GIRL IN ACTION INITIATIVE WAZINDUA KAMPENI KUMSITIRI MTOTO WA KIKE

GIRL IN ACTION INITIATIVE WAZINDUA KAMPENI KUMSITIRI MTOTO WA KIKE - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa GIRL IN ACTION INITIATIVE WAZINDUA KAMPENI KUMSITIRI MTOTO WA KIKE, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : GIRL IN ACTION INITIATIVE WAZINDUA KAMPENI KUMSITIRI MTOTO WA KIKE
kiungo : GIRL IN ACTION INITIATIVE WAZINDUA KAMPENI KUMSITIRI MTOTO WA KIKE

soma pia


GIRL IN ACTION INITIATIVE WAZINDUA KAMPENI KUMSITIRI MTOTO WA KIKE

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

TAASISI ya Girl in Action Initiative imezindua kampeni ya siku 40 iliyopewa jina la Msitiri Mtoto wa Kike ambapo kupitia kampeni hiyo wanatarajia kukusanya nguo za ndani pamoja na sidiria ambazo zitagawiwa kwa watoto wa kike na hasa wanafunzi. Akizungumza leo wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo ya Msitiri Mtoto wa Kike Mwanzilishi wa taasisi hiyo Miriam Lukindo Mauki amesema wameizundua kampeni hiyo leo na itafika tamati Machi 13 mwaka huu huku akifafanua asilimia kubwa ya wanafunzi wanatoka kwenye familia zenye kipato cha chini ambapo inafika wakati wanashindwa hata kupata fedha ya kununulia nguo za ndani(Chupi na Sidiria).

"Msitiri wa mtoto wa kike ni kampeni iliyoandaliwa mahususi kwa ajili ya kumsaidia mtoto wa kike ambaye yuko shuleni ili aweze kufikia ndoto yake ya kupata elimu na kampeni hi inazinduliwa leo rasmi Februari 1 hadi Machi 13,2019,"amesema Miriam Mauki kuwa kampeni hiyo imekuja baada ya kuona watoto wengi wa kike huwa wanapata changamoto za kujisitiri katika maungo yao ya siri na hiyo kusababisha wengi wao kukosa umakini na kujiamini wawapo madarasani.

Amefafanua Girl in Action Initiative imeona ni vema kuwasaidia hao watoto wa kike kwa kidogo walichonacho ili kuhakikisha wanasoma kwa furaha na wanajisitiri vyema na kuongeza ukimuinua mtoto wa kike umeinua jamii nzima na njia pekee ya kumuinua mtoto wa kike ni kumpatia elimu.

"Ni ukweli usiopingika Serikali ya Awamu ya Tano inafanya jitihada kubwa kuhakikisha vijana hasa wanawake wanapata elimu bora, na imesaidia kuingiza taulo za kike bila kulipiwa kodi ili kumsaidia mtoto wa kike ajisitiri na hatimaye asome kwa kufaraha na kuzifikia ndoto zake .

"Pamoja na hayo kuna changamoto ndogondogo ambazo zinaweza kuwa ni kikwazo kwa mtoto wa kike kuzifikia ndoto zake kielimu.Kampeni hii itahusisha kukusanya fedha pamoja na nguo za ndani kutoka kwa wasamaria wema, taasisi na asasi mbalimbali ili kuhakikisha kila mtoto mwenye hitaji anafikiwa,"amesema .

Ameongeza kuwa kumjenga mtoto wa kike uwezo wa kujiamini, kumpatia mtoto wa kike elimu ya kujisitiri na baadhi ya mahitaji katika muhimu ya kujisitiri na kumsaidia kuwa huru na furaha ili aweze kufocus katika masomo yake."Kupitia kampeni hii huku tukishirikiana na washika dau wetu na wapenda maendeleo ya mtoto wa kike ili kuwafikia watoto wengi wa kike kadri inavyowezekana."

Miriam Mauki amesema ili kuifanikisha wanaomba kwa yeyote anayewiwa kuwa sehemu ya kampeni hiyo anaweza kutoa mchango wake ambao ni kuanzisha Sh.1000 kwa kutumia namba ya simu ya tigopesa 0677069428 ambayo imesajiliwa kwa jina la Christom Solution na ni imani yake kama jamii itashirikiana kwa pamoja wanaweza kufikia kampeni hiyo kwa kuwafikia hao watoto wa kike wengi zaidi.

