title : ABIRIA MBEZI MWISHO WALIA NA GHARAMA KUBWA ZA CHOO YA UMMA
kiungo : ABIRIA MBEZI MWISHO WALIA NA GHARAMA KUBWA ZA CHOO YA UMMA
ABIRIA MBEZI MWISHO WALIA NA GHARAMA KUBWA ZA CHOO YA UMMA
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
ABIRIA na wafanyabiashara ndogondogo katika kituo cha daladala cha Mbezi mwisho jijini Dar es salaam wamelalamikia gharama kubwa ya choo cha umma kilichopo kituoni hapo, huku wakisema kuwa gharama hiyo imekuwa tofauti na vituo vingi vya daladala.
Wakizungumza na globu ya jamii kwa nyakati tofauti baadhi ya abiria na wafanyabiashara kituoni hapo wamesema kuwa malipo ya shilingi 500 kwa kulipia huduma ya choo ni kubwa sana ukilinganisha na sehemu nyingi ambazo bei yake ni shilingi 200 na wameomba mamlaka inayosimamia huduma hiyo kuiangalia kwa mara ya pili hasa kwa kupunguza gharama.
Kwa upande wao madereva na makondakta wa daladala wamesema kuwa wanalazimika kutumia mifuko ya plastiki au chupa za maji kama vyoo na hiyo yote ni kuepuka gharama hiyo.
"Tunakaa hapa kituoni muda mwingi kwa siku unaweza kutumia hata shilingi 5000 kwenda chooni tuu, ni bora tutumie tuu chupa ili kuokoa gharama" ameeleza mmoja wa dereva anayefanya safari zake kutoka Mbezi hadi Makumbusho.
Hadi Globu ya jamii inaondoka eneo la tukio haikufanikiwa kuwapata wahusika wa huduma hiyo kituoni hapo jitihada za kuwapata zinaendelea.
Muonekano wa bei za huduma ya choo katika kituo cha mabasi Makumbusho jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa bei za huduma ya choo katika kituo cha mabasi Mbezi mwisho jijini Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Massaka, Blogu ya jamii)
Hivyo makala ABIRIA MBEZI MWISHO WALIA NA GHARAMA KUBWA ZA CHOO YA UMMA
yaani makala yote ABIRIA MBEZI MWISHO WALIA NA GHARAMA KUBWA ZA CHOO YA UMMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala ABIRIA MBEZI MWISHO WALIA NA GHARAMA KUBWA ZA CHOO YA UMMA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/abiria-mbezi-mwisho-walia-na-gharama.html
0 Response to "ABIRIA MBEZI MWISHO WALIA NA GHARAMA KUBWA ZA CHOO YA UMMA"
Post a Comment