title : UVCCM YASEMA WANASIASA UCHWARA HAWAJIAMINI
kiungo : UVCCM YASEMA WANASIASA UCHWARA HAWAJIAMINI
UVCCM YASEMA WANASIASA UCHWARA HAWAJIAMINI
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) umesema ukuaji wa Demokrasia umetoa fursa pana kwa kila mwananchi kufanya mambo yake kwa uhuru bila usumbufu wa aina yoyote katika jamii.
Umebainisha kuwa wapo baadhi ya wanasiasa uchwara wanaokesha wakiwaaminisha na kuwapotosha Wafuasi wao kuwa Demokrasia imebinywa jambo ambalo sio la kweli kwani Demokrasia isingekuwepo hata hizo Kauli wanazotoa zisingeweza kusikika nchini. Hayo ameyasema Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar Mussa Haji Mussa katika hafla ya uzinduzi wa Matembezi ya kuyaenzi Mapinduzi ya mwaka 1964,ambapo hafla hiyo imefanyika katika Kijiji cha Chokocho Wilaya ya Mkoani Pemba.
Alisema wanasiasa wanaoilalamikia serikali kuwa imebana Demokrasia ni wale waliozoea siasa za vurugu, vitisho na migogoro ya kisiasa hivyo kwa sasa wanaona hawana tena nafasi ya kufanya matukio ya aina hiyo ndio maana wanalalamika na kueleza bila aibu kuwa Tanzania na Zanzibar kwa ujumla hakuna demokrasia na uhuru wa kutoa na kupkea habari.
Naibu Katibu Mkuu huyo wa UVCCM Mussa alisema Utekelezaji mzuri wa Ilani ya CCM ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020 umeenda sambamba na matakwa ya ASP katika upatikanaji wa huduma za kijamii na kiuchumi nchini. Amesema mbali na kuimarika kwa huduma za kijamii na kiuchumi kwa asilimia 100 pia CCM na Jumuiya zake wameendelea kuwa vinara wa Demokrasia na Utawala bora hali inayotoa fursa pana kwa wananchi wa Zanzibar kushiriki kwa uhuru katika shughuli za kimaendeleo.
NAIBU Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar Mussa Haji Mussa akisoma taarifa ya Matembezi ya kuenzi miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika Pemba.
BAADHI ya Vijana wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) Zanzibar wakisikiliza nasaha mbalimbali zinazotolewa na viongozi katika hafla ya Matembezi hayo.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala UVCCM YASEMA WANASIASA UCHWARA HAWAJIAMINI
yaani makala yote UVCCM YASEMA WANASIASA UCHWARA HAWAJIAMINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala UVCCM YASEMA WANASIASA UCHWARA HAWAJIAMINI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/uvccm-yasema-wanasiasa-uchwara.html
0 Response to "UVCCM YASEMA WANASIASA UCHWARA HAWAJIAMINI"
Post a Comment