Pia amefafanua kabla ya kuzinduliwa kwa kampeni hiyo walifanya utafiti na kubaini kuna idadi kubwa ya watoto wa kike walioko shuleni hawana uwezo wa kununua nguo za ndani na kwamba wakiwa Karatu walibaini kati ya watoto 400 ni wawili tu ndio waliokuwa wamevaa sidiria na watoto hao ndio hata darasani wanaouwezo mkubwa kuliko wengine kimasomo."Kampeni hii ya siku 40 lengo letu ni kuwafikia watoto 1000, hivyo tunaomba jamii kushirikiana nasi kufanikisha kampeni hii."

Kwa upande wake Mmoja wa wahamasishaji wa kampeni hiyo Sadaka Saidambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji Family Dynamics ametumia nafasi hiyo kuiomba jamii ya Watanzania kujitokeza kuchangia ili kufanikisha kupata nguo hizo na hatimaye kutatua changamoto iliyopo kwa wanafunzi hao.

Ametoa ombi kwa wanaohitaji kuchangia ni vema kabla ya kununua sidiria wakawasiliana Girl in Action Initiative ili kupata saizi ya sidiria lakini kwenye nguo ya ndani hizo hazina shida sana huku naye akisisitiza namba ambayo inapaswa kutumika kutuma fedha ni hiyo ya tigopesa lakini wanaendelea kufanya mazungumzo na kampuni nyingine za simu ili kuwasaidia namba ambazo zitatumika kutumia fedha hizo.

"Mtoto wa kike anapojisitiri maungo yake ya siri kuna faida nyingi, kwanza anajiamini sana na anakuwa hana wasiwasi lakini pia mtoto wa kike hasa aliyepevuka anapojisitiri mwili anajiepusha na mafisi ambao wao wakiona tu mwili wa binti wanaingiwa na tamaa na wakati mwingine kufanya ubakaji,"amesema.

Wakati huo huo Mhamasishaji mwingine wa kampeni hiyo ambaye ni MC Mkongwe Sisila Ngalemwa amewataka wazazi wa kiume kuwasiliza watoto wao wa kike ikiwamo kuwasaidia kifedha kununua mahitaji yao muhimu yanayohusu kujisitiri.

Amesema kuwa wapo baadhi ya watoto wa kike wamekuwa na ukaribu mkubwa kuliko mama zao, hivyo ukaribu huo wazazi wa kiume wautumie kuzungumza na watoto zao wa kike huku akishauri ni vema kukawa na bajeti maalumu ya mtoto wa kike ya kila mwezi.

"Miaka ya nyuma ilikuwa ni ngumu mtoto wa kike kukaa na baba yake lakini siku hizi ni jambo la kawaida mtoto wa kike kuwa karibu na baba yake , sababu ziko nyingi na mojawapo ni kwamba anapokuwa na mama kuna baadhi ya mambo wanatofautiana. Kwa mfano mtoto anaweza kuambiwa osha viombo na anapoonesha kutokuwa tayari lazima mama atachukia lakini kwa baba anaona ndio kimbilio lake. Hivyo ni vema wazazi wa kiume watumia nafasi hiyo kuwasaidia watoto wao,"amesema.
 Mhamasishaji wa Kampeni ya Msitiri Mtoto wa Kike MC Reeves Sisila Ngalemwa (wa kwa za kulia)akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo yenye lengo la kukusanya nguo za ndani ili kuwapelekea watoto wake na hasa wanafunzi wenye mahitaji.
 Mhamasishaji wa Kampeni ya Msitiri Mtoto wa kike Sadaka Said(watatu kulia) akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo iliyozinduliwa leo jijini Dar es Salaam.
Mwanzilishi wa Girl in Action Initiative(wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa kampeni ya Msitiri Mtoto wa Kike iliyozinduliwa leo jijini Dar es Salaam.


Hivyo makala GIRL IN ACTION INITIATIVE WAZINDUA KAMPENI KUMSITIRI MTOTO WA KIKE

yaani makala yote GIRL IN ACTION INITIATIVE WAZINDUA KAMPENI KUMSITIRI MTOTO WA KIKE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala GIRL IN ACTION INITIATIVE WAZINDUA KAMPENI KUMSITIRI MTOTO WA KIKE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/girl-in-action-initiative-wazindua.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "GIRL IN ACTION INITIATIVE WAZINDUA KAMPENI KUMSITIRI MTOTO WA KIKE"

Post a Comment