title : UWT YAWATAKA VIONGOZI KUJENGA MSHKAMANO KUTATUA KERO ZA JAMII
kiungo : UWT YAWATAKA VIONGOZI KUJENGA MSHKAMANO KUTATUA KERO ZA JAMII
UWT YAWATAKA VIONGOZI KUJENGA MSHKAMANO KUTATUA KERO ZA JAMII
Wananchama na viongozi wa Umoja wa Wanawake nchini (UWT) wametakiwa kujenga mshikamano na umoja sanjari na kuhamasisha wenzao kuungana kwa pamoja kujenga maendeleo na kuibua kero mbali mbali ili ziweze kupatiwa ufumbuzi na serikali.
Akiongea kwenye kikao cha majumuisho kilichoshirikisha mikoa ya Singida,Manyara,Tanga,Kilimanjaro na wenyeji Arusha Katibu mkuu wa umoja huo Queen Mlonzi amewaambia kuwa upendo ndio silaha kuu ya wanawake katika kukabiliana na majukumu ya ujenzi wa taifa na Familia hivyo mafunzo waliotoa ni shemu ya kujenga jamii.
Amewataka wanawake kujenga na kuacha kupeleka maneno huko na huko kwani wao ni sehemu ya taifa na wanamchango mkubwa wa kuisaidia nchi kufikia malengo tarajiwa ya uchumi wa kati mbali na changamoto mbali mbali wanazokutana nazo.
“Kwenye ziara hii tumekutana na changamoto mbali mbali za migogoro ya wananchi ikiwemo lishe duni,elimu,ukekektaji na ndoa za utotoni haya tumeyafundisha kwenye semina zetu kote tulipo pita nyie viongozi mkawe mabalozi wazuri wa kuhubiri na kuyafanyia kazi hizi changamoto kwenye jamii zenu zinazowazunguka”alisisitiza Mlonzi.
Kwa Upande wake Naibu Katibu mkuu wa umoja huo Jesca Mbogo amesema kuwa wanawake Kote nchini wanawajibu wa kuhakikisha lishe duni inakuwa historia ndani ya mikoa yetu hadi ngazi za familia kwa kuishi kwa upendo na kuwajali wenzetu pindi tunapoona wana matatizo tuwasaidie kwa hali na mali.
Amesema kuwa tukiishi kwa mshikamano na umoja tutafikia kwenye malengo ya uzalendo utakaopelekea kuona mchango wa maendeleo kwenye taifa letu tuishi kwa kuhubiri upendo ili kuweza kuitunza amani yetu na umoja wetu kama wanawake na mwisho wa siku taifa liendelee.
Ameinyooshea kidole baadhi ya halmashauri kushindwa kutoa mikopo kwa kina mama kwa wakati hali inayowafanya kushindwa kuzichangamkia fursa za kimaendeleo hivyo kuwataka kuwapatia mikopo wakinamama na vijana kwa wakati na kuwafuta huko walipo
“Ziara hizi ambazo tumefanya semina mbali mbali kuhusiana na masuala ya Ukeketaji,Elimu,Lishe duni na Ndoa za utotoni ambazo zipo kwenye jamii yetu ili kuondoa changamoto na kuweza kuisaidia serikali kufikia malengo ya maendeleo kwani ukimueleimisha mwanamke ambaye ana usawishi mkubwa kwenye jamii utakuwa umeielimisha jamii nzima”alisema Mbogo.
Awali mbunge wa viti maalum Catherine Mgige alitoa Pikipiki Saba kwa viongozi wa umoja huo kwa lengo la kuwawezesha viongozi hao kuwafikia wananchini na wananchama hadi vijijini ambao ndio malengo ya serikali kuwafikia wananchi wa hali ya chini kuweza kuwainua kiuchumi.
Amesema kuwa pikipiki hizo ziwe chachu ya ushindi wa chama hicho kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mapema mwishoni mwa mwaka huu wakitanguliza mshikamano kama wanachama wa chama cha mapinduzi kwani umoja ni ushindi na mshikamano unahitajika bila kuyapa nafasi makundi kutugawanya.
Nae mwenyekiti wa Umoja huo mkoani hapa Jasmin Bachu amewataka wanachama wa umoja huo kutembea vifua mbele kwa kazi inayofanywa na serikali ya Awamu ya tano chini ya Dkt.John Magufuli na kujipanga kuisaidia katika kuhakikisha malengo ya serikali yanatimia na wao kama mkoa na umoja huo wamejipanga kuyasemea yote yanayofanywa na serikali hii.
Amesema kuwa wanawake wa mkoa wa Arusha wamejipanga kutekeleza maagizo yote yaliotolewa na viongzo wao wa ngazi ya taifa na kuyafanyia kazi kwa umoja wao na mshikamano na kuacha kusemana kwa kupeleka maneno upande huu na huu ambapo aliwaomba wenzao wa mikoa mingine kuja kujifunza Arusha na wao pia wataenda kujifunza kwao kwa lengo la kufikia kwenye umoja.
“Kwa dhati nisema kuwa wanawake wenzangu wa mkoa wa Arusha tumejipanga kuhakikisha umoja na mshikamano utakaopelekea ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi ujao wa serikali za mitaa ili yote mlio yasema kwenye ziara yenu viongozi wangu tutyafanyia kazi kwa vitendo na tutayaishi katika maisha yetu”alisema Bachu
Hivyo makala UWT YAWATAKA VIONGOZI KUJENGA MSHKAMANO KUTATUA KERO ZA JAMII
yaani makala yote UWT YAWATAKA VIONGOZI KUJENGA MSHKAMANO KUTATUA KERO ZA JAMII Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala UWT YAWATAKA VIONGOZI KUJENGA MSHKAMANO KUTATUA KERO ZA JAMII mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/uwt-yawataka-viongozi-kujenga-mshkamano.html
0 Response to "UWT YAWATAKA VIONGOZI KUJENGA MSHKAMANO KUTATUA KERO ZA JAMII"
Post a Comment