WANANCHI WATAKIWA KUTUNZA MIUNDO MBINU YA MAJI

WANANCHI WATAKIWA KUTUNZA MIUNDO MBINU YA MAJI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WANANCHI WATAKIWA KUTUNZA MIUNDO MBINU YA MAJI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WANANCHI WATAKIWA KUTUNZA MIUNDO MBINU YA MAJI
kiungo : WANANCHI WATAKIWA KUTUNZA MIUNDO MBINU YA MAJI

soma pia


WANANCHI WATAKIWA KUTUNZA MIUNDO MBINU YA MAJI

Mkurugenzi wa uzalishaji na usambazaji maji wa DAWASA, Injinia Aron Joseph akiwaonyesha Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA iliyoongozwa na Mwenyekiti wao Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange (kwanza kulia) jinsi maji yanavyovunwa katika Mtambo wa Ruvu Juu - Ruvu Kibaha - Pwani. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 
Wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) wakiongozwa na Mwenyekiti Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange wakiwa wamefika katika mtambo wa Ruvu Juu ikiwa ni ziara kwa ajili ya kujifunza baadhi ya mambo mbali mbali. 
Ziara ikiendelea.
Mkurugenzi wa uzalishaji na usambazaji maji wa DAWASA, Injinia Aron Joseph akiwaonyesha Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA iliyoongozwa na Mwenyekiti wao Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange (kwanza kulia) mitambo ya mashine za maji eneo la Ruvu Juu walipofanya ziara ya kwa ajili ya kujifunza. 
Mkurugenzi wa uzalishaji na usambazaji maji wa DAWASA, Injinia Aron Joseph akiwaongoza Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA iliyoongozwa na Mwenyekiti wao Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange (kwanza kulia) mitambo ya kusafisha maji enwalipofanya ziara ya kwa ajili ya kujifunza. 
Mkurugenzi wa uzalishaji na usambazaji maji wa DAWASA, Injinia Aron Joseph akitoa maelezo. machache. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA na Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange wakionyeshwa mitambo ya mashine za maji.
Meneja wa DAWASA Kibaha - Pwani, Crossman Makere akitoa ripoti mbele ya Wakurugenzi Bosi ya DAWASA mara baada ya kutembelea ofisini hapo. 
Wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) wakiongozwa na Mwenyekiti Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange wakiwasili katika mradi wa ujenzi wa Kituo cha Kusukuma maji na nyumba za wafanyakazi eneo la Kibamba, Ubungo kujionea walipofikia. 
Msimamizi wa Mradi wa ujenzi wa kituo cha Kusukuma maji na nyumba za wafanyakazi eneo la Kibamba injinia Ishmaeli Kakwezi akitoa maelezo kwa Wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) wakiongozwa na Mwenyekiti Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange. 
Msimamizi wa Mradi wa Kisarawe na Kibaha injinia Ishmaeli Kakwezi akitoa maelezo mbele ya Wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) wakiongozwa na Mwenyekiti Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange mara baada ya kufika eneo la Minarani Kisarawe, Pwani kujionea ujenzi wa tanki la maji. 
Mafundi wakiendelea na kazi. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Jenerali Mstaafu Mwamunyange akiwa na Wajumbe wa Bodi wakitoa ufafanuzi juu ya masuala mbali mbali yahusuyo miradi hiyo mara baada ya kufanya ziara ya kujifunza wanavyofanyakazi. Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii. 

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Jenerali Mstaafu Mwamunyange amewataka wananchi wa maeneo yanayozunguka miradi ya maji ikiwemo miundo mbinu kuweza kuitunza ili iweze kudumu. Jenerali Mstaafu Mwamunyage akiwa na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi DAWASA wameanza ziara ya siku tatu ya kutembelea miradi mbalimbali ya mamlaka hiyo katika Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.

 Akizungumza baada ya kumaliza siku ya kwanza Jenerali Mstaafu Mwamunyange amewataka wananchi kutunza miundo mbinu ya maji ili iweze kuwapatia maji safi na salama. "Niwaombe wananchi watunze miundo mbinu ya maji maana ujenzi wake ni gharama sana tofauti na wao wanavyofikiria wanapoona maji yamewafia majumba," amesema Jenerali Mstaafu Mwamunyange. Ziara hiyo ilianzia katika chanzo cha maji cha Mto Ruvu Juu, Ofisi ya DAWASA ya Kibaha, Tenki la Kibamba lenye ujazo wa lita Milioni 10 na ujenzi wa tanki la Kisarawe lenye ujazo wa Lita Milioni sita. 

Katika ziara yake Mwamunyage ametembelea pia Ujenzi wa mradi wa bomba la maji kutoka Kibamba (Bomba kuu la kusafirisha maji kutoka Ruvu juu) hadi Kisarawe utakaokuwa na uwezo wa kuzalisha maji Lita Milioni 4 kwa siku na wananchi mbalimbali wa maeneo ya Kisarawe watafaidika na maji. Amesema kuwa, ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa tenki hilo na kama wakandarasi wataendelea hivyo kufikia mwezi Septemba mwaka huu ujenzi utakua umekamilika. 

Katika mradi huo Jenerali Mstaafu Mwamunyange ametembelea tenki la maji lenye ukubwa wa lita milioni 10 kwenye eneo la Kibamba na kuoneshwa pampu nne za kusukumia maji hadi Kisarawe. Kazi zingine zinazoendelea kutekelezwa na Mamlaka hiyo kwenye mradi wa Kisarawe ni ujenzi wa bomba la kusafirishia maji lenye kipenyo cha inchi 16 urefu wa Km 15.65, mabomba ya kusafirisha na kusambaza maji kwenda kwenye maeneo ya Viwanda lenye urefu wa Km 5.15 na kipenyo cha inchi 12 na lingine likiwa ni urefu wa Km 8 na kipenyo cha inchi 8.9 Ujenzi wa tenki la kuhifadhia na kusambaza maji lenye ukubwa wa Lita milioni 6 katika eneo la Mnarani Kisarawe na ujenzi wa Kituo cha Kusukuma maji na nyumba za wafanyakazi eneo la Kibamba. Maeneo yatakayofaidika na mradi huo ni kata ya Kisarawe, Kata ya Kazimzumbwi pamoja na maeneo ya Kiluvya, Kisopwa, Mloganzila na maeneo maalumu ya viwanda.


Hivyo makala WANANCHI WATAKIWA KUTUNZA MIUNDO MBINU YA MAJI

yaani makala yote WANANCHI WATAKIWA KUTUNZA MIUNDO MBINU YA MAJI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WANANCHI WATAKIWA KUTUNZA MIUNDO MBINU YA MAJI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/wananchi-watakiwa-kutunza-miundo-mbinu.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WANANCHI WATAKIWA KUTUNZA MIUNDO MBINU YA MAJI"

Post a Comment