title : YANGA YAONDOLEWA MICHUANO YA SPORTPESA
kiungo : YANGA YAONDOLEWA MICHUANO YA SPORTPESA
YANGA YAONDOLEWA MICHUANO YA SPORTPESA
Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii
Timu ya Yanga imekuwa timu ya pili kuondolewa kwenye michuano ya Sportpesa baada ya kukubali kichapo cha goli 3-2 kutoka kwa Kariobang Sharks.
Mchezo huo wa pili ulizikutanisha timu hizo katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam na KK Sharks kufanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali.
Ilichukua dakika 10 kwa KK Sharks kuandika goli la kwanza kupitia kwa mchezaji wake Duke Abuye.Yanga waliendelea kupambana kupata goli la kusawazisha wakishindwa nafasi walizozipata na kuwapa nafasi wapinzani wao kufanya mashmbulizi ya mara kwa mara langoni mwao.
Katika dakika ya 37 mchezaji wa KK Sharks anaipatia timu yake goli la pili na kuelekea mapumziko wakiwa wanaongoza kwa jumla ya goli 2-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kutafuta namna ya kufanya marekebisho ya makosa ya kipindi cha kwanza kwa kusaka magoli ya kusawazisha.
Mshambuliaji wa Yanga Amisi Tambwe anaipatia Yanga goli la kwanza kwenye dakika ya 86 ya kipindi cha pili na haikuchukua mda mrefu Duke Abuye wa KK Sharks anaiandikia Timu yake goli la 3 dakika za nyongeza na kupeleka simanzi zaidi kwa Yanga.
Dakika ya 90+5 Tambwe anaipatia timu yake goli la 2 na kupelekea matokeo kuwa 3-2. Mpaka dakika 90 za mtanange huo unamalizika Yanga inakuwa timu ya pili baada ya Singida United kuaga mashindano hayo kwa jumla ya goli 3-2.
Michuano hiyo inaendelea tena kesho kwa Gor Mahia kuumana na Mbao Fc huku Simba wakishuka dimbani kuvaana na AFC Leopard na mshindi wa michuano hii atacheza na timu ya Everton kutoka Ligi Kuu Uingereza zote zikiwa ni timu zinazodhaminiwa na kampuni ya ubashiri Sportpesa.
Wachezaji wa Kariobang Sharks wakiwa wanashaangalia baada y kufanikiwa kuiondoa Yanga kwenye hatua ya robo fainali ya Michuano ya Sportpesa leo katika dimba la Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Hivyo makala YANGA YAONDOLEWA MICHUANO YA SPORTPESA
yaani makala yote YANGA YAONDOLEWA MICHUANO YA SPORTPESA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala YANGA YAONDOLEWA MICHUANO YA SPORTPESA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/yanga-yaondolewa-michuano-ya-sportpesa.html
0 Response to "YANGA YAONDOLEWA MICHUANO YA SPORTPESA"
Post a Comment