title : HALIMA MDEE ASHINDWA KUFIKA MAHAKAMANI AKIMUUGUZA MBUNGE MWENZAKE
kiungo : HALIMA MDEE ASHINDWA KUFIKA MAHAKAMANI AKIMUUGUZA MBUNGE MWENZAKE
HALIMA MDEE ASHINDWA KUFIKA MAHAKAMANI AKIMUUGUZA MBUNGE MWENZAKE
Na Karama Kenyunko Globu ya Jamii.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo Februari 7, 2019 imeshindwa kuendelea na usikilizwaji wa kesi kutoa lugha chafu dhidi ya Rais John Magufuli inayomkabili Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee baada mahakama kupewa taarifa kuwa ameshindwa kufika kwa madai kuwa anamuuguza Mbunge Bunda mjini Ester Bulaya mkoani Dodoma.
Hayo yameelezwa mdhamini wa Mdee, Faris Lupomo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa
Lupomo amedai, aliwasiliana na mbunge huyo na kumueleza kuwa atashindwa kufika mahakamani kwa kuwa anamuuguza mbunge mwenzie Bulaya ambaye anaishi naye Dodoma nyumbani kwake na anamuuguzia Katika hospitali ya Bunge mkoani humo.
Wakili wa Utetezi Hekima Mwasipu naye alikiri Mahakamani hapo kwa mshtakiwa huyo hayupo na amepewa taarifa na mdhamini huyo kuwa anamuuguza Bulaya mjini Dodoma.
Baada ya kusikiliza maelezo hayo, Hakimu Simba amesema, sababu zilizotolewa na mdhamini huyo kuhusiana na kushindwa kufika mahakamani kwa mshtakiwa zinaleta ukakasi na kubainisha kuwa zina lengo la kuifanya kesi hiyo isimalizike kwa wakati kwa sababu wapo madaktari na wabunge wengine wanawake ambao wanaweza kumuuguza, sasa tukiruhusu haya yaendelee tutashindwa kumaliza kesi.
"Kiukweli jambo hili linakwaza na linatia wasiwasi kama hii kesi tutaweza kumaliza kwa mwendo huu, tunakubali sababu hiyo ya kuuguza lakini kwa shingo upande,
Kesi hiyo imeahirishwa hadi, Februari 28, mwaka huu kwa aji
Mpaka sasa mashahidi watatu wamekwisha kutoa ushahidi katika kesi hiyo akiwemo Mkuu wa Kituo cha Polisi Urafiki, Mrakibu wa Polisi Batseba Kasanga.
Mdee anadaiwa kutenda kosa hilo Julai 3, mwaka jana maeneo ya Ofisi za Chadema zilizopo mtaa wa Ufipa wilayani Kinondoni, Dar es Salaam ambapo alimtukana Rais Dk John Magufuli kwamba "anaongea hovyohovyo anatakiwa afunge break", kitendo ambacho kingeweza kusababisha uvunjifu wa amani.
Hivyo makala HALIMA MDEE ASHINDWA KUFIKA MAHAKAMANI AKIMUUGUZA MBUNGE MWENZAKE
yaani makala yote HALIMA MDEE ASHINDWA KUFIKA MAHAKAMANI AKIMUUGUZA MBUNGE MWENZAKE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala HALIMA MDEE ASHINDWA KUFIKA MAHAKAMANI AKIMUUGUZA MBUNGE MWENZAKE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/halima-mdee-ashindwa-kufika-mahakamani.html
0 Response to "HALIMA MDEE ASHINDWA KUFIKA MAHAKAMANI AKIMUUGUZA MBUNGE MWENZAKE"
Post a Comment