 kupiga simu mitandao yote, kifurushi cha intaneti yenye kasi cha GB 2, pamoja na kuwezeshwa SMS 500.
Endapo kifurushi hiki kitafikia ukomo, mteja ataweza kuwasiliana kwa gharama nafuu kabisa.
Mteja ataweza kupiga simu kwenda mitandao yote kwa shilingi 1 tu, atatumia shilingi 2 tu kwa sekunde kupiga simu kimataifa, atajipatia MB 1 kwa shilingi 5 tu, na kutuma SMS kwa shilingi 2.
Katika hatua nyengine Mkurugenzi huyo amefafanua uwepo huduma nyingine ya “TOMATO BANDO” ambayo ni maalum kwa wateja wa Halotel itakayowawezesha kupiga simu bure kwenda halotel kwa dk 5 za mwazo pamoja na kupata salio la ziada la bure la Sh4, 000 ambapo mteja atalitumia kwenye huduma nyingine za halotel (Kwa Mwezi mzima).
Amesema kuwa mteja ataweze kufurahia huduma hiyo kama atakuwa laini ya Halotel ya Tomato ambayo atainunua kwa Sh 8000 ambayo itamuwezesha’ Kupiga simu kwa kila namba yoyote ya Halotel bure kwa dakika 5 za mwanzo.
“Mteja ana uhuru wa kuchagua kuunganishwa moja kwa moja na huduma hii, lakini pia itajumuishwa na vifurushi vilivyobakia alivyojiunga awali au kuamua kujiunga mwenyewe kulingana na uhitaji wake katika mawasiliano" amesema.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Halotel Mhina Semwenda, amesema kuwa wataendelea kuwa ubunifu kila kukicha ili kuweza kuyafikia makundi yote ya wateja katika maeneo yote hapa nchini.
Bw. Semwenda amesema kuwa wanatambua wateja wetu wanapenda huduma zenye ubora wa hali ya juu, kwa gaharama nafuu na zenye uhakika.
Hivyo makala KAMPUNI YA HALOTEL YALETA HAUWENI KWA WATEJA WAKE, WAZINDUA HUDUMA MPYA YA ROYAL BANDO, TOMATO BANDO.
yaani makala yote KAMPUNI YA HALOTEL YALETA HAUWENI KWA WATEJA WAKE, WAZINDUA HUDUMA MPYA YA ROYAL BANDO, TOMATO BANDO. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KAMPUNI YA HALOTEL YALETA HAUWENI KWA WATEJA WAKE, WAZINDUA HUDUMA MPYA YA ROYAL BANDO, TOMATO BANDO. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/kampuni-ya-halotel-yaleta-hauweni-kwa.html
0 Response to "KAMPUNI YA HALOTEL YALETA HAUWENI KWA WATEJA WAKE, WAZINDUA HUDUMA MPYA YA ROYAL BANDO, TOMATO BANDO."
Post a Comment