title : VIONGOZI NA WANANCHI WILAYANI NEWALA WAJUMUIKA NA WAZIRI MKUCHIKA KUOMBOLEZA KIFO CHA MAMA TECLA MKUCHIKA
kiungo : VIONGOZI NA WANANCHI WILAYANI NEWALA WAJUMUIKA NA WAZIRI MKUCHIKA KUOMBOLEZA KIFO CHA MAMA TECLA MKUCHIKA
VIONGOZI NA WANANCHI WILAYANI NEWALA WAJUMUIKA NA WAZIRI MKUCHIKA KUOMBOLEZA KIFO CHA MAMA TECLA MKUCHIKA
Viongozi mbalimbali wa serikali, dini, vyama vya siasa, watumishi wa umma na wananchi wilayani Newala wamejitokeza kwa wingi kuungana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt. (Mst) George Mkuchika (Mb) kuomboleza kifo cha mama yake mzazi, Bibi Tecla Bernadetha Mkuchika aliyefariki tarehe 2, 2019 akiwa na umri wa miaka 93 na kuenzi mchango alioutoa katika taifa enzi za uhai wake akiwa mtumishi wa umma na mtumishi katika hospitali zinazoendeshwa na taasisi za kidini.
Akisoma wasifu wa marehemu wakati wa ibada takatifu ya mazishi iliyofanyika katika Kanisa la Anglikana la Msalaba Mtakatifu lililopo kijiji cha Nambunga wilayani Newala, Msemaji wa familia Bw. Noel Boma alisema marehemu alijiunga na Mafunzo ya Ukunga katika Chuo cha kanisa Anglikana (UMCA) mwaka 1943 na mara baada ya kuhitimu alianza kazi St. Mary’s Hospital Newala.
Bw. Boma aliongeza kuwa, marehemu Bibi Mkuchika alihamishiwa Serikalini kutokana na uchapakazi wake, weledi na uadilifu aliokuwa nao wakati akifanya kazi kwenye zahanati ya kanisa la Nambunga na Mnyambe.
Bw. Boma aliainisha kuwa, marehemu akiwa serikalini alifanya kazi katika zahanati za Mihambwe, Mchichira, kitangari, Kilidu na Nambunga mpaka anastaafu.
Aidha, Bw. Boma alisisitiza kuwa, marehemu Bibi. Mkuchika ataendelea kukumbukwa na jamii kwa mchango wake mkubwa alioutoa wakati akihudumu Zahanati ya Kilidu ambayo hivi sasa inatambulika kama Samora kwa kitendo cha kushiriki kikamilifu kutoa huduma usiku na mchana kwa majeruhi wa vita vya ukombozi wa Msumbiji ambavyo vilipamba moto wakati huo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akiwaongoza wanafamilia kuwasha mishumaa juu ya kaburi la Bibi Tecla B. Mkuchika, aliyefariki tarehe 2 Januari, 2019 katika Hospitali ya Misheni Ndanda alikopelekwa kupatiwa matibabu.
Askofu wa Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Masasi, Dkt. James Almasi Askofu Mstaafu Dkt. Mwachiko Boma, Askofu Oscar Mnung’a wa Dayosisi ya Newala na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakiwa katika ibada ya mazishi ya mama mzazi wa Mhe. Mkuchika kabla ya kumpumzisha mama Tecla B. Mkuchika katika nyumba yake ya milele kijiji cha Nambunga Wilayani Newala.
Baadhi ya waombolezaji waliojitokeza kushiriki ibada ya mazishi ya Bibi Tecla B. Mkuchika ambaye ni mama mzazi wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb), aliyefariki tarehe 2 Januari, 2019 katika Hospitali ya Misheni Ndanda alikopelekwa kupatiwa matibabu.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akiwa na ndugu zake wakiweka shada la maua kwenye kaburi la mama yao mpendwa, Bibi Tecla B. Mkuchika aliyefariki tarehe 2 Januari, 2019 katika Hospitali ya Misheni Ndanda alikopelekwa kupatiwa matibabu.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiweka shada la maua kwenye kaburi la mama mzazi wa Mhe. Mkuchika, Bibi Tecla B. Mkuchika aliyefariki tarehe 2 Januari, 2019 katika Hospitali ya Misheni Ndanda alikopelekwa kupatiwa matibabu.

Hivyo makala VIONGOZI NA WANANCHI WILAYANI NEWALA WAJUMUIKA NA WAZIRI MKUCHIKA KUOMBOLEZA KIFO CHA MAMA TECLA MKUCHIKA
yaani makala yote VIONGOZI NA WANANCHI WILAYANI NEWALA WAJUMUIKA NA WAZIRI MKUCHIKA KUOMBOLEZA KIFO CHA MAMA TECLA MKUCHIKA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala VIONGOZI NA WANANCHI WILAYANI NEWALA WAJUMUIKA NA WAZIRI MKUCHIKA KUOMBOLEZA KIFO CHA MAMA TECLA MKUCHIKA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/viongozi-na-wananchi-wilayani-newala.html
0 Response to "VIONGOZI NA WANANCHI WILAYANI NEWALA WAJUMUIKA NA WAZIRI MKUCHIKA KUOMBOLEZA KIFO CHA MAMA TECLA MKUCHIKA"
Post a Comment