DC KITETO AWATAKA WAFUGAJI NA WAKULIMA KUTOVAMIA MAENEO YA HIFADHI

DC KITETO AWATAKA WAFUGAJI NA WAKULIMA KUTOVAMIA MAENEO YA HIFADHI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DC KITETO AWATAKA WAFUGAJI NA WAKULIMA KUTOVAMIA MAENEO YA HIFADHI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DC KITETO AWATAKA WAFUGAJI NA WAKULIMA KUTOVAMIA MAENEO YA HIFADHI
kiungo : DC KITETO AWATAKA WAFUGAJI NA WAKULIMA KUTOVAMIA MAENEO YA HIFADHI

soma pia


DC KITETO AWATAKA WAFUGAJI NA WAKULIMA KUTOVAMIA MAENEO YA HIFADHI


Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara, mhandisi Tumaini Magessa akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya hiyo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara, Lairumbe Mollel akifungua kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya hiyo.

Diwani wa kata ya Makame Wilayani Kiteto Mkoani Manyara, Jacob Nini (CCM) akiapishwa baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo, awali alijiuzulu kwa kuondoka Chadema kwa kumuunga mkono Rais John Magufuli na Mkuu wa mkoa huo Alexander Mnyeti.
 
…………………….
MKUU wa Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara, mhandisi Tumaini Magessa amewataka wakulima na wafugaji kutovamia maeneo ya hifadhi kwa kupotosha kauli ya Rais John Magufuli aliyoitoa hivi karibuni juu ya vijiji 366 vinavyopakana na hifadhi. 

Mhandisi Magessa aliyasema hayo wakati akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo. Mhandisi Magessa alisema baadhi ya wafugaji na wakulima hawakuelewa ipasavyo taarifa ya hiyo hivyo kusababisha upotoshwaji. 

Alisema baada ya taarifa hiyo kutolewa baadhi ya wafugaji na wakulima walijiandaa kulima na kufugia mifugo ambayo itasababisha migogoro upya.
“Kwenye hivyo vijiji 366 vilivyotajwa na Rais Magufuli na kunufaika na tamko hilo sisi Kiteto tuna vitongoji viwili pekee sasa hao wengine wasiokuwepo wasijiingize huko,” alisema mhandisi Magessa. 

Alisema utaratibu ulishawekwa vizuri juu ya maeneo hayo na wao kama serikali ya wilaya hawatakubali kuona watu wachache wanawaingiza kwenye migogoro. Diwani wa Kata ya Partimbo, Paul Tunyoni alisema baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto linapaswa kumpongeza Rais Magufuli kwa kuwajali wafugaji na wakulima. 

Tunyoni alisema kauli ya Rais Magufuli ya kuwajali wanyonge na kuhakikisha jamii ya wafugaji na wakulima wanafaidi rasilimali zilizopo ni jambo la kupongezwa. 
Hata hivyo, mbunge wa jimbo la Kiteto, Emmanuel Papian alisema pori la akiba la Mkungunero linatambulika kisheria hivyo baadhi ya viongozi wasipotoshe hilo. Papian alisema kumekuwepo na wapotoshaji juu ya kauli ya Rais Magufuli juu ya sehemu zenye migogoro ya hifadhi na jamii inayowazunguka. 


Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Lairumbe Mollel alisema wananchi wanapaswa kuwa watulivu wakati huu ambapo serikali inaweka utaratibu vizuri. Mollel alisema wananchi wote wanapaswa kusubiri ili uhakiki ufanyike kwa ushirikishwaji wa uwazi kuliko kuingia sehemu zisizoruhusiwa na kuzua migogoro upya.


Hivyo makala DC KITETO AWATAKA WAFUGAJI NA WAKULIMA KUTOVAMIA MAENEO YA HIFADHI

yaani makala yote DC KITETO AWATAKA WAFUGAJI NA WAKULIMA KUTOVAMIA MAENEO YA HIFADHI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DC KITETO AWATAKA WAFUGAJI NA WAKULIMA KUTOVAMIA MAENEO YA HIFADHI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/dc-kiteto-awataka-wafugaji-na-wakulima.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "DC KITETO AWATAKA WAFUGAJI NA WAKULIMA KUTOVAMIA MAENEO YA HIFADHI"

Post a Comment